CHADEMA yawa gumzo Mtwara

Point ya maana kwako ikoje? Haya sio maneno yangu ni maneno ya Mbunge wa Chadema Nassari ndio alisema Chadema kujitenga mie utanionea bure labda ungemwambia mbunge wako.

Halafu mie naitwa Ritz wa JF hayo mambo yenu ya kupeanda vyeo vya kinafiki eti great thinkers wala mie siitaji mkuu wangu itaneni tu nyie Pro-Chadema JF.
afadhali umekiri kuwa sio great thinker hilo limenionyesha uwezo wako wa kufikiri ni mdogo nimekusamehe! Swala la Nassary lilishatolewa maelezo na mh. Mbowe na yeye mwenyewe Nassary kwenye press conference lakini wewe kulileta hapa kiushabiki ndio maana nimekuambia ongea point ya maana! JF ni mahali pa fikra pana na mjadala mtambuka na ujenzi wa hoja sio ushabiki wa kwenye magazeti ya udaku!
 
Jambo lipo dhahiri, kwamba CHADEMA watalazimika kufanya kazi ya ziada ili waweze kukubalika maeneo ya pwani! Iwe ni matunda ya propaganda au vinginevyo, tayari taswira ya CHADEMA machoni mwa watu wengi haioneshi utaifa kama ilivyo kwa CCM! Inawezekana kabisa kwamba CCM kikaonekana ni very CORRUPT, lakini linapokuja suala la muonekano wa kitaifa, CCM is far better than CHADEMA and even CUF!

Hili, halikuja kwa bahati! Ni dhahiri kwamba, propaganda za CCM zimesaidia kujenga taswira hiyo ya CHADEMA kuonekana enzi zile kwamba ni chama cha Wachaga, ikaja kuwa cha Kikristo na sasa cha kikanda! Kwa bahati mbaya sana, ama kwa makusudi ama kwa ukosefu wa weledi wa kile kinachosemwa "Think All Before You Speak, But Don' Speak All Before You Think", imetokea mara kadhaa kauli za viongozi wa CHADEMA kuleta mshabihiano wa yale yanayosemwa na wapinzani wa CHADEMA!! Mbaya zaidi, kosa ambalo lilitokea kwa CUF limerejea CHADEMA! Wakati CUF kikituhumiwa kwamba ni Chama Cha Waislamu, ikatokea Waislamu wengi wakajiunga na Chama hicho na tangu hapo hata mamo ya CUF yakakaa Kiislamu Islamu! Ilikuwa ni jamo la kawaida kwenda kwenye mikutano ya CUF na kukuta full Barkhashia!! Hivyo hivyo, wapo Watanzania wengi tu hivi sasa ambao wanajikuta wanaiunga mkono CHADEMA kwa ajili tu ya Ukristo wao! Hata hapa JF, ukiangalia Wakristo ambao wamekubuhu kwa udini, utakuta ni watetetzi wakubwa wa CHADEMA! Si hilo, utakuta members wengi humu JF ambao Signatures zao ni vifungu vya Biblia, basi wengi wao kama sio wote ni watetezi wakubwa wa CHADEMA! Mara nyingi member hawa hata michango yao utakuta inaegemea zaidi kwenye udini udini kuliko Siasa za kawaida hata kama hoja inayojadiliwa ni ya kisiasa! Members hawa, wanatia kinyaa na wanachangia kwa kiasi kikubwa kuifanya CHADEMA ionekane dhahiri ni chama cha Wakristo!

Harakati za CHADEMA nazo zinazua mashaka mengine! Hata uendaji wa Kusini hivi sasa unaonekana ni kama tu katika kuzima kelele za wapinzani wao kwamba CHADEMA ni chama cha kikanda na chama cha Wakristo! Mbwembwe za CHADEMA kwenda kusini hazijaanza leo….na hata kama wataenda bado hawana hamasa kiasi hicho! Molemo, ametuletea habari za gazeti la Majira…..CHADEMA tuliowazoea si wa kusuiri Majira waandike stori kisha waje hapa kui-paste! Safari, imekosa hamasa!

Kama ilivyo ugumu kwa CUF kukubalika Bara ndivyo hivyo hivyo CHADEMA watakavyopata ugumu wa kukubalika Pwani ingawaje wapo wapumbavu watakaosema kwamba watu wa pwani hawana uelewa! Yaani leo hii Mmasasi ambae anaishi kwa kuhamahama awe na uelewa kuliko mtu aliye-settle sehemu moja!
 
Point ya maana kwako ikoje? Haya sio maneno yangu ni maneno ya Mbunge wa Chadema Nassari ndio alisema Chadema kujitenga mie utanionea bure labda ungemwambia mbunge wako.

Halafu mie naitwa Ritz wa JF hayo mambo yenu ya kupeana vyeo vya kinafiki eti great thinkers wala mie siitaji mkuu wangu itaneni tu nyie Pro-Chadema JF.

Ukitofautiana sana na watu basi mwisho wa siku lazima utakuwa na matatizo... Kama ukiona katika watu kumi 8 au 9 wanakupinga basi ujue hayo mawazo yako hayafai... Najua inawezekana wewe hili unalielewa lakini kwa sababu ya maslahi binafsi unashindwa kufanya maamuzi sahihi.
 
Ukweli unaumaaaaaa......
Wachaga wana ubaguzi xana!!!!! Hata marehem baba yangu pale Mikindani aliniambiaaaa..... CDM hamtaweza kukubalika milele!!!!!!

Pili huku kuna waislam tupu, na ule udini mmechemka!!!!! Niko huku Lipwidi, Mtwara Vijijin nalimaaaa!!!!

kama kweli unaishi Lipwidi basi unamatatizo makubwa kwenye kufikiri.Uchaga sio Ugonjwa ni Kabila ambalo anazaliwa anakuta wazazi wake wanalo.Mbona Mtwara kuna M bunge Viti maalumu Mama Wambura ni Mkulya.Upoandika jamvini usifikiri Mtu wa Mtwara uko peke yako ili udanganye watu humu.
 
Tunakumbushi mlichokisema na end result yake! na mtwara itakuwa hivyo hivyo...
Kwa watu wanaolewa mwenendo wa CDM na uducteta uliopo, hawawezi kukishobokea CDM.
Am happy watu wa Pwani ni waelewa na wanajua kupima mambo kabla ya kukurupukia vitu!

Hivi uducteta ndio nini?
 
Hata Uzini ilikuwa hivi hivi..
Natafuta comment ya Slaa hapa JF siku wawalipoenda Uzini.
Nafikiri wote mliona CDM walichoambulia kule!!

usichanganye mambo UZINI ilikuwa wakati wa uchaguzi,alafu huko tunajua kuwa kuna mahusiano ya kiutawala kati ya CUF na CCM .CHADEMA wanakuja kukiimarisha chama Kusini.Karibuni sana CHADEMA.
 
Tunakumbushi mlichokisema na end result yake! na mtwara itakuwa hivyo hivyo...
Kwa watu wanaolewa mwenendo wa CDM na uducteta uliopo, hawawezi kukishobokea CDM.
Am happy watu wa Pwani ni waelewa na wanajua kupima mambo kabla ya kukurupukia vitu!

wewe unatudhihaki sisi watu wa Pwani unatuöa ni Maamuma tu,hutoamini kitakachotokea Mtwara.
 
Ukitofautiana sana na watu basi mwisho wa siku lazima utakuwa na matatizo... Kama ukiona katika watu kumi 8 au 9 wanakupinga basi ujue hayo mawazo yako hayafai... Najua inawezekana wewe hili unalielewa lakini kwa sababu ya maslahi binafsi unashindwa kufanya maamuzi sahihi.

Jambo la msingi ni hoja na sio idadi ya watu!! Wajuzi wa mambo huku Uswahilini wanatuambia kwamba nyani mmoja ana akili nusu ya ile aliyonayo binadamu; lakini haimaanishi kwamba pakiwepo nyani 72 ndo watakuwa na akili 36, la hasha....bali ni ile ile nusu!!

Si hivyo, ukiangalia sana basi utagundua kwamba kitu ambacho kinashabikiwa na wengi basi kina walakini! KWANINI?! Wanadamu huwa hatuna silika ya kuumiza kichwa na kutafuta ukweli na badala yake tunalazimika kukikubali kile kilicho rahisi kwetu kukimeza au kile ambacho wahubiri wake wakuu wana uwezo wa kuteka hisia za wengi! Angalia suala la uwepo wa mungu.....wengi tunaamini, lakini ukilitafakari "crtically" unakutana na walakini kibao!! Tunaogopa kuhoji critically kwavile tunaambiwa tutakufukuru kwa kumchimba chimba yule (mungu)tunayemwamini!

Therefore, achana na udikteta wa fikra....acha watu wafikirie vile wanavyoamini ni RIGHT na sio wafikirie vile amavyo wewe na wenye imani kama yako mngependa wengine wote wafikirie!
 
afadhali umekiri kuwa sio great thinker hilo limenionyesha uwezo wako wa kufikiri ni mdogo nimekusamehe! Swala la Nassary lilishatolewa maelezo na mh. Mbowe na yeye mwenyewe Nassary kwenye press conference lakini wewe kulileta hapa kiushabiki ndio maana nimekuambia ongea point ya maana! JF ni mahali pa fikra pana na mjadala mtambuka na ujenzi wa hoja sio ushabiki wa kwenye magazeti ya udaku!

Wewe kweli kauzu yani ukiwa mshabiki wa Chadema humu JF ndio great thinkers halafu kazi yako ni kuisifia Chadema ndio unakuwa unaongea pointi?
 
Ukitofautiana sana na watu basi mwisho wa siku lazima utakuwa na matatizo... Kama ukiona katika watu kumi 8 au 9 wanakupinga basi ujue hayo mawazo yako hayafai... Najua inawezekana wewe hili unalielewa lakini kwa sababu ya maslahi binafsi unashindwa kufanya maamuzi sahihi.

Mkuu mie sio mtumwa wa akili nasimamia mawazo yangu...halafu nakukumbusha JF sio mali ya Chadema ni jukwaa huru.
 
Mkuu mie sio mtumwa wa akili nasimamia mawazo yangu...halafu nakukumbusha JF sio mali ya Chadema ni jukwaa huru.

Mkuu wangu unajaribu kuukimbiza upepo.Maoni ya wadau ndani ya JF ndiyo uthibitisho tosha M4C haikamatiki tena.Count my words!
 
Huu ndio uzuri wa kuanza na Mungu na kutenda kazi kwa kumshirikisha Mungu.
Wao wana wakuu wa Wilaya, wakuu wa Mikoa, wana Jeshi ila sisi tuna Mungu!!!!
Duh njema sana hiyo.....!!!!
 
Mkuu wangu unajaribu kuukimbiza upepo.Maoni ya wadau ndani ya JF ndiyo uthibitisho tosha M4C haikamatiki tena.Count my words!

Mkuu wangu Tanzania kuna watu zaidi ya milioni 40 JF kuna members 70,000 na kuna zaidi ya Multiple ID's 40,000 Members hai unaweza kukuta wapo 20,000 tu Chadema wape members 15,000 hawa ndio wanawawakilisha Watanzania milioni 45? Ha haa haaa haaaa haaaaaa!
 
Mkuu wangu Tanzania kuna watu zaidi ya milioni 40 JF kuna members 70,000 na kuna zaidi ya Multiple ID's zaidi ya 40,000 Members hai unaweza kukuta wapo 20,000 tu Chadema wape members 15,000 hawa ndio wanawawakilisha Watanzania milioni 45? Ha haa haaa haaaa haaaaaa!

Mkuu wangu moja na moja huwa mbili.Nakuhakikishia CDM haikamatiki tena.Mlizoea kuwadanganya vijana sasa wamebadilika wanataka mageuzi.Ritz nikuambie kinachoipeleka CDM Ikulu ni kushindwa kwenu kuboresha maisha ya watanzania.Ni hilo tu.Kila leo ni afadhali ya jana.Watu wanaishi maisha ya shida.Tembea vijijini uone.CDM sasa imebaki ndiyo tegemeo lao pekee.Ni kama mtu anayekata roho atakavyofurahi akipata mponyaji.Na ndivyo kwa watanzania sasa kwamba kwa maisha yao ni sawa na watu wanaokata roho na mponyaji wao ni CDM.Porojo hazina nafasi tena kama CCM mnavyotaka iwe.
 
Kwa hali kama hii nani ataendelea kuishabikia CCM!

[h=3]UBOVU WA BARABARA YA KWENDA MTWARA[/h]

Gari Toyota Fuso likiwa limenasa katika tope kwenye Barabara ya Kilwa eneo la Ndundu Somanga hivi karibuni, barabara hiyo imeharibika vibaya kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.
 
You are not among GT which means I will never argue with you!

Ndo tatizo lenu hilo pro-CHADEMA, GT ni yule anaewaza ki-CHADEMA CHADEMA hata kama anachokiongea hakina mashiko!! Kwenu nyinyi, GT ni yule anayeshikiwa akili zake na wapiga proganda za kisiasa hususani CHADEMA! For the second time, YOU'RE VERY WRONG!! Am Free Thinker Broda, check out my Signature!!!!
 
Back
Top Bottom