Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 15,280
- 9,719
Ndugu zangu Watanzania,
Haihitaji akili kubwa sana wala shahada ya chuo kikuu wala kusubiri kuambiwa wala kupewa ufunuo katika kutambua kuwa Dr Slaa Ni mtu ambaye kifua na moyo wake unaonyesha kuwa na chuki kubwa sana na Rais wetu Mh mama Samia Suluhu Hasssan. Ukisikiliza maneno ya Dr Slaa kwa nyakati na vipindi tofauti tofauti wakati huu wa Urais wa Rais Samia unaona wazi kabisa kuwa kaelemewa na hasira,kinyongo na maumivu makubwa ndani ya moyo wake dhidi ya Rais Samia.
Jaribuni ndugu zanguni kufuatilia maneno ,matamshi ,kauli , mazungumzo na hata matendo ya Dr Slaa miaka mitano iliyopita na Dr Slaa wa wakati huu wa Rais samia, ili muelewe hiki nachokiandika hapa kuwa Dr Slaa kuna jambo linamsumbua sana moyoni na akilini mwake.amebeba mzigo wa maumivu ,maumivu yakuona Rais Samia akifanikiwa kwa kiasi kikubwa na kuungwa mkono na mamilioni ya watanzania tofauti pengine na matarajio yake yeye mwenyewe.
Sasa maumivu hayo yameshindikana kutunzika katika moyo na kifua chake na sasa kaamua kutoa sauti yake.sasa anawapangia watu mambo ya kusema,sasa hataki na anaumia sana anapoona watu wakimponge Rais Samia.hataki watu wafanye hivyo maana anaumia.hataki vijana kwa maelfu yao wampongeze Rais samia baada ya kupata ajira baada ya kusota mitaani kwa miaka mingi,hataki wakulima wanaoendelea kuneeemeka na mbolea za Ruzuku pamoja na bei nzuri za mazao wampongeze Rais samia kwa juhudi zake za kuinua kilimo na mkulima.
Hataki wazazi wampongeze Rais samia baada ya kuwatua mzigo wa kulipa ada kama walivyokuwa wanafanya awali,hataki vijana wa vyuo vikuu wampongeze Rais samia baada ya kuwa sasa wote wenye sifa wanapata mikopo bila shida yoyote ile,hataki watumishi wa umma wampongeze Rais samia baada ya kuongezewa mishahara kwa 23% hasa wale wa kima cha chini baada ya kusota wakisubiri kwa miaka mingi,hataki watumishi ambao sasa wamepandishwa madaraja,kulipwa malimbikizo ya madeni na kupewa nyongeza ya mshahara kila mwaka wampongeze Rais samia.
Dr Slaa hataki na anaumia sana anapoona wafanyabiashara wakimpongeza Rais samia kwa kuweka mazingira mazuri ya biashara na uwekezaji,Dr Slaa hataki kuona Rais Samia akipongezwa kwa kuiheshimisha nchi yetu kimataifa mpaka sasa tumerudishwa kwenye mpango wa millenium challenge huku miradi ya maendeleo ikiendelea kutekelezwa kila kona ya nchi yetu.
Sasa kwanini Dr Slaa hataki tumpongeze Rais wetu? Kwanini anaumia sana? Mbona awali alikuwa mtoa sifa na pongezi mzuri sana na alituasa hata watanzania kupongeza juhudi na kazi kubwa sana iliyokuwa ikifanywa na serikali ya awamu ya tano? Kwanini leo iwe kama kosa au jinai kumpongeza Rais samia kwa kazi kubwa na uchapa kazi wake uliotukuka ulioliletea maendeleo makubwa Taifa letu ndani ya muda mfupi?
Anataka nini Dr slaa? Kwani yeye anatakaje? Anataka tuseme nini pale Rais wetu anapofanya vizuri?
Napenda kusema na kumwambia Dr Slaa kuwa Rais Samia ni mpango wa Mungu Mwenyewe,hakuinuliwa kwa mkono wa mwanadamu bali na mkono wa Mungu Mwenyewe,hivyo hawezi kushushwa na mikono wala maneno ya mwanadamu mwenye chuki zake binafsi. Atapambana sana lakini hataweza kumshusha mama yetu.ukiinuliwa na Mungu mwanadamu hawezi kukushusha.ukipewa kibali na Mungu mwanadamu hawezi kukuzuia kupita na kukubalika mahali popote pale.Mungu yupo upande wa Rais Samia na Anaendelea kumpatia njia na maarifa ya kuongoza Taifa letu.
Uzuri wa Rais wetu yeye hakatishwi tamaa wala kunyong'onyeshwa na maneno au chuki ya mwanadamu .siku zote yeye hutizama mbele kwa matumaini na ujasiri wa hali ya juu katika kuyakabili matatizo na Changamoto mbalimbali ili kuwatua mizigo Watanzania.
Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel mwashambwa Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.
0742- 676627.