Hukumu ya ICC yamtaja Rostam Aziz mmiliki wa Dowans!

NGOJA NISAFISHE BASTOLA YANGU SITAOGOPA HATA NIKIMPIGA MGUU YATOSHA: NIMECHOKA SANA KUSEMA BILA KUTENDA:israel:
 
Tanesco ililia na Rostam











Rostam(5).jpg

Rostam Aziz




Taarifa sasa zimevuja juu ya aina ya utetezi ya uliowasilishwa na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), kwenye kesi dhidi ya Dowans Tanzania Limited katika Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi (ICC), ambako imeamriwa kulipa mabilioni ya shilingi kwa kuvunja mkataba wa kuzalisha umeme wa dharura.
Katika utetezi wake ambao NIPASHE imeuona, Tanesco mbali ya kujenga hoja mbalimbali, iliamua kulia na Mbunge wa Igunga, ambaye pia ni mfanyabiashara maarufu nchini, Rostam Aziz, kuwa ndiye hasa Dowans.
Tanesco katika utetezi wake ilidai kuwa Dowans haijasajiliwa Costa Rica kama ilivyodai, ila mradi ni unaomilikiwa au kuendeshwa au kuhusishwa na Rostam.
Tanesco pia ilishuku barua za utambulisho wa Dowans, moja ikiwa imeandikiwa Desemba 8, 2006 na nyingine Desemba 18, 2006, zikiitambulisha kama kampuni yenye hadhi na ikiwa inatambuliwa na walau benki mbili maarufu duniani, ikiwamo Royal Bank ya Canada na CRDB ya Tanzania.
Utetezi huo wa Tanesco pamoja na mwingine, vilitupiliwa mbali na ICC na hivyo kuipa ushindi Dowans katika shauri hili ambalo liliwasilishwa kwake baada ya kuvunjwa kwa mkataba iliourithi kutoka Richmond Development Corporation.
Katika kesi hiyo, Tanesco imeamrishwa kulipa zaidi ya Sh. Bilioni 94.
Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, juzi aliwaambia waandishi wa habari kuwa kiwango kinachotakiwa kulipwa kwa Dowans ni Dola za Marekani 63,812,630 sawa na Sh. Bilioni 94 na si Sh. Bilioni 185 kama ambavyo imekuwa ikiripotiwa na vyombo vya habari.
Katika hukumu ya ICC pia utetezi mwingine wa Tanesco ulijiegemeza kwenye ubatili wa kubadili mkataba wa Richmond kwenda Dowans kwamba ulikiuka sheria.

Source: Nipashe Jumapili (IPPMedia) 01-09-2011 Jumapili
Hivyo usalama wa Taifa, msururu wa wanaharakati, wanasheria waliobobea, Wapiganaji wa ufisadi na hata Waheshimiwa wetu wabunge walishindwa kuutowa ushahidi kuthibitisha maovu ya mtu mmoja? Au pengine ule msemo wa penye kweli uongo hujitenga?

Pengine hili linaweza kuwa funzo kwetu kwa kuendesha mambo yetu kwa maneno ya wanasiasa wenye maslahi yao binafsi.

Hili liwe funzo
 
Wananchi Kweli JK Akilipa Dowans Tutapigana Tanzania. JK Wana Cover Up Dowans na Kaharakisha Kuwalipa. Haiwezekani na Hata Mara Moja HATUTAKUBALI. Check ya Kwanza Ikilipwa Dowans Tunataka Inform. na Tutakuwa na Maandamano Taifa Zima. Nafikiri CCM Hawatuelewi Watanzania, Wamewaonea Wazazi Wetu na Sasa Wanataka Kutuonea Sisi Pia. "This is It"

Kwa maneno naam!
 
Ngoja nitafute pesa ninunue kijenereta cha kuendesha tv yangu kuanzia february 8. Labda historia ya February 2008 itajirudia
 
Wanaojua maana ya uhuru hawatoshangaa kwamba ni nani nchini Tanzania ambaye hajui kama uhuru haupo siku nyingi.

Lakini kwa wale ambao kwao uhuru maana yake ni kupokea nyaraka kutoka Langcaters House huko miaka ya 60 halafu ndio basi wala hawatokaa waelewe Watanzania tunaposema tunapigania uhuru wa kweli. Ila kwa swali lako inamaanisha kwamba uhuru wa

1. kutoa maoni na hisia kama ilivyoandikwa kwenye katiba yetu ni ruksa na wala hauawi mtu kwa ajili hiyo.

2. Uhuru wa kuchagua kiongozi tunayemtaka ni shwaari wala hamna uchakachuaji.

3. Haki ya ibada bila kulazimisha maoni na au ibada za kikundi kufanywa teule wala sio shida.

4. Uhuru wa kutokubaguliwa kwa misingi ya itikadi za kidini, kisiasa, kijinsia au umri haina adha kwako.

5. Uhuru wa kujumuika pamoja na nyingine nyingi tu sio shida

Kwangu mimi UHURU si kumbadili Mzungu na kuweka rangi nyeusi tu na kukabidhiwa bendera bali UHURU ni mpaka kuonekana kwepo na kuhisiwa kwepo wakati wote.

Ulishawahi kuwepo kwa vigezo vyako?
 
oooooh,naona tujadili tutaandama lini kupinga hao watu kulupwa kuliko kuendelea kupeana sintojua za nani mmiliki wa dowans
 
Rostam AZIZ, jamaa lenyewe jizi kufa halifi, wanakufa tu watu wema na wanaotanguliza maslahi ya taifa mbele, kama CHACHA WANGWE NA FARRES KABUYE.
 
Yaani hata ICC wameona kuwa kukazania umiliki wa Dowans ni wa Rostam ni upuuzi mtupu.

Au ICC nayo iko kwenye himaya yake? umewashuka!

NO DOUBT! YOU ARE ONE OF THEM........OUR NATION ENEMY (ENZI ZA MWALIMU WAHUJUMU UCHUMI) :sad:
 
Haki ya watanganyika itasimama. Kufanywa wajinga kuna mwisho wake.

Mtanganyika ni wewe ambaye bado unaishi kwenye ujima.

Sisi ni Watanzania, na tupo makini.

Utaendelea kuwa mjinga tu manake unang'ang'ani utanganyika.

Mmelogwa nyie watu wa hiki chama?
 
Mkataba wa Dowans umevunjwa makusudi kabla ya miezi mitatu kumalizika !!!! Kwa nini? hizo ndo dili za bongo. hayo mabango ya kampeni yatalipwaje? haa Tanzania yangu wee!!!!!!! wajanja wanakula nchi na vikaragosi vinajiita usalama wa taifa, i mean usalama wa CCM vimefyata mkia hapo kijitonyama.
,
 
MI NAULIZA TUU JAMANI KWANI DOWANS WAMEIWEKA SERIKALI MIFUKONI MWAO KWA KIASI GANI??????????????????????:faint:
 
Wananchi Kweli JK Akilipa Dowans Tutapigana Tanzania. JK Wana Cover Up Dowans na Kaharakisha Kuwalipa. Haiwezekani na Hata Mara Moja HATUTAKUBALI. Check ya Kwanza Ikilipwa Dowans Tunataka Inform. na Tutakuwa na Maandamano Taifa Zima. Nafikiri CCM Hawatuelewi Watanzania, Wamewaonea Wazazi Wetu na Sasa Wanataka Kutuonea Sisi Pia. "This is It"

Hello wanaJF,

Haswa wewe umenena. Bila shaka siku hundi hiyo ikilipwa, sisi tuanze kujibinafsisha hizo kampuni zake 17 alizozitaja Waziri S. Lakini, hiyo mosi, pili hii hapa: Kwanini Bwana huyo "Mjanja" alisema sihusiki na Dowans na siku 2 baadaye Serikali ikatoa Tamko? Hivi hapo hatuwezi kuona kuwa kulikuwa na majadiliano ya mezani kati ya hao wawili kabla ya tamko la serikali? Kama sivyo, kwanini siku zote hizo, sisi huyo Bwana wala Serikali ilitaja majina ya wamiliki wa Dowans? Kwanini wafuatane kujibu hoja za Dr. Slaa?
 
Watanzania sijui tuna matatizo gani...Ndio maana watawala wanatumia matatizo tuliyo nayo kutukandamiza. baada ya mwaka ishu ya downans zitasahaulika na yatakuja madowans menginena sikuya uchaguzi tuna kauka makoo kuwashangilia eti CCM oyee
 
Rostam is damn smart he is orchestrating the whole ruling system....Hebu angalia connection iliyopo kati ya dowans, Ngereja, Vodacom,karamagi,...isee huyu jama is very powerful hapa bongo.....Nakubaliana kabisa na jamaa anayesema atamuua peke yake kwa mikono yake bila silaha pindi revolution itapokuja
 
Back
Top Bottom