FT| NBC | Namungo 1-1 Simba Sc | Majaliwa Stadium | Mei 3, 2023

ntazana ntazana

JF-Expert Member
Sep 18, 2021
1,707
3,020
Mechi ni saa 1 usiku

Kuna mabadiliko makubwa kwenye kikosi cha leo na kile cha mwisho kilichocheza kule Morroco

Pamoja na hoja ya kuwapumzisha wachezaji lakini mtu kama Moses Phiri kukosekana hata benchi kunaongeza maswali.

Kibu D naye mechi hii kaikosa.

simbasctanzania_20230503_p_3094608320035627932_1_3094608320035627932.jpg

LIGI KUU: SIMBA YASHIKWA, YAZUIWA KUIKIMBIZA YANGA KWENYE UBINGWA
Simba imeshindwa kuikimbiza Yanga katika mbio za kuwania ubingwa wa Ligi Kuu Bara Msimu wa 2022/23 baada ya kutoka sare ya goli 1-1 dhidi ya Namungo FC kwenye Uwanja wa Majaliwa, Lindi.

Kwa matokeo hayo Simba imebaki nafasi ya pili ikiwa na pointi 64 katika mechi 27, nyuma ya #Yanga yenye pointi 68 katika mechi 26 wakati NamungoFC ipo nafasi ya 6 ikiwa na pointi 36 kwenye mechi 27.

Goli la Simba limefungwa na Jean Baleke dakika ya 27 kisha Hassan Kabunda akasawazisha katika dakika ya 39.

FvOKiVpXwAIdJfd.jpg
 
Back
Top Bottom