CHADEMA ni wachawi wa upinzani - Mtatiro

Hana jipya huyo, kwa hiyo kupewa hela na SABODO ni kuungana na CCM? Huyu bwana mdogo akubali tu kwamba alishaingia choo cha kike, wenzake wanajadiliana maswala ya CUF mskitini ambapo yeye hawezi kufika, halafu anakuja kukurupuka na kuongea upuuzi tu.

CUF wameungana na CCM Zanzibar kuunda what is called serikali ya kitaifa, je wana-qualify vipi kuwa wapinzani? Dogo akiweza hata achomoke tu na aende CHADEMA anaweza pokelewa tu, muulize alijaribu ubunge Ubungo alipata kura ngapi??

Hata Zito Kabwe hawezi kuingia Kanisani wakati wenzake wakijadili masuala ya CHADEMA!!!!!!!
 
CDM Wachawi wa upinzani ana maana kwamba, umoja ni nguvu, utengano ni udhaifu. Vyama vya upinzani havina tena umoja, ni malumbano tu hasa CDM inavyojibagua na wenzake. Mtafika wapi? Hata mmoja akifanikiwa kuchukua madaraka, itakuwa vurugu tu ya tamaa ya madaraka na kuoneana wivu. Bora tubaki tulivyo tuendelee kusukuma gurudumu tunalolijua.
CDM ndio wanaobaguliwa,we mwenyewe ni shahidi makombora yote ya scuud kutoka vyama vyote yanaelekezwa kwao wao wamebaki na UMMA
 
Anaumizwa na kile alichokikosa cdm, akili yake ipo cdm na anaamini hilo lakini tumbo lake lipo cuf na inabidi aseme hivyo ili ashibe:washing:
 
Kama walivyo Arfi na Zitto vilee kule CDM..wenzao wanaweka mikakati yao kanisani wakiongozwa na ( Pe..go) a.ka Kibogoyo wao wanapata tabu kuijenga CDM sasa chamoto wanakiona...maana kila siku zengwe tu..mara eti oh! anatumiwa na CCM mara oh! ni swahiba wa RA..n.k

Nchi hii bana siasa kweli ni SIHASA.
Wakatabahu
Shkh Yahya.

kama zitto anaandamwa sababu ya dini yake mbona halima mdee hasemwi..zitto ushamba ndio unamsumbua,
 
CDM Wachawi wa upinzani ana maana kwamba, umoja ni nguvu, utengano ni udhaifu. Vyama vya upinzani havina tena umoja, ni malumbano tu hasa CDM inavyojibagua na wenzake. Mtafika wapi? Hata mmoja akifanikiwa kuchukua madaraka, itakuwa vurugu tu ya tamaa ya madaraka na kuoneana wivu. Bora tubaki tulivyo tuendelee kusukuma gurudumu tunalolijua.

Mwanangu kama hujui malumbano ni mazuri sana kwa mwananchi, ili apime mchele na pumba bila malumbano tusinge jua picha kamili ya cuf.
Tuungane kudai katiba sio muungano huu mnaoutaka wa panya100 ili akija paka mchimbe wote100.
 
Wakati wenzenu wanafanya siasa na maendeleo, tanzania mpo kwenye mipasho na kuongelea watu! Poleni sana!
 
kama zitto anaandamwa sababu ya dini yake mbona halima mdee hasemwi..zitto ushamba ndio unamsumbua,
....INGELIKUWA MAJINA NDIO DINI..BASI ASKOFU WA LEBANON ASINGELIITWA MUSTAFA! Huwa nafurahi sana great thinkers wanaposhindwa kuonesha fikra pevu zao!
 
....INGELIKUWA MAJINA NDIO DINI..BASI ASKOFU WA LEBANON ASINGELIITWA MUSTAFA! Huwa nafurahi sana great thinkers wanaposhindwa kuonesha fikra pevu zao!

Kinachokufurahisha hapa ni nini badala ya kuwahuzunikia kwa sababu wanatumia rasilimali zao kwenye mambo yasiyo na tija!
 
Kaimu Katibu Mkuu wa CUF, Jurius Mtatiro amesema Chadema ni wachawi wa upinzani Tanzania, tena ni vigeugeu wakubwa watu wa propoganda kila siku wanaumiza vichwa vyao jinsi gani watawauwa CUF; wanaeneza propoganda CUF wamaeungana na CCM hawawezi kushirikiana nao wakati huo huo Chadema wanachukuwa pesa kutoka kwa kada wa CCM SABODO, ni sawa sawa kusema utaki kula nyama ya nguruwe lakini supu yake unakunywa.

MLIMANI TV

Ana matatizo huyo......kwani kuchangiwa unaangalia nani katoa? hajui kuwa SABODO ni mwanachama mfu wa CCM.....
 
Hivi m/kiti wa kwanza na wapili wa CUF wapo wapi na nini kiliwatoa huko CUFni, alafu Mtatiro naona hamjui Maalimu vyema, Maalimu mwenyewe ni CCM damu tokea utotoni sasa sijui upinzani aliingia vipi? na alikuja kufanya nini? ni Sawa leo utwambie Mzee Mwinyi ni Upinzani.

Mkuu umenistua na hizo data zako kabla uja challenge jaribu kwanza kufanya utafiti, wewe una sema Maalim Seif ni CCM toka utotoni.
Maalim Seif kazaliwa 22 October 1943.
CCM imeanzishwa 5 Februari 1977.
hapa mtoto sijui ni nani acha kukurupuka
 
....INGELIKUWA MAJINA NDIO DINI..BASI ASKOFU WA LEBANON ASINGELIITWA MUSTAFA! Huwa nafurahi sana great thinkers wanaposhindwa kuonesha fikra pevu zao!

Usilete mipasho!
Mwenzio alichosema kwamba hatuhukumiani kwa imani isiyoonekana, bali kwa matendo yanayoonekana hadharani.
 
Kaimu Katibu Mkuu wa CUF, Jurius Mtatiro amesema Chadema ni wachawi wa upinzani Tanzania, tena ni vigeugeu wakubwa watu wa propoganda kila siku wanaumiza vichwa vyao jinsi gani watawauwa CUF; wanaeneza propoganda CUF wamaeungana na CCM hawawezi kushirikiana nao wakati huo huo Chadema wanachukuwa pesa kutoka kwa kada wa CCM SABODO, ni sawa sawa kusema utaki kula nyama ya nguruwe lakini supu yake unakunywa.

MLIMANI TV
Hivi kuna kesi yoyote CHADEMA kumpora mtu yeyote fedha kwa kipindi chochote kila ndani na nje ya nchi??

Ewe Juliasi (Nyerere), linda heshima ya hilo jina vizuri tafadhali; hata ungeyasema haya kwenye kukampenia kule DARUSO enzi hizo nadhani ndio kabisaa wangekupiga chini!!

Inamaana kitendo cha CUF kuwa serikali kule zenji si kitu cha kweli tena bali ni uchawi na ubunifu tu wa CHADEMA sio???
 
Mkuu umenistua na hizo data zako kabla uja challenge jaribu kwanza kufanya utafiti, wewe una sema Maalim Seif ni CCM toka utotoni.
Maalim Seif kazaliwa 22 October 1943.
CCM imeanzishwa 5 Februari 1977.
hapa mtoto sijui ni nani acha kukurupuka

Maalimu ni CCM tena damu kabisa... Aliondoka pale kwa sababu ya mwalimu kila mtu anajua... Sasa Mwalimu hayupo basi ndo hivyo tena kesharudi CCM....
Mbona kila siku CUF wakilalamika hamwambii jamaa kama msemaji mkuu wa chama na Katibu mkuu kuomba CHADEMA wawashirikishe kwenye upinzani??? Mgombea mwenza wa Lipumba Duni Haji ni waziri kule hapo hapo aliwapinga CCM... Jamani kuungana ni ngumu kuelewa?? Jamaa wameungana acheni uzumbukuku siri za upinzani zitavuja kama tukishirikiana nao
 
Naona umekurupuka mimi sipo huko unapoelekea ebu rudia kusoma hiyo post niliomjibu huyo anaesema Maalim Seif ni CCM toka utoto! sio kukubaliana kila kitu ata kama pumba kwa kuwa wote ni Chadema hapana mkuu
 
Niliwahi kumwambia kuwa CUF siyo yake na pia siasa za CUF sio na pia niliwahi kuongea na Jussa kablaya ya uchaguzi mkuu na kumwambia juu ya upinzani na athali za kuungana sana kule Zanzibar na hatma ya Upinzani hasa kule visiwani ila alikataa na kuona kuwa wapo sahihi ila Ukweli kuwa CUF ndio mwisho wao na pia hakuna tena upinzania kule visiwani ndio wameua demokrasia. Kitu kizuri ni kuwa kungekuwa na Political tolerence baina ya vyama sio Muungano
 
Muda fulani akiwa pale Hills nilidhani TZ ina vijana makini sana, alipotua CUF na kutangaza kuwa mgombea kupambana na Mnyika nikajua katumwa na CCM, Tangia hapo nilimfuta kabisa, hafai hata kidogo! Nachukizwa sana na upupu wake dhidi ya CDM
 
Huyu kijana vipi, mbona ana ongea utumbo? Ndo kazi aliyopewa na CUF, kuifuatilia cdm? anyway hizo ni chuki za kubwagwa mbaya ubungo!
 
Back
Top Bottom