CHADEMA, anzisheni TV/Radio Station!

mbona bado wapo kimya? au hii thhread haiaisomagi wahusika? au kuna vikwazo vyovyote huko?
 
mbona bado wapo kimya? au hii thhread haiaisomagi wahusika? au kuna vikwazo vyovyote huko?

Wakati mwingine huwa najiuliza kama kuna tofauti kati ya ccm na Chadema katika kusikiliza maoni ya wananchi na kuyafanyia kazi. Pengine tungejua kwanza wasifu wa timu ya mawasiliano ya Chadema. Wamelalamikiwa mno, mara nyingi sana na mara zote hawajawahi kujibu lolote wala kutekeleza chochote. Prove me wrong
 
mnachekesha, usajili huo atatupa nani? Labda tuanzishe strategy ambayo inaweza kuwalazimisha hawa mafisadi kutoa hiyo leseni ya mawa7iliao6
 
mnachekesha, usajili huo atatupa nani? Labda tuanzishe strategy ambayo inaweza kuwalazimisha hawa mafisadi kutoa hiyo leseni ya mawa7iliao6
 
Ni wazo zuri naomba viongozi walifanyie kazi. Mamluki wataendelea kuwepo tu hawakwepeki! Ni kuangalia namna ya kuwathibiti tu!
 
Naunga mkono hoja na mimi bunafsi nitatoa usd 500 kama mchango wa harambee hiyo
 
  • Je media(TV/magazet/radio) zina nguvu kiasi hicho ?
  • Je media zinazomilikiwa na maswahiba wa serikali iliyo madarakani inaweza kuzuia mageuzi?
  • Je media media 'huru' zinaweza kuleta mageuzi?
  • je mapambano ya hoja kati ya tabaka la watawala na watawaliwa nje ya media ndiyo yenye nguvu kuliko propaganda za media?
  • je Mapambano ya hoja ktk bunge, midahalo, mikutano, JamiiForums, midahalo ya UDASA (UDSM), Karimjee hall, Juzi mkutano wa CHADEMA huko Tabora(majina mia ya mafisadi) n.k ndio yenye tija kubadili mawazo ya wananchi na hata mawazo ya wahariri na wamiliki wa vyombo vya habari kamaMagazeti, Vituo vya Radio/TV?
  • Juzi tumesikia kina Msekwa, Malecela, Daily News , CCM wakilia kuchomwa na mwiba wa nguvu za hoja nje ya media za kawaida(RADIO/TV/Magazeti) za JAMIIFORUMS na hivyo kuna umuhimu wa kuwa na jamiiforums za vijiweni/vijijini/wilayani ambayo siyo online au electroniki bali vikundi vya harakati vya kijamii vikiongozwa na mawazo ya CHADEMA vinavyokutana ngazi ya mashina?
Sikiliza clip hii:
 
Last edited by a moderator:
Hoja zinazotolewa ati si busara kwa CHADEMA kuanzisha vituo vyake vya mawasiliano bado ni dhaifu na zinahitaji tafakuri ya kina. Kwa vyovyote vile vyombo vya mawasiliano vinabaki muhimu kabisa katika kuendeleza propaganda kama wanavyofanya CCM na Radio yao ya UHURU na TBC, Channel Ten na mara nyingine ITV ambavyo mara kadhaa vimeegemea chama Tawala.

Anayesema si busara kwa CHADEMA kumiliki vyombo vya mawasiliano atafakari impact wa Blogs zilivyotumiwa kikamilifu na wapenda mabadiliko kuihamasisha jamii kuelewa uovu wa CCM dhidi ya taifa na mwitikio wa wananchi haswa vijana. kitendo cha vijana kumiminika kwenye ma blogs kutafuta habari za CHADEMA kidokeza hitaji kubwa zaidi la vyombo vya kuwahabarisha.

CHADEMA lazima wawe makini sana na ushauri wanaopewa kama huu wa leo katika JF kwani serikali na CCM imepenyeza majasusi wengi wenye kazi ya kuwapotosha CHADEMA wasichukue uamuzi unaofaa. haiingii akilini hata kidogo kwamba vyombo vinavyoisaidia CCM kueneza propaganda zake kwa mafanikio vilete matokeo tofauti katika CHADEMA. Kama hivyo ndivyo kina RA et al wasingehaha kuinunua Habari Corporation iliyokuwa very critical kwa CCM na uongozi wake mbovu.

Ushauri wangu ni kwamba CHADEMA ijipange, ianzishe TV na Radio yake na hata information Centres ambazo vijana wanaweza kukutana na kuhabarishana juu ya mikakati ya kuitetea nchi dhidi ya angamizo la mafisadi wa CCM wanaotulaghai ati wamejivua gamba. Ukweli ni kwamba nyoka akijivua gamba hubaki na sumu ileile na kamwe hageuki mjusi. Hivi watayatibu vipi majeraha waliyolisababishia taifa hili kwa ujambazi wao wa kuuza na kugawana rasilimali za serikali kwa bei ya kutupwa na mara kadhaa bila hata ya kufuata taratibu wakigawana wao na maswahiba zao? Wameuza viwanda vya msingi wa maendeleo kuanzia vidogo hadi vikubwa kwa maslahi yao binafsi, wameiingiza nchi kwenye mikataba inayotiririsha damu ya taifa hadi miaka ishirini au zaidi ijayo, wamegawana hadi nyumba za serikali na kudunisha kabisa uwezo wa serikali kuwapatia watumishi wake makazi.

Nasisitiza ni muhimu wa CHADEMA kumiliki vyombo vya mawasiliano na wananchi ili kupata upande wa pili wa habari na kujibu propaganda za chama tawala zinazosambazwa na vyombo vya habari vya CCM ambayo kwa bahati mbaya imeviteka hata vyombo vinavyoendeshwa kwa kodi yetu kama TBC.
 
Usitake kuingiza CHADEMA kwenye mkenge. Chadema staili yake ya kuendesha 'elimu kwa umma' kwa kutumia mikutano ya wazi na wananchi inatosha kuwaelewesha wananchi haki zao za msingi.

Historia inaonyesha kuwa ukianzisha vyombo rasmi vya kuwasiliana na wananchi kwa njia ya radio, TV au gazeti unakaribisha 'mamluki' kujipenyeza na kuchafua hali ya hewa.

CHADEMA iendelee kutumia mikutano na wanachi ili kuishitaki serikali ya CCM kwa kutowajibika kwa wananchi masuala ya RADIO UHURU, STAR TV, magazeti ya UHURU/MZALENDO/DAILY NEWS waachiwe CCM. CHADEMA tayari ina safu za viongozi na makada na wapenzi wake ambao wanatosha kusambaza 'elimu kwa umma juu ya siasa' na hakuna mantiki ya kuingia gharama ya vyombo rasmi vya habari.

Midahalo ambayo CCM huikimbia CHADEMA wanaitumia kikamilifu, vyombo huru kama JamiiForums CHADEMA inashiriki kikamilifu kutetea hoja zake. Mitego hii ya kutaka kuingiza mkenge CHADEMA gharama zisizo na tija inafaa kuepukwa kama suala hili la kuwa na TV/RADIO/Magazeti rasmi.
Mkuu nakubaliana na wewe kwamba chadema ina nafasi kubwa katika kuelimisha wananchi kupitia vyombo huru vya habari.

Lakini mimi naona bado kuna haja ya kuanzisha TV ya chama! Hivi karibuni vyombo vingi vya habari vimeonekana kwa makusudi vikiancha kutangaza habari za chadema ambazo kwa kimsingi zina maslahi kwa umma wa watanzainia!!! Hawa vyombo vingine vya habari hatuna matatizo navyo lakini ili tuwe na uhakika na mambo yetu hata wakati hivi vyombo vimehongwa na CCM kupotezea habari za CHADEMA.

Tunaogopa gharama lakini gharama ambazo tutazilipa kwa kuwaachia hawa wavua magamba watawale kwenye vyombo vya habari. Kwani mimi naona kuna mkakati mahususi wa kuinima chadema kutangazwa!!!! kwa hali kama hiyo unategemea nini? Mimi nafikiri sisi kama watanzania tuanze kuchangia ili ikifika 2014 uwe tumeshapata TV station ambayo licha ya kuitwa ni ya chadema itaupa umma kila unachokihitaji na sio hili TV la umma ambalo kwa naman isiyoeleweka limetekwa na mavua gamba!!!!
 
mnachekesha, usajili huo atatupa nani? Labda tuanzishe strategy ambayo inaweza kuwalazimisha hawa mafisadi kutoa hiyo leseni ya mawa7iliao6
Tutafuata kila sheria inayotakiwa kufuatwa sasa wakileta mizengwe kutuzuia tunaingia mitaani!! umesahau kuhusu katiba mwanzoni walibana je tunakoelekea unaonaje?
 
Wazo zuri sana la kuwa na Vyombo vya habari, itasaidia hata kupata habari zikiwa na ukweli, Vyomb vingine vikichakachua CDM TV inaweka ukweli hazarani, tupo tayari kuchangia.

tupo wengi sana wapenda Chadema, na tukihamasishana yanaweza kusanywa mamilioni.
Naunga mkono na mimi pia niko tayari kuchangia kama wengine wengi walivyo tayari!!
 
Hiyo Tv itakuwa ya kukashifu watu nini?!
Unamatatizo ya akili huwezi kuchanganua kati ya kashifa na ukweli kinachofanya na chadema ni kuwapa wananchi ukweli kuhusu wahujumu wa rasilimali za nchi yao!!!! kwa akili yako mtu akisema Rostam Azizi ni mwizi amekashifu, kweli unahitaji kikombo cha Babu ili ukombolewe kifikira.
 
CHADEMA Television

Chama cha Democrasia na Maendeleo (CDM) kina kila sababu sasa kuhakikisha kinaa zisha kituo cha TV ili kuondoa hujuma tunzozishuhudia katika TV yetu ya umma TBC dhidi ya kile kinachoonekana dhahili kuziminya habari za chama hiki na wakati mwingine kutokukipa muda wa kutosha ukilinganisha na CCM.

Wote tunaelewa kuwa chama hiki kimeonesha kukubalika na wengi hasa vijana wengi wao wakiwa mijini, nadhani hapa jitihada za maksudi zinahitajika zifanyike ili elimu ya mabadiliko ifike mpaka vijijini ambako ccm bado imepafanya kama mtaji wa chama.

So nafikiri,kama cdm tv itaanzishwa na ikawa na uwezo wa kuchana mawimbi nchi nzima basi moja kwa moja CCM ijiandae kuzikwa rasmi 2015.

Wito wangu kwa viongozi wa cdm kuandaa mkakati kabambe wa kitaifa waje nao kwa wapenzi na wanachama wote wa cdm bila kuwasahau hata wasiokuwa na chama ili kuendesha mchango wa fedha nchi nzima wa kuanzishwa kwa tv chadema je tuko tayari?

Lakini nikileta hoja hii kwenu naomba pia nijulishwe je mamlaka ya anga hapa tz ina kizuizi kisheria juu ya jambo hili kufanyika?naomba kuwasilisha
.

NB: Haya maneno si ya kwangu bali tu ni kwamba hata na mie hapa nilitamani kuyaona uzuri zaidi, kuyasoma na kuyaelewa.

Hii TV tunalihitaji kama tangu juzi vile!!!
Licha ya kuelimisha na kuhabarisha umma Pia TV na redio ya chadema itakuwa ni chanzo cha mapato kwa chama na hivyo kuimarisha chama!!
 
Wakati mwingine huwa najiuliza kama kuna tofauti kati ya ccm na Chadema katika kusikiliza maoni ya wananchi na kuyafanyia kazi. Pengine tungejua kwanza wasifu wa timu ya mawasiliano ya Chadema. Wamelalamikiwa mno, mara nyingi sana na mara zote hawajawahi kujibu lolote wala kutekeleza chochote. Prove me wrong

mi siongei tena mpaka siku wanaJF kama Mbowe,zitto,dr mkumbo,dr slaa,mnyika,regia mtema, et all walio jf watoe majibu . Si lazima mmeseme kuwa mmeanza kutekeleza au hamtatekeleza bali mwaweza kutueleza kama mnaona inafaa au hapana,gharama hamuiwezi au vp,etc etc. Viongozi wetu,sema neno tu,nafsi zetu ziwaelewe! Tunawasubiri.
 
mi siongei tena mpaka siku wanaJF kama Mbowe,zitto,dr mkumbo,dr slaa,mnyika,regia mtema, et all walio jf watoe majibu . Si lazima mmeseme kuwa mmeanza kutekeleza au hamtatekeleza bali mwaweza kutueleza kama mnaona inafaa au hapana,gharama hamuiwezi au vp,etc etc. Viongozi wetu,sema neno tu,nafsi zetu ziwaelewe! Tunawasubiri.

Zungumzeni basi tuanze fund rising. Hakuna kulala hii iwe ya umma.:hat:
 
Hoja zinazotolewa ati si busara kwa CHADEMA kuanzisha vituo vyake vya mawasiliano bado ni dhaifu na zinahitaji tafakuri ya kina. Kwa vyovyote vile vyombo vya mawasiliano vinabaki muhimu kabisa katika kuendeleza propaganda kama wanavyofanya CCM na Radio yao ya UHURU na TBC, Channel Ten na mara nyingine ITV ambavyo mara kadhaa vimeegemea chama Tawala.

.....haingii akilini hata kidogo kwamba vyombo vinavyoisaidia CCM kueneza propaganda zake kwa mafanikio vilete matokeo tofauti katika CHADEMA. Kama hivyo ndivyo kina RA et al wasingehaha kuinunua Habari Corporation iliyokuwa very critical kwa CCM na uongozi wake mbovu.
.

Juhudi za CCM pamoja na fedha kibao za mafisadi zinazoendesha vyombo vyao vya habari vya propaganda vya CCM zimeshindwa kufifisha moto wa kutaka mabadiliko.

Operesheni Sangara za CHADEMA zimefanikiwa kwa kiwango kikubwa kubadili picha ya kisiasa nchini vya majimbo mengi kutwaliwa na CHADEMA. Mchanganyiko wa oparesheni Sangara, jamiiforums, midahalo na hata vyombo vya habari vitakavyomilikiwa na CHADEMA vikiendesha 'elimu kwa umma' kwa malengo sahihi zinaweza kwa pamoja kufanikisha dola kuchukuliwa na CHADEMA.
 
Ni muhimu Chadema kuwa na TV na redio hata wakitangaza masaa sita tu kwa siku lakini wawe navyo,kunaupotoshaji mkubwa wa habari zao na propaganda za kuwauwa kisiasa
 
Wakuu,

Kwa maoni yangu TV, Radio etc hazitakuwa na impact kubwa na hasa vijijini. Ikumbukwe vijijini ndo hasa tanakolenga, na changamoto za huko wote tunazijua, hakuna umeme, hata masafa kufika kule ndani ndani ni shida vilevile. hata kama hayo yote yata wezekana, ni wangapi vijijini wana uwezo wa kumiliki (kununua) ka TV hata ka nchi 12??

Mawazo yangu: Nadhani ni busara kutumia hiyo bajeti ya kusimika TV kuimarisha ziara za wawakilishi wetu tulio nao: Wabunge, madiwani na wapiganaji wote tulio nao. Halafu ninavyojua mimi mikutano ni effective zaidi kuliko TV, Radio na/au magazeti.

Ninavyofahamu utendaji kazi wa serikali ya ccm, wataweka vizingiti kibao kwenye leseni, kodi za vifaa utajikuta imechukua zaidi ya miaka miwili ndo wanawapa leseni kwa majaribio, ghafla 2015 hii hapa.
 
mi siongei tena mpaka siku wanaJF kama Mbowe,zitto,dr mkumbo,dr slaa,mnyika,regia mtema, et all walio jf watoe majibu . Si lazima mmeseme kuwa mmeanza kutekeleza au hamtatekeleza bali mwaweza kutueleza kama mnaona inafaa au hapana,gharama hamuiwezi au vp,etc etc. Viongozi wetu,sema neno tu,nafsi zetu ziwaelewe! Tunawasubiri.

dr, Slaa jana kaja hapa na kutoa majibu na akaishukuru JF ngoja nikutafutie ile post nitaiquote na kuja nayo hapa
 
Back
Top Bottom