Ba Martha
JF-Expert Member
- Aug 13, 2010
- 349
- 102
Kutokana na msukumo na hali halisi hapa kwetu Tanzania kuonyesha kuwa vyombo vingi vya habari ama kununuliwa na selikali ya CCM au watu wenye maslahi yao binafsi katika kutangaza habari na kutetea upande wao, huku upande wa pili ukikandandamizwa, Ningependa kutoa ombi hasa kwa CHADEMA kumiliki vyombo vyake vya habari hasa televisheni na radio ili wananchi wengi zaidi waweze kupata kile ambacho kinastahili wakipate katika nyanja za kisiasa, kijamii, kiuchumi na kiutamaduni.
Nadhani hilo litakuwa na faida nyingi sana katika kutangaza sera za chama na malengo yake kwa wananchi walio wengi wenye kiu ya mabadiliko katika nchi yetu..
Natoa hoja.
Mungu ibariki Tanzania
Nadhani hilo litakuwa na faida nyingi sana katika kutangaza sera za chama na malengo yake kwa wananchi walio wengi wenye kiu ya mabadiliko katika nchi yetu..
Natoa hoja.
Mungu ibariki Tanzania
Chama cha Democrasia na Maendeleo (CDM) kina kila sababu sasa kuhakikisha kina azisha kituo cha TV, ili kuondoa hujuma tunazo zishuhudia katika TV yetu ya umma TBC dhidi ya kile kinachoonekana dhahiri kuziminya habari za chama hiki na wakati mwingine kutokukipa muda wa kutosha ukilinganisha na CCM.
Wote tunaelewa kuwa chama hiki kimeonesha kukubalika na wengi hasa vijana wengi wao wakiwa mijini,nadhani hapa jitihada za makusudi zinahitajika zifanyike ili elimu ya mabadiliko ifike mpaka vijijini ambako CCM bado imepafanya kama mtaji wa chama.so nafikiri,kama cdm tv itaanzishwa na ikawa na uwezo wa kuchana mawimbi nchi nzima basi moja kwa moja CCM ijiandae kuzikwa rasmi 2015.
Wito wangu kwa viongozi wa CDM kuandaa mkakati kabambe wa kitaifa waje nao kwa wapenzi na wanachama wote wa CDM bila kuwasahau hata wasiokuwa na chama ili kuendesha mchango wa fedha nchi nzima wa kuanzishwa kwa tv CHADEMA. Je, tuko tayari? Lakini nikileta hoja hii kwenu naomba pia nijulishwe je mamlaka ya anga hapa TZ ina kizuizi kisheria juu ya jambo hili kufanyika?
Kwa mujibu wa thread fulani ya siku za nyuma, Dk Slaa ulijitokeza na kusema tarehe 15 tutarajie habari mpya juu ya mabadiliko makumbwa kuhusu vyombo vya habari ikiwemo television.
Naomba utujuze tena mmefanikiwa au laa na kama hamjafanikiwa mchakato unaendelea vizuri?