Sasa sijui wewe unafuata mkumbo au ndio Chadema-Kata..Chadema hii ni janga la taifa juzi tena tumeona wamedakia suala la mgomo wa madaktari na kutaka kuligeuza liwe mtaji wao wa kisiasa wa kujinadi na kusikika kwa wananchi wakati inajulikana na wote kwamba mgomo ni suala la kikazi linalohusu maslahi na kwa hiyo ufumbuzi wake ni kati ya mwajiriwa na mwajiri wake, kama ni mjadala utakuwa baina ya pande mbili zinazohusika mwajiri na mwajiriwa hakuna upande wa tatu wa aidha bunge ama chama cha siasa, lakini Chadema hasa akina Mnyika na Mbowe na Slaa walitaka mgomo ujadiliwe bungeni.
Polisi wa nchi gani unawazungumzia? Kama ni polisisiemu basi utakuwa na wewe umechanganyikiwa kama Mwigulu. Mbona huelezi gari lililokamatwa na kura hewa Mkoani Mara zote zikiwa zimeshapigiwa kwa mgombea wa ccm zilikwenda wapi? Wewe ni kama hujifahamu wenzako wakishakutumia watakavyo wanakutupa kama toilet paper au ndoo zitumikazo ktk ujenzi.Hizi si tuhuma za kwanza za Dr Slaa kwa usalama wa taifa mwaka 2010 alisema usalama wa taifa kushirikiana na tume ya uchaguzi imeingiza makontena ya kura za bandia kutoka Afrika Kusini polisi walipoyakamata hayo makontena wakayafungua mbele ya viongozi wa Chadema na kubainika hayakuwa na kura bandia bali ni Vipodozi! Viongozi wa Chadema wakaonekana waongo na wazushi.
Nini kilimtuma kwenda kwenye mkutano usiomhusu na kuanza kurusha mawe? Kipi kilistahili kujadiliwa bungeni katika ya mgomo wa madaktari na huyu mrusha mawe? Au Mwigulu na ugonjwa wake wa akili ni wa mhimu sana bungeni kwa vile anatoka chama cha mabwepande? Huna hoja wewe na uache machozi ya mamba, pokea fedha haramu ya Nape kwa kazi haramu ya kutetea machinjachinja na mafisadi wa mabwepande kioja we!
Profesa mkuu wangu,Kweli CCM ina madudu na uozo mwingi tu kwa sababu ambazo wote tunazijua, kulewa madaraka kwa viongozi wake wapumbavu, maana si wote werevu ingawa wapo ambao ni wazuri sana ambao kwa sasa wanawakati mgumu kukookoa chama kutoka mikononi mwa wapumbavu wachache wanaokiletea sifa mbaya chama na kushabikia ujinga.
Isipokuwa, mashabiki wote w CHADEMA humu ndani mmenisikitisha saaaaana sana, ninajua mnazungumzia ushabiki wa kisiasa ila, hakika ninawaambia, kama hamtafuata falsafa ya hoja na kujenga hoja na kupangua hoja kwa busara na uwerevu wa kipimo kinachoheshimika, basi haya mnayofanya katika majibu yote hapo juu pamoja na hasira, mwenye kujua naweza akapima, ni aibu tupu. Sitaki kukubali kuwa mnawakilisha mawazo ya CHADEMA bali yenu wenyewe. Msisahau, mimi ni CCM, lakini sisiti kukosoa viongozi wa CCM hasa pale ambapo siridhishwi na mambo fulani.
Mimi nitafurahi CHADEMA wakichukua nchi, ila hofu yangu kubwa ni kama jinsi mnavyojadili hoja humu ndio mlivyojipanga, basi si Bungeni wala serikalini kitaeleweka, maana kama mnajibu watu kwenye siasa hivi, hata ndani ya serikali kwenye maswala nyeti sitashangaa majibu yakawa haya. Onysheni mfano watu tuone wivu na tuvutiwe kwa jinsi mnavyowaza na kupangua hoja.
BADILIKENI!
aaaaaaaaaaaaaahhhhhhhhh!! mma j'amaa leka aamahelu, ukulile lino, keta kutuka bo bajanga, nungwe ulijanga!!!!!!!!!!! leka amahelu , ulikusiGwe kinyelo kya nguku!!
Mkuu wangu hawa Chadema kama unakumbuka walianza kufanya maandamano ya ajabu yenye lengo la kuvamia kituo cha polisi mjini Arusha kilichokuwa na silaha za moto, haijulikani kama azma yao ingefanikiwa sijui ingekuaje.
Hawa ndio wana Chadema wanataka tuwakabidhi nchi watutawale.....
:A S-baby: Umetumwa leo ulete ujinga wako hapa? Vyombo vya dola ndivyo vinatuhumiwa kuua raia wema badala ya kuwalinda, kwa hiyo dola inaweza kuaminiwa kwa hayo inayofanya? You must be fool.Wanabodi,
Baada ya kuja na mbinu za kisiasa tofauti tofauti hatimaye Dr Slaa, kaja na mbinu mpya ambayo ni harakati bila mikatati na mbinu dhaifu.
Dr Slaa sasa kaanza mkakati wa kutaka aonewe huruma na wananchi kutokana na kile anachokiita kufuatwafuatwa na vyombo vya dola kwa ni ya kutaka kumuua, inashangaza Dr Slaa kubadili mwelekeo wa siasa zake za kutaka nchi isitawalike na kuomba huruma kwa wananchi.
Neno kutaka kuniua ni zito sana ni jinai ndio maana mtu akitishiwa kuuwawa anakimbilia polisi kutoa taarifa na kupatiwa RB. Hakuna aliyeko juu ya sheria ambaye anaweza kumtishia kuua kiongozi kama Dr Slaa halafu akaachwa tu eti yeye ni usalama wa taifa.
Dr Slaa anasema hana imani na taasisi za dola, huyo huyo anayelilia kutaka kwenda Ikulu sasa akifika huko atafanya kazi na taasisi gani, Itakumbukwa mwaka 2010 Dr Slaa aliwangoza viongozi wa chama chake kupinga matokeo ya urais lakini wakikubali matokeo ya ubunge na udiwani. Alikuja na msamiati wa kuchakachuliwa kura zake bila ushaidi.
Dr Slaa kama hana imani na uongozi wa rais Kikwete ilikuaje yeye pamoja na viongozi wenzake kuwa watu wa kwanza kwenda Ikulu kuonana na rais Kikwete katika mchakato wa katiba...hivi Dr Slaa kweli hujui kwamba hii amani na utulivu tunayojivunia Watanzania tangu tupate uhuru wetu inatokana na uimara wa taasisi zetu za dola.
tunajua watu tuna vyama vyetu vya siasa,ni haki ya msingi lakini kuwa na vyama au shabiki wa vyama husitufanye kuwa mazezeta wa kufikiri. Hivi we ndugu issue ya kutishiwa kuuwawa umeanza kuisikia kutoka kwa dr slaa? Hebu turudi nyuma kidogo tuone jinsi nchi yetu ilivyogeuka kuwa ya kijambazi na kitekaji, leo hii tanzania imefikia hatua mtu ambaye ni waziri katika serikari anatoa tuhuma na ushaidi wa kutaka kuuwawa.huyu ni waziri kaka hukumbuki dr mwakyembe alivyolalamika?vipi umesahau issue ya samweli sitta? Hatua gani jeshi la polis limefikia? Juzi mke wa dr mwakyembe akitoa mchango wake kwa kanisa kama sehemu ya shukurani kwa mungu anasema "wamewasamehe waliotaka kumuua dr" vipi kauli hii ni kwamba mh waziri na familiya yake wanawafahamu waliotaka kumua .sasa huyu ni waziri anawafahamu wauaji lakini hana jinsi hawawezi kushughulikiwa alafu unasema dr slaa anatafuta huruma.wanabodi,baada ya kuja na mbinu za kisiasa tofauti tofauti hatimaye dr slaa, kaja na mbinu mpya ambayo ni harakati bila mikatati na mbinu dhaifu.dr slaa sasa kaanza mkakati wa kutaka aonewe huruma na wananchi kutokana na kile anachokiita kufuatwafuatwa na vyombo vya dola kwa ni ya kutaka kumuua, inashangaza dr slaa kubadili mwelekeo wa siasa zake za kutaka nchi isitawalike na kuomba huruma kwa wananchi.neno kutaka kuniua ni zito sana ni jinai ndio maana mtu akitishiwa kuuwawa anakimbilia polisi kutoa taarifa na kupatiwa rb. Hakuna aliyeko juu ya sheria ambaye anaweza kumtishia kuua kiongozi kama dr slaa halafu akaachwa tu eti yeye ni usalama wa taifa.dr slaa anasema hana imani na taasisi za dola, huyo huyo anayelilia kutaka kwenda ikulu sasa akifika huko atafanya kazi na taasisi gani, itakumbukwa mwaka 2010 dr slaa aliwangoza viongozi wa chama chake kupinga matokeo ya urais lakini wakikubali matokeo ya ubunge na udiwani. Alikuja na msamiati wa kuchakachuliwa kura zake bila ushaidi.dr slaa kama hana imani na uongozi wa rais kikwete ilikuaje yeye pamoja na viongozi wenzake kuwa watu wa kwanza kwenda ikulu kuonana na rais kikwete katika mchakato wa katiba...hivi dr slaa kweli hujui kwamba hii amani na utulivu tunayojivunia watanzania tangu tupate uhuru wetu inatokana na uimara wa taasisi zetu za dola.