CHADEMA ni wachawi wa upinzani - Mtatiro

Nakushauri Mtatiro kw mara ya mwisho kuacha siasa za maji taka, wewe bado ni kijana mdogo na you have a long to go! CCM watakuchafua, unaonekana uko kidogo kama Zitto japokuwa mwenzako anajirudi sasa, pia elewa kuwa Watanzania wa leo ni waelewa sana. Kwa taarifa yako CUF ilikuwa ni ile ya zamani enzi za akina Mapalala, kanda ya ziwa sote tulikuwa CUF, bahati mbaya CUF ilikufa Bara na wewe unaisaidia kufa kama Mkwere anavyoiua CCM. Kumbuka au fahamu Yuda aliumbwa ili amsaliti Yesu, hakuna huruma kwa Yuda kwani from the beggining Yuda aliumbwa kuwa ni agent wa Shetani. Acha kabisa kuuzunguka ukweli kuwa CUF ni sehemu ya serikali na Katibu mkuu ni mtendaji mkuu wa Chama na kwa kuwa ni makamu wa Rais haiwezi kwenda kinyume na serikali yake. Tambua tunaposema CCM imeshidwa na CUF mmo!
 
CDM Wachawi wa upinzani ana maana kwamba, umoja ni nguvu, utengano ni udhaifu. Vyama vya upinzani havina tena umoja, ni malumbano tu hasa CDM inavyojibagua na wenzake. Mtafika wapi? Hata mmoja akifanikiwa kuchukua madaraka, itakuwa vurugu tu ya tamaa ya madaraka na kuoneana wivu. Bora tubaki tulivyo tuendelee kusukuma gurudumu tunalolijua.
 
Mtatiro ni mtu mwenye maneno mengi tena yasiyojenga zaidi sana ni kujihami na kujaribu kuharibu hali ya hewa ndani ya CDM na wananchi dhidi ya CDM, binafsi huyu jamaa ni kati ya watu ambao nimewapuuza muda mrefu, mtatiro anafaa sana kwa maneno yake mengi ya hovyo hovyo kuwa MC kwenye kicheni parties/unyagoni.

Mwenye number yake ya simu naomba ili nimpe kazi. Nataka kuanzisha kampuni ya uburudishaji. Inaelekea huyu atatufaa maana siasa zinaelekea kumshida. Seriously, Mtatiro nitafute nikupe kazi ya u-MC next week. Naingia Bongo J'tatu kwa hiyo unaweza kuni-PM).
 
Mimi ninachojuwa kuna CCM moja na CUF moja. Katibu mkuu wa CUF ni makamu wa kwanza wa rais wa Zanzibar kwenye serikali ya Umoja wa kitaifa ambayo inatekeza sera za chama cha mapinduzi. Hivyo CUF inatekeleza sera za CCM kwenye nchi ya Zanzibar na haiwezi kuwa mpinzani wa CCM tena kwani hakuna CCM Zanzibar na CCM tanganyika. Labda Kaimu Katibu Mkuu wa CUF atueleze kama kuna CUF mbili yaani ya CUF Tanganyika na CUF Zanzibar na kuwa CUF Tanganyika haina ushirikiano wowote na CCM wala CUF Zanzibar.
 
Namfahamu vyema Mtatiro, ni mropokaji, aliibuka tukiwa mwaka wa pili baada ya kumtusi Mwl wa Kiswahili- Mrs Lyimo, ulizeni mtaambiwa, so huyu jamaa sioni kuwa ana jipya kwangu na kwa jamii
 
CDM Wachawi wa upinzani ana maana kwamba, umoja ni nguvu, utengano ni udhaifu. Vyama vya upinzani havina tena umoja, ni malumbano tu hasa CDM inavyojibagua na wenzake. Mtafika wapi? Hata mmoja akifanikiwa kuchukua madaraka, itakuwa vurugu tu ya tamaa ya madaraka na kuoneana wivu. Bora tubaki tulivyo tuendelee kusukuma gurudumu tunalolijua.

Mimi ninataka hawa wanasiasa na vyama vyao wasipatane yaani wavurugane mpaka pachimbike. Kwani wakipatana tumekwisha hatutajua masuala ya ufisadi na ufirauni mwingine tunaofanyiwa kama wote wakiwa kitu kimoja. Ndio maana sifurahii hata kidogo kwa CUF, TLP na vyama vingine kupatana na CCM kwani haviwezi tena kuikosoa CCM ili itawale vizuri. Vimeishia kuwashambulia CHADEMA utadhani ndio chama tawala. Sasa hawa "so called" wapinzani wakipatana na CHADEMA si ndio tutakuwa tumekwisha? Kwa ufupi wakipatana CCM, CUF et al, na CHADEMA hakutakuwa na upinzani tena wa kuleta "Checks and balances" tunazozihitaji sana kwenye nchi hii. Watakuwa sawa na waimba mashairi tu yasiyokuwa na ujumbe wowote wa matumanini kwa wananchi wa kawaida.
 
Kaimu Katibu Mkuu wa CUF, Jurius Mtatiro amesema Chadema ni wachawi wa upinzani Tanzania, tena ni vigeugeu wakubwa watu wa propoganda kila siku wanaumiza vichwa vyao jinsi gani watawauwa CUF; wanaeneza propoganda CUF wamaeungana na CCM hawawezi kushirikiana nao wakati huo huo Chadema wanachukuwa pesa kutoka kwa kada wa CCM SABODO, ni sawa sawa kusema utaki kula nyama ya nguruwe lakini supu yake unakunywa.

MLIMANI TV
kula maembe haimaanishi kuwa na mimi ni mti wa mwembe
mwembe ni mwembe na mimi ni mimi

mwenye akili ndogo isiyo ya PhD atajiuliza zaidi uhusiano wa
SABODO NA UKADA WAKE CCM lakini si CDM NA SABODO
 
Kaimu Katibu Mkuu wa CUF, Jurius Mtatiro amesema Chadema ni wachawi wa upinzani Tanzania, tena ni vigeugeu wakubwa watu wa propoganda kila siku wanaumiza vichwa vyao jinsi gani watawauwa CUF; wanaeneza propoganda CUF wamaeungana na CCM hawawezi kushirikiana nao wakati huo huo Chadema wanachukuwa pesa kutoka kwa kada wa CCM SABODO, ni sawa sawa kusema utaki kula nyama ya nguruwe lakini supu yake unakunywa.

MLIMANI TV

Povu litawatoka sana mwaka huu.
 
Mtatiro jenga hoja na acha propaganda. Mtawezaje kuwa wapinzani wa CCM wakati lenu moja? Je tangu maalim aingizwe kwenye serikali ameshatoa kauli ya kuzungumzia hali ngumu ya maisha ya watanzania? Kabla ya hapo alikuwa moto, sasa kimyaa
 
Hivi wadau naomba niambiwe japo kwa kunong'onezwa tu. HIVI CCHADEMA ina maadui wangapi?. Na ni nini hofu ya hawa jamaa wa CCM, CUF, NCCR na TLP kwa CDM?.

Mimi naomba nitabiri yaliyotokea kwa TAMBWE HIZA yanaenda kutokea kwa huyu kijana wa CUF si muda mrefu.
 
nimegundua humu kuna mijitu mingine ina akili za makalioni kama mtatiro mwenyewe.jadili mada wewe acha uvuvuzela usiokuwa na mantiki.yani cuf utawagundua tu mapema kwa udini walio nao.

tehe tehe tehe! ama kweli nyani haoni .......! nyie!!!!!
 
mtatiro wewe ni ccm huwezi kupinga hilo na kwa sasa unatekeleza maelekezo ya wanaccm mafisadi na watawala uchwara, pole sana kijana umeshindwa kujitambua na umebakia kubwabwaja njaaaa inakushushia hadhi,
 
Nadhani tuna haja ya kuamini kuwa Chadema ndiyo chama Tawala kwa sababu ndiyo chama ambacho kinapingwa. Wapinzani wa Chadema ni CCM, CUF, NCCR - Mageuzi, TLP, UPD... Mti wenye matunda ndio unaorushiwa mawe.

Kama Chadema siyo chama Tawala iweje CCM waungane na vyama vingine kukipinga? Mara nyingi tumeona vyama vingine vinavyodhaniwa kuwa vya upinzani vikikashifu Chadema badala ya chama kilichopo madarakani. Kwa hili tukubaliane tu kwamba CCM na vyama hivyo vingine vitangaze kuwa Chadema ni chama Tawala ili yaishe.

Hii nimeipenda kwa sababu ndo ukweli wa mambo... Nashangaa vyama hata vile vinavyojiita pinzani vinapambana na CHADEMA... from today mimi kwangu chadema ni chama tawala... the rest upinzani full stop!!
 
Kwa mtu yeyote mwenye fikra pevu haitaji kuambiwa CUF ni ccm B na wala hakuna ubishi lipo wazi kwa mitazamo.
 
Hivi ni ilani ya chama gani inatekelezwa na srikali ya mapinduzi kule zanzibar?
Ingekuwa kipndi cha miaka 2.5 ni utekelezwaji wa ilani ya chama kimoja na 2.5 ya pili itekelezwe ya chama kingine, pasingekuwa na habari za mme na mke. Woote yaani sisiem na kafu wangekuwa vidume.
.
 
Kwa mtu yeyote mwenye fikra pevu haitaji kuambiwa kuwa cuf ni ccm B kwani kila wanachofanya ni kuibeba ccm iliyojifia
 
Njaa na kukurupuka, aliwapa CHADEMA masharti ya nyumba na gari ili ajiunge, wakamshtukia!!
Kama Bwana samata wa simba vile duu siasa sikuhizi unafanyika usajili kama simba na yanga...........
 
si CCM, CHADEMA wala CCM zenye uchungu wa kweli na WATANZANIA... Zoooote ni TAKA mbovu na mbaya HAZIFAI hata kutupa shambani kwa mbolea. Wote hao wanapaswa wafe PAPATIKANE KITU KIPYA WATU WAPYA NA VIONGOZI WAPYA! vinginevyo itakuwa sawa na mziki wa matarumbeta kuusikiliza mpaka uzibe masikio.

kama wote wanashindana na kushirikiana kwenye upuuzi mwenye nafuu hapo ni nani?
 
Nakuuliza Mtatiro cuf gani ambayo Cdm inataka ife?
Kwa sasa cuf zipo4
1 cuf udini!
2 cuf upemba!
3 cuf mageuzi!
4 cuf uccm!
ukinijibu nitakushauri inawezekana ulichosema ni sahihi!
 
Back
Top Bottom