Ushauri jamani, nimepewa taarifa binti yangu wa kazi ni mjamzito

Bushmamy

JF-Expert Member
Aug 18, 2019
8,848
15,253
Waungwana wa Jf,

Nimetoka mkoa ninaoishi nikasafiri mkoa mwingine kwa ajili ya mapumziko na kuweka akili sawa. Nyumbani nikimuacha binti wa kazi ambae nimekaa naye kwa muda wa mwaka mmoja sasa, ni binti mchapakazi, na asiye na kiburi na pia ni msafi sana, shida yake kubwa ilikuwa akiwa na mwanaume huyu akiachana nae ndani ya wiki anaye mwingine. Nilimuonya sana lakini ndo hivo, nikapiga simu kwa wazazi wake wakamuonya wala hakusikia.

Basi tukaamua tumuache kama alivyo ilmradi wajibu wake nyumbani anautimiza kwangu haikuwa shida, maisha yanaendelea.

Nikiwa huku ile wiki ya kwanza mwishoni napata simu kutoka kwa jirani 'Bushmamy kwema huko? Nikamjibu Nipo salama, akaendelea kusema kuwa binti yako ni mjamzito na inaonekana ana mimba ya miezi miwili maana alivyokuja hapa kwangu alisema ana kama miezi miwili hajaona siku zake, ndo nikamshauri akanunue kipimo kucheki ni Mimba tayari kinaonyesha"'akamaliza kuongea tukaagana.

Basi bwana mi nikaagiza Kilimanjaro ya baridi nikapiga pafu 4 ndo nikaanza kutafakari nafanyeje kwa sababu niliwaza yafuatayo:

Huyu binti nilimpenda tu vile hakuwa na kiburi.

Pili ni mchapakazi na msafi

Tatu kule kwao wanamtegemea kila mwezi atume hela ya kusaidia wazazi.

Nne ni mvumilivu katika hali zote za kiuchumi ninazopitia, na pia ni muaminifu sana hana tamaa na hela.

Pamoja na mambo mengine mengi tu maana nilipanga kuishi naye kabisa kama mdogo wangu ili baadaye nimpeleke ufundi cherehani au nimtafutie kazi lakini mambo ndo yameshakuwa hivyo maana hata hajui mimba ni ya nani.

Hadi sasa sijamwambia kama najua chochote kuhusu hali yake nasubiri nirudi.

Naombeni ushauri tafadhali maana binti ana miaka 20.
 
Umeshasema umekaa nae vizuri hadi ukafikiria kumpeleka ufundi cherehani, kama Upo vizuri kifedha mpe mtaji kiasi umrudishe kwao atajua yeye huko kwao kama atatoa Au atazaa! Mimba ni baraka na unaposhiriki kwa namna yoyote ile kufanikisha kuitoa basi dhambi hiyo na wewe ni yako, pia mimba Ina mambo mengi changamoto za hapa na pale (ukisema ukae nae) mrudishe kwao mpe hata laki 2/3 sio mbaya
 
Siwezi kabisa kujaribu kuitoa mimi
 
Waambie wazazi wake!!halafu aendelee na kazi kama kawa!muda wa kujifungua ukifika aende kujifungulia kwao akimaliza aje aendelee na kazi kama kawa!!mimba sio ishu mkuu!!kama vp nipe namba yake nimpongeze kwa kuibeba!!!watoto ni resource na nguvu kazi ya taifa!!!
Asante kwa ushauri
 
Kila mtu ataubeba mzigo wake mwenyewe rekebisha matendo yako utakua na msingi imara

Japo ni hater una wivu na kila mtu humu JF nimeshangaa maisha halisi una huruma za hivyo.

Fukuza tu akalee kwao utamu hauna kikomo ,akijifungua ataendelea tena na tena.
 
Mrudishe kwao..mpatie na kianzio Cha maisha ..ukimuonea huruma yatajirudia wengi ndivyo walivyo.

Housegal wa dada angu alipopata mimba alionewa huruma akakaa nae..alivyozaa akatafuta nyingine..zote baba hawajulikani dada akanawa mikono.
 
Sawa nimekusoma mkuu ila nikimfukuza nawaza kama nitapata binti wap binti mwingine ambae hata kama sipo nnakuwa na uhakika wa usalama watoto
 
Tatizo hujaangalia mbele zaidi,mimba zinabadili watu tabia je una uhakika wanao hawatateseka kuendana na mudi ya mimba ya dada wa kazi. Na akijifungua sidhan kama atakua na upendo kwa wanao kuliko mwanae,kuanzia kuchapa kazi,kuwahudumia kazi ndogo ndogo nk(usikaribishe 'mama wa kambo' kwa wanao ndani ya nyumba yako)
Sawa nimekusoma mkuu ila nikimfukuza nawaza kama nitapata binti wap binti mwingine ambae hata kama sipo nnakuwa na uhakika wa usalama watoto
 
Ndo walivyo maana wakiangalia wa kulea yupo hivyo wanajiachia.
Mrudishe kwao..mpatie na kianzio Cha maisha ..ukimuonea huruma yatajirudia wengi ndivyo walivyo.

Housegal wa dada angu alipopata mimba alionewa huruma akakaa nae..alivyozaa akatafuta nyingine..zote baba hawajulikani dada akanawa mikono.
 
Mpime Chai kwanza, ukimkuta hana chai mwache afanye kazi akusanye kahela hadi mimba ifikishe miezi nane ndio aende kwao akajifungue. Tofauti na hapo akiamua kwenda kwa mkulungwa wake mruhusu tu akajionee maisha.
 
Back
Top Bottom