Binti wangu wa kazi ni mjamzito; nifanyaje?

HIYO MIMBA UMEMPA WEWE HALAFU UNAKUJA TENA KUTUOMBA USHAURI...!!!!1 KICHAA KABISA. ANYWAY, MPE MSHAHARA WAKE ARUDI NYUMBANI AKALEE MIMBA NA UTUMUE MATUMIZI OTHERWISE TUNAKUFUNGA MIAKA 13 KWA KOSA LA KUMPA MIMBA BINADAMU WA KIKE CHINI YA UMRI WA MIAKA 18
 
Karibia mwezi umeisha msichana wangu akilalamika juu ya kuumwa na tumbo. Kazi yangu inanifanya niwe on the road almost 25 days of the month; hivyo amekuwa akienda hospt mwenyewe. Kama majuma mawili yaliyopita, alinifuata chumbani huku akilia akisema anaumwa sana, akaniletea cheti cha hospt, nikakuta amepimwa vipimo vingi including VDRL which was non reactive, ila mkojo ulikuwa na a lot of pus cells. Aliandikiwa sindano (sikumbuki jina) kama 7 hivi lakini alichomwa 5 na wakambadilishia dawa na kumpa ma Doxy ambayo yalimshinda kwani si mlaji mzuri, kwa kuwa nilikuwa nasafiri; nikamwambia aache hizo dawa anisubiri mpaka nitakaporudi.

Nimerudi juzi, jana nikampeleka govt hosp; majibu ya mkojo na vaginal swab yalikuwa okay, again VDRL was unreactive; walivyomwangalia uke (alikuwa analalamika ana vidonda) wamesema it is okay???; baadaye dr akaandika afanyiwe utra sound kuangalia pelvic infection, ndio natoka kwenye utra sound, matokeo ni kazygote ka 8 weeks.

Sijaongea naye chochote, na honestly sijui cha kuongea naye. Ni binti ambaye nimekaa naye kwa miaka kama 4 hivi, kitu ambacho nina uhakika nacho ni kuwa siwezi lea mtoto wake; kwani kazi yangu sio friendly na parenthood. Kingine ninacho ogopa ni the fact kuwa ndani ya miezi hiyo miwili alikuwepo mdogo wangu wa kiume aliyekuja field; huenda walijioa ninavyokuwa safarini.

Nishaurini ndugu zangu how do l first start councilling her, halafu namuulizaje kuhusu huyo aliyemmimba na mwisho ninamsaidiaje?

New updates
Wakati tunakula, ameanzisha maongezi yeye mwenyewe kwamba wali unamshinda. Nikapata nafasi ya kuanza kumuuliza kiutani (huwa ninamtania) kwamba ni nani mwenye bahati; akaguna. Kisha nikamuuliza huyo mtu ameshajua, akanod; nikamendelea kumprobe amesemaje, akainama huku machozi yakimlenga; nikamuuliza amekwambia muitoe? akasema ndio.
Nikamuuliza kwanini, akasema hajajiandaa na kwamba anaishi kwao bado (ni dreva wa mtu binafsi).

She is into deep thinking naye anawazia kuitoa, kisa hataweza kufanya kazi na hivyo ataishije. Baada ya kuongea naye sana, anasema mama wa huyo kijana ni nurse; nimemwambia nikirudi nitaongea naye, lkn bado ni mnyonge nafikiri akili yake kubwa iko kwenye kuutoa huo ujauzito. Ngoja niendelee kumcouncil, nipo naye hapa chumbani ananiuliza kwani akitoa atakufa.
Dada Kaunga, usitoe hiyo mimba. Kama umeipata toka mchepuko panga mkakati mbambikize boya wako yaani mme/ mpenzi wako.

Au kama wewe ni dume uliyempa mimba piga kifua ngumi kama sokwe kisha sema shabaaaash, ila umwambie asitoe hiyo mimba. Baada ya miaka 5 utakuja furahi mwenyewe haijalishi sasa hivi haujajipanga.
 
Dah, you have to be very carefully,

Kuna binti nilimrudishaga kwao kwa sbb kama hizo akaenda kuabort halafu akadedi. still I regret how nilimrudishaga.
 
Huu uzi wa kitambo sana

Halafu hapo naona kuna ID mbili zinajirudia ina maana NGABU ndio bwa'nchuchu
 
Back
Top Bottom