CHADEMA yawa gumzo Mtwara

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,225
Wakazi wa manispaa ya Mtwara wamepokea kwa furaha kubwa taarifa za ujio wa CDM katika mikoa ya kusini.Wananchi mbalimbali waliohojiwa wamesema wamekuwa wakiisikia CDM kupitia vyombo mbalimbali vya habari na hasa mambo makubwa wabayofanya viongozi wake Dr Slaa,Mbowe na wabunge wa chama hicho.Wameapa kukipokea kwa kishindo chama hicho huku wakiapa kurudisha kadi za CCM na kusimika bendera za CDM mpaka ndani ya vyumba vyao.Mzee mmoja akiongea kwa uchungu alisema anaamini CDM itawakomboa na vuguvugu lao la M4C hasa katika zao la korosho.Ameahidi mikoa ya kusini kuwa ngome kuu ya CDM kama mikoa ya kanda ya ziwa na kaskazini.
Source:Majira Jumanne

------------------------------------------------------------------------
UPDATES.....1

Mkurugenzi wa habari na uenezi-CDM John Mnyika ametangaza rasmi operesheni ya M4C kwa mikoa ya kusini itaanza tarehe 28/05/2012 na itadumu kwa wiki mbili ambapo maelfu ya wananchi wanatarajiwa kuvua Gamba na kuvaa Gwanda.

-------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------
UPDATES...2

MBOWE, SLAA KUONGOZA OPERESHENI KUSINI

Awamu mpya ya operesheni ya Chadema inayolenga kuhamaisha umma kuleta mabadiliko na uwajibikaji serikalini iliyopangwa kufanyika katika mikoa ya Kanda ya Kusini, itaanza rasmi Mei 28, mwaka huu, katika Mkoa wa Mtwara.

Akizungumza na NIPASHE jana, Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa Chadema, John Mnyika, alisema operesheni hiyo itaongozwa na Mwenyekiti wa chama hicho Taifa, Freeman Mbowe.

Alisema wengine watakaoongoza operesheni hiyo, ni Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Willibrod Slaa pamoja na wabunge wa chama hicho na kwamba, itahitimishwa katika mkoa wa Lindi.

Kwa mujibu wa Mnyika, operesheni hiyo imelenga kushughulikia mambo matatu; la kwanza likiwa ni kusimamia uwajibikaji katika ngazi zote za serikali, ili kuhakikisha changamoto zote zinazolikabili taifa zinashughulikiwa.

Mnyika ambaye pia ni Mbunge wa Ubungo, alisema jambo la pili litakaloshughulikiwa na operesheni hiyo, ni kutoa elimu ya kisiasa kwa umma kuhusu mchakato wa mabadiliko ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Alisema jambo la tatu, litakuwa ni kujenga organaizesheni ya chama mijini na vijijini katika mikoa hiyo.


Source:Nipashe Jumanne.


-----------------------------
More Updates

Makamanda wa CDM wakiongozwa na Mwenyekiti Freeman Mbowe na Katibu Mkuu Dr Wilbroad Slaa wameondoka leo kuelekea mikoa ya Mtwara na Lindi kwa operesheni itakayotikisa ukanda wote wa kusini.Jumla ya makamanda wote walioondoka ni 60 ambapo watasambaa vijiji vyote kufungua matawi, ofisi za chama kata mbalimbali,kutoa elimu ya uraia kuhusu katiba na kuhutubia mikutano kila kata na kijiji.
 
hawa si ndio wale wako radhi kula nyama ya Panya aliyekutwa amekufa...kuliko kula nyama ya Kuku iliopikwa?
Baah somo kuchidika?
Mweh soomo uvekwa achi?
 
Wishing CDM all the luck. Concentration ilijikita kazkazini mno kiasi cha kunitia wasi wasi.
 
Acha ukulima wewe kwenye swala la mabadiliko kwani kuna watu wanaoana hapa?

Ukweli unaumaaaaaa......
Wachaga wana ubaguzi xana!!!!! Hata marehem baba yangu pale Mikindani aliniambiaaaa..... CDM hamtaweza kukubalika milele!!!!!!


Pili huku kuna waislam tupu, na ule udini mmechemka!!!!! Niko huku Lipwidi, Mtwara Vijijin nalimaaaa!!!!
 
Ukweli unaumaaaaaa......
Wachaga wana ubaguzi xana!!!!! Hata marehem baba yangu pale Mikindani aliniambiaaaa..... CDM hamtaweza kukubalika milele!!!!!!
Pili huku kuna waislam tupu, na ule udini mmechemka!!!!! Niko huku Lipwidi, Mtwara Vijijin nalimaaaa!!!!
hiyo ni wewe na hicho kikongwe chenu kilichofariki lakini usiwasemee wengine
 
Mkuu habari ya Jumanne tunaijadili leo Ijumaa halafu unaiita eti News Alert...Pro-Chadema JF wana vituko bana.
 
Hata Uzini ilikuwa hivi hivi..
Natafuta comment ya Slaa hapa JF siku wawalipoenda Uzini.
Nafikiri wote mliona CDM walichoambulia kule!!
 
Back
Top Bottom