John Mnyika anaongea kuhusu mapendekezo ya CHADEMA kuhusu miswada iliyopelekwa bungeni

Rabbon

JF-Expert Member
Apr 16, 2022
15,107
22,555
Salaam, Shalom!!!

Hii ni dira muhimu kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.

Katibu MKUU wa Chama Cha DEMOKRASIA na Maendeleo CHADEMA, ndugu John Mnyika amefanya Press Conference na vyombo mbalimbali vya habari nchini Kutoa ufafanuzi juu ya HOJA mbalimbali kujibu HOJA ikiwamo Ile iliyoibuliwa na Msemaji wa Chama Cha MAPINDUZI jana.

Ndungu Mnyika ametoa ufafanuzi kama ifuatavyo;

Amesema kuwa, barua iliyoandikwa na CHADEMA ya tarehe 19 July 2023 haijajibiwa na mamlaka Hadi Leo,

Barua hiyo iliandikwa kuhoji uhalali wa Miswada minne iliyopelekwa bungeni November mwaka huu , kwamba Ili miswada hiyo ili iwe halali, ilipaswa kwanza kupelekwa mswada wa mabadiliko ya Katiba kubadili vipengele muhimu, ndipo muswada wa Tume huru ya Uchaguzi ufuate.

Ndugu Mnyika amedai kuwa, CHADEMA kama chama kikuu Cha Upinzani kinachojitambua, kamwe hakiwezi kwenda Kutoa maoni katika Tume hiyo ambayo ni kiinimacho kubariki uchafuzi.

Amedai, maoni yanayotolewa sasa hayatafanyiwa KAZI Kwakuwa Katiba haijabadilishwa katika vipengele muhimu vinavyogusa Tume ya Uchaguzi,hivyo maoni hayo hata yakitolewa na wadau, kamwe hayatopokelewa na kufanyiwa KAZI, hapatakuwa na Tume huru ya Uchaguzi inayotakiwa na wananchi.

Ndugu na Kamanda Mnyika ameshauri, Serikali ipeleke muswada wa Mabadiliko ya Katiba kwanza hapo January 2024 na kuingiza vifungu muhimu Ili kuwezesha Tume huru ya Uchaguzi ya Kweli iweze kupatikana kabla ya Uchaguzi wowote.



Source: jambo, Tv., Wananchi Tv.

Mungu ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo TANZANIA 🇹🇿

Mungu ibariki CHADEMA!!

Amen.
 
Hongera CDM,

Hongera JJ Mnyika, HAKIKA mnaitendea HAKI nafasi ya kuwa Chama kikuu Cha siasa nchini.
 
Back
Top Bottom