Nabii Huwa Hakubaliki Nyumbani, Japo Alikuwa ni Ripota wa TBC, Unabii Wake Aliufanyia Star TV. Ni Moses Mathew, Mbuyu wa Habari Mwanza ulioanguka

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,503
113,616
Nabii Huwa Hakubaliki Nyumbani, Buriani Moses Mathew, Mchango wako Sekta ya Habari, Una Thamani Kubwa Kuliko Status ya Ajira Yako.

Kwa wiki tatu mfulululizo, safu yangu imejikita kwenye Makala za Tanzia, nilianza na Rais Mstaafu wa Awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi, wiki iliyopita ilikuwa ni Tanzia ya mwanajamii Mzalendo Sanctus Mtsimbe, na wiki hii ni Mwanahabari, Moses Mathew, ripota wa TBC Mwanza ambaye tumempumzisha jana kwenye nyumba yake ya milele.

Jina la Moses Mathew, linaweza lisiwe jina maarufu kwa wengi kwasababu mwanahabari huyu alikuwa ni ripota tuu wa TBC Mwanza, tena baada ya kufariki ndio nikajua kuwa alikuwa ni Correspondent tuu na si muajiriwa rasmi wa TBC. Alifariki siku ya Jumatano wakati akipatiwa matibabu hospitali ya Bugando jijini Mwanza.

Kwanza nitoe pole kwa familia yake kumpoteza mwana familia nguzo, ni baba wa familia, ni mume, ni mtu aliyetegemewa na familia, ndugu, jamaa na marafiki, poleni sana wana familia wa Moses Mathew na wat oto wake 3 aliotuachia sasa ni watoto wetu.

Pili nitoe pole kwa TBC kumpoteza ripota wake mahiri, pole za TBC, zinaandamana na pongezi kwa TBC, kuubeba huu msiba. Pongezi hjizi kwa TBC ni kufuatia Mosses Mathew alikuwa sio muajiriwa wa TBC, ni correspondent tuu. Mtu unapokuwa ni correspondent tuu, unafanya kazi kama kibarua, mwajiri anawajibika kukupa malipo ya jasho lako tuu, lakini mengine yote, hayamhusu.

Lakini kwa TBC, ya Dr. Ayub Rioba, hali ni tofauti, kiukweli TBC imejitoa kikamilifu kuubeba huu msiba kikamilifu, na huu sio msiba wa kwanza, TBC imekuwa ikifanya hivyo hata huko nyuma, huu ni upendo mkubwa na kuwajali sana watumishi wake, Dr. Ayoub Rioba na TBC nzima, kwenye hili, wanastahili maua yao.

Hii ni kufuatia kilichowahi. Kutokea kwa mwanahabari, Daudi Mwangosi, nay eye umauti ulimkuta akiwa ni correspondent tuu.

Nitoe pole kwa Mwanza Press Club, na sekta nzima ya habari kumpoteza mwandishi mkongwe na mahiri, wa habari.

Mimi na Moses Mathew.
Nilikutanishwa kwa mara ya kwanza na Moses Mathew, na mwanahabari nguli Dotto Emmanuel Bulendu kupitia kipindi cha Jicho Letu Ndani ya Habari, kinachorushwa hewani na Star TV, ndipo nikamgundua Moses Mathew, ni miongoni mwa waandishi wa habari wa vyombo vya utangazaji ambaye yuko very bold, nyeusi ataita nyeusi na nyeupe anaita nyeupe, kitu ambacho kilichangamsha sana Jicho Letu.
Hizi ni baadhi ya mada alizoshiriki
- M/Kiti wa TEF, Deodatus Balile, M/Kiti wa MPC, Edwin Soko, Moses Mathew wa TBC na Manguli, Chini ya Dotto Bulendu na Pasco Mayalla Live on Star TV.

View: https://youtu.be/3udVN-QPkf4


Baada ya Dotto Bulendu kupumzika, kipindi kiliendeshwa na Angalieni Mpendu, Moses Mathew akiwa ni miongini mwa washiriki maarufu, na baada ya Angalieni Mpendu kustaafu, kipindi hicho nilikabidhiwa mimi, Moses Mathew, akiendelea kuwa mualikwa maarufu.

Kwa mimi, ikanitokea bahati, siku nakabidhiwa kuendesha kipindi cha Jicho Letu, siku ya kwanza nilikuwa na Moses Mathew, na siku ya mwisho, mimi nilipoaga rasmi kuendesha kipindi pale Star TV, niliaga kwa Aloyce Nyanda akiwa na Moses Mathew.
View: https://youtu.be/Qr6j25jFGyI?feature=shared
- Vyombo Vya Habari Vya Tanzania, Havina Uwezo wa Uchambuzi wa Habari, News Analysis-Jicho Letu

Nabii Hakubaliki Nyumbani.
Japo Moses Mathew kwa TBC alikuwa ni ripota tuu, yaani nyumbani TBC alikuwa ni ripota lakini kwa jirani Star TV, alikuwa ni tegemewa sana. Kwa mujibu wa misingi na maadili ya uandishi wa habari, maoni ya mwandishi, sii sehemu ya habari, hivyo Moses Mathew, hakuweza kutatumia maoni yake TBC, bali aliyatumia Star TV, hivyo Moses Mathew aliyekuwa anaonekana Star TV, ni Moses Mathew maarufu Zaidi kuliko yule Moses Mathew wa TBC, kwasababu, umaarufu wa Moses Mathew Star TV ni maoni yake, ambayo siku zote yanasimama, yaani hapindi, hakunji wala habembelezi!.

Waandishi Maguli Kufanya Kazi za Vijana.
Kila baada ya kipindi, nilikuwa namshauri, kwanini asianzishe kipindi kama hicho TBC, yeye ni nguli wa rika langu, hivyo nikashauri, waandishi na watangazaji manguli, wasifanye kazi za vijana, reporting tuiwaachia vijana. Sisi manguli tuendeshe vipindi. Akaniambia pale si unapajua maana ulikuwepo, labda nyinyi ndio mnisemee kwa wakuu wangu.

Alikuwa Very Bold.
Moja ya sifa za ziada za waandishi wazuri wa habari, ni kitu kinachoitwa boldness, mwandishi unasimamia ukweli bila kujali ukweli huo utamfurahisha nani au utamchukiza nani, kwenye ukweli, Mosses Mathew, siku zote alisimama na ukweli, aliamini kwenye kweli na siku zote alizungumza ukweli. Siku za hivi kumezuka kada mpya ya vyombo vya habari na waandishi wa habari, hii ni kada ya vyombo vya habari vya kichawa, na waandishi wa habari machawa!, Moses Mathew sii miongoni mwao!. Alikuwa too bold hadi watazamaji ma chawa chawa wakawa hawampendi! Dotto Bulendu: Usimwalike tena Moses Mathew katika mjadara wowote STAR TV
- Jicho letu ndani ya habari Star Tv huyo Moses Mathew mmemtoa wapi?

Buriani ya Kuonana

Ndugu yetu Moses Mathew, japo sisi tulikupenda, lakini Mungu amekupenda Zaidi,
Umepigana vita vilivyo vitakatifu, Mwendo umeumaliza, Imani umeilinda.

Bwana Alileta, Bwana Ametwaa, Jina Lake Lihimidiwe.

Buriani ya Kuonana, Moses Mathew.

Paskali.
 
Duh

RIP Moses

Nakumbuka kwenye mijadala pale Star tv kwa Dotto Bulendu alikuwa anawapa changamoto Sana Wanasiasa uchwara hasa Patrobas Katambi na Msukuma wakati ule akiwa Diwani na Geita haijawa mkoa
 
Huyu umepamba sana kwa kuwa ni marehemu, lakini kiuhalisia hakuwa mwandishi mwenye fikra huru. Yeye mda wote alikuwa ni kuitetea serikali hata pale ambapo ilikuwa dhahiri kuna tatizo. Alikuwa mbishi bila hoja. Kwa kifupi alikuwa kibaraka wa watawala kama Lucus Mwasha...
 
Kwanza nimtakie akae mahali pema huko peponi. Naona umeaamua kumpamba tu kuwa alikuwa anaweza kusimamia ukweli, kiukweli hakuwa anaweza kusimamia ukweli, Bali alikuwa anasimamia kinachotakiwa na serekali, na ilikuwa ikitokea kikawa kweli, hapo ndio inakuwa kasimamia ukweli. Ukisema alikuwa mbishi nitakuelewa.

Ni kama ww, acha nikuambie kabisa hata ikitokea ukafa Leo, maoni yangu itakuwa ulikuwa chawa uliyetaka uonekane unasimamia ukweli. Sana sana sifa uliyonayo ni mtu unayeongea kwa upole, na huna jazba. Lakini sifa yako kuu ni chawa mstaarabu.
 
Kuwa chawa siyo sifa, ni ujinga. Mwanaume jisimamie, utaishi hata usipobembeleza. Kifo kiko kwa kila kilicho hai.
 
Back
Top Bottom