CHADEMA, anzisheni TV/Radio Station!

Ujumbe huu,tumeshaupenyeza sana kwa Dr Slaa,mara nyingi pia kwa Regia Mtema,zaidi kwa viongozi wa juu cdm. Nadhani wanalifanyia kazi na namtaka Dr Slaa au Regia(MB) achukue muda wake,awashe komputa na kuitafuta jf ili aweze kutuliza wote wenye hamu na shauku ya kuwa na vyombo huru vya umma wa watanzania,ikumbukwe kuwa kwa sasa hatuna vyombo vya umma kwa kuwa TBC Corporation imebinafshwa,je hapo 2015 chama tawala chadema itawezeje kutufikia wananchi? Katibu mkuu chadema hitimisha thread hii! Thanks Jf.
 
Mawazo mazuri mkuu, kwa vijijini nadhani hata radio CDM ni muhimu kuwa nayo, Radio hiyo iwe km RTD ya zamani! CDM NDIO CHAGUO LETU SOTE, 2015 MWAKA WETU!
 
Vituo vya Tv/Radio ni gharama kuviendesha na kutumia ruzuku za vyama (CHADEMA) kuendesha vyombo vya habari haina tija zaidi ya mikutano ya CHADEMA na wananchi/kuboresha ofisi/mitandao vyuoni n.k
  • Pia CHADEMA kupata source/vyanzo vya hela nje ya ruzuku(matangazo ya biashara/wadhamini) kwa sasa ni mtihani mkubwa
  • Gharama za kuendesha Vyombo vya TV/Radio zitadhoofisha harakati zingine za kuwafikia wananchi kule walipo.
  • Ikiwa gharama za TV/Radio ni Tshs. Billioni 1(Clouds FM/Radio Uhuru bajeti zao ni mfano) kwa mwaka kwa uchache ni project isiyowezekana na ukienda ndani zaidi kufikia umma kona zote kupitia vyomb hivyo TV/Radio ni changamoto. Bora kuwawezesha makada/viongozi mashinani/vyuoni n.k waendeleze moto wa CHADEMA.
  • Mamluki kuingiza studio 'nyaraka za siri za serikali' na kisha kukilaumu CHADEMA ni rahisi au hata kuchoma moto vifaa ghali vya kutendea kazi studio baada ya gharama kubwa kuvinunua ni rahisi kwa mafisadi na kupelekea kukidhoofisha chama cha CHADEMA.
Niishie hapo kuna sababu nyingi tu za 'kiintelejensia' ila kwa mikakati iliyopo ya sasa ya CHADEMA kuwafikia wananchi ni tosha kabisa kuleta mageuzi nchini.

Vituo vya Tv/Radio ni gharama kuviendesha na kutumia ruzuku za vyama (CHADEMA) kuendesha vyombo vya habari haina tija zaidi ya mikutano ya CHADEMA na wananchi/kuboresha ofisi/mitandao vyuoni n.k
Mtoa hoja hajasema kuwa tutaanzisha TV na kuacha mengine. Hapana. Ujenzi wa Chama ngazi za chini unaendelea kama kawaida, iwe vyuoni ama kwa wanachi wa kawaida. Tutaendeshaje vyote viwili kwa pamoja kwa kuwa ni gharama kubwa hiyo ni siri ya kamati kuu na secretariet.
Pili, vyombo vya habari vitapunguza gharama ya mikutano. Mikutano husika itatangazwa ktik gazeti la Chama na Tv yake, badala ya kukodi gari na vyombo vya muziki na kuzunguka mitaani kwa siku mbili kwa gharama kubwa kabla mikutano husika.

[*]
Pia CHADEMA kupata source/vyanzo vya hela nje ya ruzuku(matangazo ya biashara/wadhamini) kwa sasa ni mtihani mkubwa

Mimi mjumbe wa baraza kuu siwezi kulismea kamati kuu na secretarieti kuhusu hili, wewe unawezaje?

[*]Gharama za kuendesha Vyombo vya TV/Radio zitadhoofisha harakati zingine za kuwafikia wananchi kule walipo.
wewe umefanyia wapi utafiti? Je, kama mikutano lengo ni kufikia wananchi si Tv nayo inafikia wanachi? Kama mikutano ikipungua sababu ya TV na TV ikawafikia watu wengi zaidi kuliko mikutano, je hiyo si faida? Kwa taarifa, TV inaweza kuwafikia watazamaji mil moja kwa dk 5. Je CHADEMA inahitaji Tsh Ngapi kufanya mikutano mingapi kwa muda gani kuwafikia idadi hiyo?

[*]Ikiwa gharama za TV/Radio ni Tshs. Billioni 1(Clouds FM/Radio Uhuru bajeti zao ni mfano) kwa mwaka kwa uchache ni project isiyowezekana na ukienda ndani zaidi kufikia umma kona zote kupitia vyomb hivyo TV/Radio ni changamoto.

Sina hakika na data zako hapo juu, hii nayo inahitaji utafiti. Suala la uwezo ni la ndani sana ya Chama si hoja kwa sasa. Tunahitaji ukweli kuhusu IMPACT ya Tv kufikia wanachi kila kona. Kwani TBC inawafikiaje wanachi kila kona. Hapo inapoishia propaganda za TBC dhidi ya CHADEMA ndipo nasi tunapotaka kuishia.

[*]Mamluki kuingiza studio 'nyaraka za siri za serikali' na kisha kukilaumu CHADEMA ni rahisi

Hoja iwe tutazuiaje nyaraka feki na si tusianzishe TV. Kama Dr Slaa anaweza kupembua nyaraka feki na halisi na akaweza kuitikisa serikali, atashindwaje TV iliyoko chini yake kama katibu mkuu isitangaze nyaraka feki?

au hata kuchoma moto vifaa ghali vya kutendea kazi studio baada ya gharama kubwa kuvinunua ni rahisi kwa mafisadi na kupelekea kukidhoofisha chama cha CHADEMA.
Hii ni hoja dhaifu sana pia.
Mosi kila kitu kina risk yake. Hata kuendesha gari au kupanda dala dala ina riski. Je, tuache kupanda dala dala au tusinunue magari binafsi na tutembee kwa miguu? Kuchoma tv station ni changamoto tu, siyo sababu ya kutoanzisha tv au magazeti.
Pili, wewe bagamoyo hufahamu kuwa kuna kampuni za Insurance? Si tutaweka comperesive insurance tu? Wakichoma the next week tunafunga vipya na kupata attention kubwa zaidi itakayoongeza watazamaii.
[/LIST]Niishie hapo kuna sababu nyingi tu za 'kiintelejensia' ila kwa mikakati iliyopo ya sasa ya CHADEMA kuwafikia wananchi ni tosha kabisa kuleta mageuzi nchini.

Mwisho nashukuru kwa nia njema uliyo nayo kwa Chama chetu japo jina lako ni bagamoyo nyumbani kwa hasimu wetu wa kisiasa?
 
Ni muhimu sana kwa CDM kuwa na chombo chake cha habari. So far ni gazeti la Mbowe na vyombo vingine vichache kabisa ndivyo vinavyoitangaza Chadema.

Good idea. Bravo!
 
Usitake kuingiza CHADEMA kwenye mkenge. Chadema staili yake ya kuendesha 'elimu kwa umma' kwa kutumia mikutano ya wazi na wananchi inatosha kuwaelewesha wananchi haki zao za msingi.

Historia inaonyesha kuwa ukianzisha vyombo rasmi vya kuwasiliana na wananchi kwa njia ya radio, TV au gazeti unakaribisha 'mamluki' kujipenyeza na kuchafua hali ya hewa.

CHADEMA iendelee kutumia mikutano na wanachi ili kuishitaki serikali ya CCM kwa kutowajibika kwa wananchi masuala ya RADIO UHURU, STAR TV, magazeti ya UHURU/MZALENDO/DAILY NEWS waachiwe CCM. CHADEMA tayari ina safu za viongozi na makada na wapenzi wake ambao wanatosha kusambaza 'elimu kwa umma juu ya siasa' na hakuna mantiki ya kuingia gharama ya vyombo rasmi vya habari.

Midahalo ambayo CCM huikimbia CHADEMA wanaitumia kikamilifu, vyombo huru kama JamiiForums CHADEMA inashiriki kikamilifu kutetea hoja zake. Mitego hii ya kutaka kuingiza mkenge CHADEMA gharama zisizo na tija inafaa kuepukwa kama suala hili la kuwa na TV/RADIO/Magazeti rasmi.

Haya ni mawazo ya CCM
 
vituo vya tv/radio ni gharama kuviendesha na kutumia ruzuku za vyama (chadema) kuendesha vyombo vya habari haina tija zaidi ya mikutano ya chadema na wananchi/kuboresha ofisi/mitandao vyuoni n.k

  • pia chadema kupata source/vyanzo vya hela nje ya ruzuku(matangazo ya biashara/wadhamini) kwa sasa ni mtihani mkubwa
  • gharama za kuendesha vyombo vya tv/radio zitadhoofisha harakati zingine za kuwafikia wananchi kule walipo.
  • ikiwa gharama za tv/radio ni tshs. Billioni 1(clouds fm/radio uhuru bajeti zao ni mfano) kwa mwaka kwa uchache ni project isiyowezekana na ukienda ndani zaidi kufikia umma kona zote kupitia vyomb hivyo tv/radio ni changamoto. Bora kuwawezesha makada/viongozi mashinani/vyuoni n.k waendeleze moto wa chadema.
  • mamluki kuingiza studio 'nyaraka za siri za serikali' na kisha kukilaumu chadema ni rahisi au hata kuchoma moto vifaa ghali vya kutendea kazi studio baada ya gharama kubwa kuvinunua ni rahisi kwa mafisadi na kupelekea kukidhoofisha chama cha chadema.
niishie hapo kuna sababu nyingi tu za 'kiintelejensia' ila kwa mikakati iliyopo ya sasa ya chadema kuwafikia wananchi ni tosha kabisa kuleta mageuzi nchini.
nakubaliana na wewe ktk baadhi ya points, lakini kinachokera katika sertikali yetu ni ile kuwekewa vikwazo vya kuelimisha umma. Hicho kibali cha kutaka kukusanyika au kuandamana lazima polisi watoe na mara nyingi chadema hunyimwa hicho kibali. Ktk tv au redio ni rahisi kutoa dukuduku wakati huo huo badala ya kupanga siku ya kuandamana.
Nimewakilisha
 
Naunga mkono hoja.

Sio kuanzisha tv tu bali pia magazeti, majarida, midahalo/vipindi nk

Mtaji mkubwa wa Chadema ni kuwa tayari wameufikia umma kwa uncoventional means. Sasa sio dhambi kutumia advantages ya teknolojia.

Waweke utaratibu mzuri kisha tu kisha tuanze kuchangia
 
Usitake kuingiza CHADEMA kwenye mkenge. Chadema staili yake ya kuendesha 'elimu kwa umma' kwa kutumia mikutano ya wazi na wananchi inatosha kuwaelewesha wananchi haki zao za msingi.

Historia inaonyesha kuwa ukianzisha vyombo rasmi vya kuwasiliana na wananchi kwa njia ya radio, TV au gazeti unakaribisha 'mamluki' kujipenyeza na kuchafua hali ya hewa.

CHADEMA iendelee kutumia mikutano na wanachi ili kuishitaki serikali ya CCM kwa kutowajibika kwa wananchi masuala ya RADIO UHURU, STAR TV, magazeti ya UHURU/MZALENDO/DAILY NEWS waachiwe CCM. CHADEMA tayari ina safu za viongozi na makada na wapenzi wake ambao wanatosha kusambaza 'elimu kwa umma juu ya siasa' na hakuna mantiki ya kuingia gharama ya vyombo rasmi vya habari.

Midahalo ambayo CCM huikimbia CHADEMA wanaitumia kikamilifu, vyombo huru kama JamiiForums CHADEMA inashiriki kikamilifu kutetea hoja zake. Mitego hii ya kutaka kuingiza mkenge CHADEMA gharama zisizo na tija inafaa kuepukwa kama suala hili la kuwa na TV/RADIO/Magazeti rasmi.

Mimi sikubaliani na wewe. Huitakii mema cdm, nimekushtukia:help:
 
Chama cha Democrasia na Maendeleo (CDM) kina kila sababu sasa kuhakikisha kina azisha kituo cha TV, ili kuondoa hujuma tunazo zishuhudia katika TV yetu ya umma TBC dhidi ya kile kinachoonekana dhahiri kuziminya habari za chama hiki na wakati mwingine kutokukipa muda wa kutosha ukilinganisha na CCM. Wote tunaelewa kuwa chama hiki kimeonesha kukubalika na wengi hasa vijana wengi wao wakiwa mijini,nadhani hapa jitihada za makusudi zinahitajika zifanyike ili elimu ya mabadiliko ifike mpaka vijijini ambako CCM bado imepafanya kama mtaji wa chama.so nafikiri,kama cdm tv itaanzishwa na ikawa na uwezo wa kuchana mawimbi nchi nzima basi moja kwa moja CCM ijiandae kuzikwa rasmi 2015. Wito wangu kwa viongozi wa CDM kuandaa mkakati kabambe wa kitaifa waje nao kwa wapenzi na wanachama wote wa CDM bila kuwasahau hata wasiokuwa na chama ili kuendesha mchango wa fedha nchi nzima wa kuanzishwa kwa tv chadema je tuko tayari?.lakini nikileta hoja hii kwenu naomba pia nijulishwe je mamlaka ya anga hapa TZ ina kizuizi kisheria juu ya jambo hili kufanyika? Naomba kuwasilisha.

TBC = CCM
ITV = CCM
ATV = CCM
NK = CCM
Clouds ccm
Sasa jamii forum inawafikia watanzania wangapi. Tunataka kupata habari wakati muafaka. kama mtu mmoja anaweza kuendesha TV. peoples power itashindwa. Sisi wana falsafa tunataka live news za cdm, hatuzipati. Tutachangingia People's TV People's Power:love:
 
Vituo vya Tv/Radio ni gharama kuviendesha na kutumia ruzuku za vyama (CHADEMA) kuendesha vyombo vya habari haina tija zaidi ya mikutano ya CHADEMA na wananchi/kuboresha ofisi/mitandao vyuoni n.k
  • Pia CHADEMA kupata source/vyanzo vya hela nje ya ruzuku(matangazo ya biashara/wadhamini) kwa sasa ni mtihani mkubwa
  • Gharama za kuendesha Vyombo vya TV/Radio zitadhoofisha harakati zingine za kuwafikia wananchi kule walipo.
  • Ikiwa gharama za TV/Radio ni Tshs. Billioni 1(Clouds FM/Radio Uhuru bajeti zao ni mfano) kwa mwaka kwa uchache ni project isiyowezekana na ukienda ndani zaidi kufikia umma kona zote kupitia vyomb hivyo TV/Radio ni changamoto. Bora kuwawezesha makada/viongozi mashinani/vyuoni n.k waendeleze moto wa CHADEMA.
  • Mamluki kuingiza studio 'nyaraka za siri za serikali' na kisha kukilaumu CHADEMA ni rahisi au hata kuchoma moto vifaa ghali vya kutendea kazi studio baada ya gharama kubwa kuvinunua ni rahisi kwa mafisadi na kupelekea kukidhoofisha chama cha CHADEMA.
Niishie hapo kuna sababu nyingi tu za 'kiintelejensia' ila kwa mikakati iliyopo ya sasa ya CHADEMA kuwafikia wananchi ni tosha kabisa kuleta mageuzi nchini.

Wapenzi wa Chadema wanaweza kukaribishwa kununua hisa ili kujenga na kukuza mtaji na wakaweka management ya kuendesha vyombo hivyo vya habari
 
nakubaliana na wewe ktk baadhi ya points, lakini kinachokera katika sertikali yetu ni ile kuwekewa vikwazo vya kuelimisha umma. Hicho kibali cha kutaka kukusanyika au kuandamana lazima polisi watoe na mara nyingi chadema hunyimwa hicho kibali. Ktk tv au redio ni rahisi kutoa dukuduku wakati huo huo badala ya kupanga siku ya kuandamana.
Nimewakilisha

Ndgu Bagamoyo, kwa ufupi ni kwamba kila kitu kina gharama. Kuwa na tv/redio kuna gharama na kutokuwa navyo pia kuna gharama zake. Pima faida ya kufanya hilo jambo. Je kuna gharama gani inayozidi uhai na ustawi wa mwandamu, kwa maudhiu hii ya mTz?

- Kuwa source/vyanzo vya hela nje ya ruzuku ni mtihani mkubwa kwa sasa.......... kwa nini? Wanatakiwa kufuata tu principles za biashara i.e. kuwa na competent marketing strategies and quality brand nk
- Kuogopa gharama (eti kwa sababu bajeti ya uendeshaji ni Tshs 1b+) ni udhaifu na ulegevu wa fikra. Hao wenye kuweza wanafanyaje?
- Kwa nini unadhani kuwa na tv/redio kutadhoofisha harakati nyingine za ukombozi wa Tz?
- Sababu ya hujuma (za aina yoyote) ni jambo la kawaida katika maisha na mazingira ya kisiasa kwa hiyo kuwa na tv au kutokuwa nayo hakuondoi uwepo wa hujuma. Hujuma zipo na zitakuwepo kadiri aishivyo mwandamu chini ya jua.
 
Mimi nafikiri si CDM TV tu bali na redio pia. Ni muhimu sana kupata ya upande wa pili kutoka vyanzo unavyo viamini kuliko kuwekewa maneno mdomoni na vyanzo usivyoviamini tena kwakati ambao si sahihi.
 
Wazo zuri sana la kuwa na Vyombo vya habari, itasaidia hata kupata habari zikiwa na ukweli, Vyomb vingine vikichakachua CDM TV inaweka ukweli hazarani, tupo tayari kuchangia.

tupo wengi sana wapenda Chadema, na tukihamasishana yanaweza kusanywa mamilioni.
 
nakubaliana na wewe ktk baadhi ya points, lakini kinachokera katika sertikali yetu ni ile kuwekewa vikwazo vya kuelimisha umma. Hicho kibali cha kutaka kukusanyika au kuandamana lazima polisi watoe na mara nyingi chadema hunyimwa hicho kibali. Ktk tv au redio ni rahisi kutoa dukuduku wakati huo huo badala ya kupanga siku ya kuandamana.
Nimewakilisha

Wakuu,
Naona mjadala wa changamoto inayoikabili CHADEMA kuwa na vyombo vyake rasmi vya habari umekuwa mzuri na utasaidia hatimaye kufikia maamuzi wa nini kifanyike, mitego gani ya kuiepuka na suala la uhuru wa habari kutiwa ndani ya KATIBA MPYA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA baada ya Wana-JF kuchanganua kwa kina hoja zote tulizozileta hapa na ndiyo uzuri wa JamiiForums.

[Adui mwingine kwa vyombo vya habari ni mahakama. Mahakama mara nyingine hutoa adhabu kali dhidi ya vyombo vya habari kwa kuvitaka kulipa fidia kwa watu waliokashifiwa kiasi kwamba kulipa fidia hizo kunaweza kusababisha chombo kukosa mtaji na hivyo kufutika katika ramani ya nchi.

Adui mwingine kwa vyombo huru vya habari Tanzania ni :''Mwaka 2006, wadau wa habari nchini walianzisha mchakato maalum wa kudai sheria ya haki ya habari ambapo waliandaa rasimu mbadala na kuiwasilisha kwa serikali mwaka 2008. Hata hivyo, tangu wakati huo serikali bado inasita kupeleka sheria hiyo Bungeni''.

Source: http://www.ipsinternational.org/africa/sw/nota.asp?idnews=3815]
 
Suala la msingi la kujiuliza hapa ni kwamba; je kuna chombo cha habari gani ambocho kipo huru mithili ya Aljazira. Mimi nionavyo kwa Tanzania hakuna. hivyo tunahitaji kuwa informed sio kila siku kula taarifa zilizochujwa na kuchakachuliwa. Kuna hili la kukipa chama fulani extra coverage, limeonyeshwa na TBC. Wakati ulani kunakuwa na matukio makubwa ya kitaifa lakini TBC huwa ya mwisho kuingia, mfano mabomu ya gongolamboto. Kuna midaalo mizuri ya Taifa, kama hii ya katiba TBC Bubu. Sio wote tunaweza kuingia uwanja wa taifa lakini TV na Radio zinaweza kusaida kupata Taarifa.

Sasa CDM itakapoanzisha au kuwezesha kuanzisha free news broadcasting system:
Naamini itakuwa ya mfano kwani wao wako makini
Itatoa nafasi kwa vyama vingine vichanga
Itatoa nafasi kwa wasomi
Itatoa nafasi kwa wanyonge
Itatoa elimu kwa umma, na mengine mengi

Nategemea MH Myika Kutoa Msimamo kuhusu hili:hug:
 
Ndoto hiyo inhgetimia inge mkomboa kila mtanzania kifikra na kumpa mwanga mpya mtanzania
Binafsi naipenda chadema zaid ya kawaid kiasi cha kufikiri zaid namna ya
Kukichangia chamachetu.
 
Huu si wakati wa kukimbia gharama yoyote,sababu kutokuwa vyombo vya habari ambavyo vitafanya coverage ya kutosha ni kudhoofisha.DR tuko tayari kununua hisa kwa ajili ya PEOPLE TV.
 
Wakuu,
Naona mjadala wa changamoto inayoikabili CHADEMA kuwa na vyombo vyake rasmi vya habari umekuwa mzuri na utasaidia hatimaye kufikia maamuzi wa nini kifanyike, mitego gani ya kuiepuka na suala la uhuru wa habari kutiwa ndani ya KATIBA MPYA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA baada ya Wana-JF kuchanganua kwa kina hoja zote tulizozileta hapa na ndiyo uzuri wa JamiiForums.

[Adui mwingine kwa vyombo vya habari ni mahakama. Mahakama mara nyingine hutoa adhabu kali dhidi ya vyombo vya habari kwa kuvitaka kulipa fidia kwa watu waliokashifiwa kiasi kwamba kulipa fidia hizo kunaweza kusababisha chombo kukosa mtaji na hivyo kufutika katika ramani ya nchi.

Adui mwingine kwa vyombo huru vya habari Tanzania ni :''Mwaka 2006, wadau wa habari nchini walianzisha mchakato maalum wa kudai sheria ya haki ya habari ambapo waliandaa rasimu mbadala na kuiwasilisha kwa serikali mwaka 2008. Hata hivyo, tangu wakati huo serikali bado inasita kupeleka sheria hiyo Bungeni''.

Source: TanzaniaMashirika ya Kiraia Yadai Uhuru wa Habari]

Hiyo Tv itakuwa ya kukashifu watu nini?!
 
Wacheni kuwa na uoga wa gharama za information. Information is power, mikutano ya hadhara ina nguvu kiasi lakini vyombo vya habari, yaani radio na TV vinaweza kuwafikia mamilioni ya wananchi hata wanapokuwa shambani. Humu JF kuna majasusi wasioitakia mema cdm. Sishangai mtu kuona TV na Radia kwa mazingira tuliopo sio muhimu. Wataimaliza CDM. Kama huamini angalia TBC sasa utaona taarifa ya mwanzo katika taarifa ya haba ni nini kama sio CCM, Nape na Mukama.

Wake up and stand up for you nation:whoo:
 
Back
Top Bottom