Nilipewa na mkaka wa ofisini, baada ya kuona anaweza kumsaliti mchumbaye aliyekuwa shuleni (binti alikuwa anamtega kwa madai ya huyo kaka)
mdogo wako wa kiume how old is he?
walibaki peke yao kwa siku ngapi?
pole kaunga....
Zungumza na huyo binti kwa upole na upendo akutajie mwenye mzigo ni nani....
Ukishamjua (awe mdogo wako au mtu wa nje) uwasiliane nae kujua what next.....
Anaweza kuendelea kukaa hapo mpaka mwezi wa 7 msaidie vyote vya muhimu arudi kwao kujifungua..... Au
Kama mwenye mtoto ni mdogo wako then zungumza na wazazi na mhusika jinsi nduguyo atakavyomlea mtoto.....
Then baada ya kujifungua unaweza kuangalia kama atarudi kufanya kazi au vipi....
Kuhusu kuongea naye, nimeongea naye saana tu. Na nilipanga nimuendeleze kielimu baada ya kunisimulia historia yake (baba yake alimwambia afeli mtihani kwa kuandika madudu kwenye mtihani wa darasa la saba; kama ulishasikia wazazi wa Kibondo wanavyofanya).
Nina wasiwasi na mdogo (cousin) wangu, coz alishamsimulia niece wangu kwamba HG wangu alikuwa anampigia simu usiku wa manane hadi mdogo wangu akatofautiana na girlfriend wake. She (my maid) is very seductive, nilimchukua toka kwa kaka mmoja tunayefanya naye kazi baada ya kile alichokiita kutegwa na binti; ndio maana nahisi my cousin could not resist her, na ukizingatia ni kazuri!
Wasi wasi wangu hatasema ukweli, na pia ninaanza kuwa na mashaka maana kesho tu nitasafiri; hakawii kutoroka baada ya kuniliza.
hata leo wewe ongea nae. wewe ni mtu mzima, usimwonyeshe namna usivyokipenda hicho kitu. ongea nae kwa kawaida tu , ukichukua hiyo ni kama jambo la kawaida kabisa. atasema kila kitu. nimekusoma kuwa utasafiri karibuni. sasa hapo ndo hakikisha unaongea nae kabla hujaondoka kwani ukiondoka bila yeye kujua wewe ukijua utalipokeaje lazima akutoroke. aidha akisha sema ni nani, kinachofuata sasa ni wewe kumpa maneno mazuri zaidi, ili aangalie nyumba, ukiwa safari ndo utazidi kutafakari proper handling ya mustakabali wake, na ukirudi utakuwa kwenye nafasi ya kuamua vizuri zaidiAisee nashukuru sana kwa ushauri na kushare experience yako. Je niongee naye leo au niache siku zipite kidogo?
Jamani nimejitahidi kumcouncil ndio maana akaweza last hata that long, halafu kwangu hakuna wanaume zaidi ya mlinzi wa usiku ambaye ni mzee mzee.
Aisee, wewe ulijitafutia balaa. Angeweza kumtega hata kakako wa tumbo moja. Na cousin wako alipokuja ungewakemea wote. Anyways, too late, usimuache hapo wkwako alone. Kama una ndugu wa kumuachia for a few days umuache ili ukija ushughulikie issue yake itakuwa vyema. Otherwise, ongea nae usiku huu. Mpe nauli na mtaji kama wa laki akaanze genge kijijini. Kama kuna kufuatilia mchumba utarudi baadae ukiwa na nafasi.
Swali kwako, yule shemeji yangu wa kigoma sasa nae hajategwa? Unafuga maradhi mabaya aisee, alipofika ungemuwashia moto kuhusu seduction, dah.
Jamani nimejitahidi kumcouncil ndio maana akaweza last hata that long, halafu kwangu hakuna wanaume zaidi ya mlinzi wa usiku ambaye ni mzee mzee.
hata leo wewe ongea nae. wewe ni mtu mzima, usimwonyeshe namna usivyokipenda hicho kitu. ongea nae kwa kawaida tu , ukichukua hiyo ni kama jambo la kawaida kabisa. atasema kila kitu. nimekusoma kuwa utasafiri karibuni. sasa hapo ndo hakikisha unaongea nae kabla hujaondoka kwani ukiondoka bila yeye kujua wewe ukijua utalipokeaje lazima akutoroke. aidha akisha sema ni nani, kinachofuata sasa ni wewe kumpa maneno mazuri zaidi, ili aangalie nyumba, ukiwa safari ndo utazidi kutafakari proper handling ya mustakabali wake, na ukirudi utakuwa kwenye nafasi ya kuamua vizuri zaidi
Jamani si unajua ninaye Eiyer tu ambaye yuko Mwanza. Huku nafanya kazi tu, sifanyi mahusiano! LOL
Thannks kwa ushauri, ngoja niongee naye kwa upendo kwanza nione reaction yake; kwa muda kuna msichana wa niece wangu hapa nyumbani so sidhani kama ataweza kuniliza; hana tabia ya wizi (ingawa haimaanishi hawezi kufikiria ukizingatia kwa muda huu atakuwa na mawazo mengi).
inategemea na tolerance yako.
Kuna mama jirani yangu ilikuwa hivi.
Kaleta dada mpya, kakaa kama wiki 1
yeye anashinda kazini.
Jioni karudi, dada kaja fungua geti kama kawaida.
akaingia chumbani kwa dada
anakuta shuka zimejaa damu tele
taharuki, kuna nini
pekua pekua wanagundua mtoto hai kaviringishwa kwenye mashuka.
Wanampeleka dispendary, wote wako safi.
Nini wafanye?
Wanaamua kumpa nafasi sababu hakuwa na pa kuanzia.
Dada anaendelea ka kazi na kichanga chake
kaishi nao zaidi ya 8years hadi alipoolewa.
Ila huyu mama alikuwa na watoto wote wako boarding, alihitaji mtu wa kulinda nyumba tu mchana.
Sasa wewe waweza muacha, kama una kifua ila kama huna basi arudi kwao.
Ila kabla hajarudi, hakikisha si wifi yako maana nalo lawezekana.
Mkalishe umweleze hali halisi na umshawishi asifanye jaribio la kutoa. Muulize baba mtoto ni nani, kutokea hapo sasa ndio utakuwa na cha kuamua ukiwa na details za kutosha.
inategemea na tolerance yako.
Kuna mama jirani yangu ilikuwa hivi.
Kaleta dada mpya, kakaa kama wiki 1
yeye anashinda kazini.
Jioni karudi, dada kaja fungua geti kama kawaida.
akaingia chumbani kwa dada
anakuta shuka zimejaa damu tele
taharuki, kuna nini
pekua pekua wanagundua mtoto hai kaviringishwa kwenye mashuka.
Wanampeleka dispendary, wote wako safi.
Nini wafanye?
Wanaamua kumpa nafasi sababu hakuwa na pa kuanzia.
Dada anaendelea ka kazi na kichanga chake
kaishi nao zaidi ya 8years hadi alipoolewa.
Ila huyu mama alikuwa na watoto wote wako boarding, alihitaji mtu wa kulinda nyumba tu mchana.
Sasa wewe waweza muacha, kama una kifua ila kama huna basi arudi kwao.
Ila kabla hajarudi, hakikisha si wifi yako maana nalo lawezekana.
Mkalishe umweleze hali halisi na umshawishi asifanye jaribio la kutoa. Muulize baba mtoto ni nani, kutokea hapo sasa ndio utakuwa na cha kuamua ukiwa na details za kutosha.
Sorry wifi, nilidhani wewe ndo uko mwanza.
kama kuna mtu muambie amuangalie. Usiwashe sana moto, muambie unafikiria umsaidieje. Ukinyamaza she will be more devastated. Muambie maisha ni kujifunza kwa makosa.
next time unapata kicheche upike biriani utuite tuje kumfunda kama bi ponza wa clouds,lol