Binti wangu wa kazi ni mjamzito; nifanyaje?

Nilipewa na mkaka wa ofisini, baada ya kuona anaweza kumsaliti mchumbaye aliyekuwa shuleni (binti alikuwa anamtega kwa madai ya huyo kaka)

Duh,

Sasa wewe ushasikia binti mwingi wa habari na wewe ukasema "mlete huku"?
 
pole kaunga....

Zungumza na huyo binti kwa upole na upendo akutajie mwenye mzigo ni nani....

Ukishamjua (awe mdogo wako au mtu wa nje) uwasiliane nae kujua what next.....

Anaweza kuendelea kukaa hapo mpaka mwezi wa 7 msaidie vyote vya muhimu arudi kwao kujifungua..... Au
Kama mwenye mtoto ni mdogo wako then zungumza na wazazi na mhusika jinsi nduguyo atakavyomlea mtoto.....

Then baada ya kujifungua unaweza kuangalia kama atarudi kufanya kazi au vipi....

Nashukuru BADILI TABIA, nitafanya kama ulivyonishauri; ila najiuliza sijui nimuache kwanza adigest hiyo newz mwenyewe kwanza nimuulize siku nyingine au nimuulize leo leo?
 
Last edited by a moderator:
Kuhusu kuongea naye, nimeongea naye saana tu. Na nilipanga nimuendeleze kielimu baada ya kunisimulia historia yake (baba yake alimwambia afeli mtihani kwa kuandika madudu kwenye mtihani wa darasa la saba; kama ulishasikia wazazi wa Kibondo wanavyofanya).

Nina wasiwasi na mdogo (cousin) wangu, coz alishamsimulia niece wangu kwamba HG wangu alikuwa anampigia simu usiku wa manane hadi mdogo wangu akatofautiana na girlfriend wake. She (my maid) is very seductive, nilimchukua toka kwa kaka mmoja tunayefanya naye kazi baada ya kile alichokiita kutegwa na binti; ndio maana nahisi my cousin could not resist her, na ukizingatia ni kazuri!

Wasi wasi wangu hatasema ukweli, na pia ninaanza kuwa na mashaka maana kesho tu nitasafiri; hakawii kutoroka baada ya kuniliza.

Aisee, wewe ulijitafutia balaa. Angeweza kumtega hata kakako wa tumbo moja. Na cousin wako alipokuja ungewakemea wote. Anyways, too late, usimuache hapo wkwako alone. Kama una ndugu wa kumuachia for a few days umuache ili ukija ushughulikie issue yake itakuwa vyema. Otherwise, ongea nae usiku huu. Mpe nauli na mtaji kama wa laki akaanze genge kijijini. Kama kuna kufuatilia mchumba utarudi baadae ukiwa na nafasi.

Swali kwako, yule shemeji yangu wa kigoma sasa nae hajategwa? Unafuga maradhi mabaya aisee, alipofika ungemuwashia moto kuhusu seduction, dah.
 
Duh,

Sasa wewe ushasikia binti mwingi wa habari na wewe ukasema "mlete huku"?

Jamani nimejitahidi kumcouncil ndio maana akaweza last hata that long, halafu kwangu hakuna wanaume zaidi ya mlinzi wa usiku ambaye ni mzee mzee.
 
Mkuu maswali yako!!!, Kaunga hapo ndo busara inahitajika, i'm out for sometime i'll be back after a moment!
 
Aisee nashukuru sana kwa ushauri na kushare experience yako. Je niongee naye leo au niache siku zipite kidogo?
hata leo wewe ongea nae. wewe ni mtu mzima, usimwonyeshe namna usivyokipenda hicho kitu. ongea nae kwa kawaida tu , ukichukua hiyo ni kama jambo la kawaida kabisa. atasema kila kitu. nimekusoma kuwa utasafiri karibuni. sasa hapo ndo hakikisha unaongea nae kabla hujaondoka kwani ukiondoka bila yeye kujua wewe ukijua utalipokeaje lazima akutoroke. aidha akisha sema ni nani, kinachofuata sasa ni wewe kumpa maneno mazuri zaidi, ili aangalie nyumba, ukiwa safari ndo utazidi kutafakari proper handling ya mustakabali wake, na ukirudi utakuwa kwenye nafasi ya kuamua vizuri zaidi
 
Jamani nimejitahidi kumcouncil ndio maana akaweza last hata that long, halafu kwangu hakuna wanaume zaidi ya mlinzi wa usiku ambaye ni mzee mzee.

When you took that move,may be you were trying to help, please carry on even at this stage!
 
Pole sana Kaunga! Na kushauri uongee nae na umwambie ukweli kuwa huwezi kulea mtoto wake ili nae ajiandae jinsi ya kukabili maisha!

Mwambie akwambie ukweli hiyo mimba ya nani, na nikama ya ndugu yako, hapo itakubidi utumie busara maana itakuwa damu ya ndugu yako!

Sema nae ujue ukweli.
 
Aisee, wewe ulijitafutia balaa. Angeweza kumtega hata kakako wa tumbo moja. Na cousin wako alipokuja ungewakemea wote. Anyways, too late, usimuache hapo wkwako alone. Kama una ndugu wa kumuachia for a few days umuache ili ukija ushughulikie issue yake itakuwa vyema. Otherwise, ongea nae usiku huu. Mpe nauli na mtaji kama wa laki akaanze genge kijijini. Kama kuna kufuatilia mchumba utarudi baadae ukiwa na nafasi.

Swali kwako, yule shemeji yangu wa kigoma sasa nae hajategwa? Unafuga maradhi mabaya aisee, alipofika ungemuwashia moto kuhusu seduction, dah.

Jamani si unajua ninaye Eiyer tu ambaye yuko Mwanza. Huku nafanya kazi tu, sifanyi mahusiano! LOL
Thannks kwa ushauri, ngoja niongee naye kwa upendo kwanza nione reaction yake; kwa muda kuna msichana wa niece wangu hapa nyumbani so sidhani kama ataweza kuniliza; hana tabia ya wizi (ingawa haimaanishi hawezi kufikiria ukizingatia kwa muda huu atakuwa na mawazo mengi).
 
Last edited by a moderator:
inategemea na tolerance yako.

Kuna mama jirani yangu ilikuwa hivi.

Kaleta dada mpya, kakaa kama wiki 1
yeye anashinda kazini.
Jioni karudi, dada kaja fungua geti kama kawaida.
akaingia chumbani kwa dada
anakuta shuka zimejaa damu tele

taharuki, kuna nini
pekua pekua wanagundua mtoto hai kaviringishwa kwenye mashuka.

Wanampeleka dispendary, wote wako safi.

Nini wafanye?
Wanaamua kumpa nafasi sababu hakuwa na pa kuanzia.
Dada anaendelea ka kazi na kichanga chake
kaishi nao zaidi ya 8years hadi alipoolewa.

Ila huyu mama alikuwa na watoto wote wako boarding, alihitaji mtu wa kulinda nyumba tu mchana.

Sasa wewe waweza muacha, kama una kifua ila kama huna basi arudi kwao.

Ila kabla hajarudi, hakikisha si wifi yako maana nalo lawezekana.

Mkalishe umweleze hali halisi na umshawishi asifanye jaribio la kutoa. Muulize baba mtoto ni nani, kutokea hapo sasa ndio utakuwa na cha kuamua ukiwa na details za kutosha.
 
hata leo wewe ongea nae. wewe ni mtu mzima, usimwonyeshe namna usivyokipenda hicho kitu. ongea nae kwa kawaida tu , ukichukua hiyo ni kama jambo la kawaida kabisa. atasema kila kitu. nimekusoma kuwa utasafiri karibuni. sasa hapo ndo hakikisha unaongea nae kabla hujaondoka kwani ukiondoka bila yeye kujua wewe ukijua utalipokeaje lazima akutoroke. aidha akisha sema ni nani, kinachofuata sasa ni wewe kumpa maneno mazuri zaidi, ili aangalie nyumba, ukiwa safari ndo utazidi kutafakari proper handling ya mustakabali wake, na ukirudi utakuwa kwenye nafasi ya kuamua vizuri zaidi

Thanks again Kindimbajuu, nitaongea naye leo ngoja nimbembeleze ale, maana ulaji wake umekuwa shida sana!
 
Last edited by a moderator:
Jamani si unajua ninaye Eiyer tu ambaye yuko Mwanza. Huku nafanya kazi tu, sifanyi mahusiano! LOL
Thannks kwa ushauri, ngoja niongee naye kwa upendo kwanza nione reaction yake; kwa muda kuna msichana wa niece wangu hapa nyumbani so sidhani kama ataweza kuniliza; hana tabia ya wizi (ingawa haimaanishi hawezi kufikiria ukizingatia kwa muda huu atakuwa na mawazo mengi).

Sorry wifi, nilidhani wewe ndo uko mwanza.
kama kuna mtu muambie amuangalie. Usiwashe sana moto, muambie unafikiria umsaidieje. Ukinyamaza she will be more devastated. Muambie maisha ni kujifunza kwa makosa.
next time unapata kicheche upike biriani utuite tuje kumfunda kama bi ponza wa clouds,lol
 
inategemea na tolerance yako.

Kuna mama jirani yangu ilikuwa hivi.

Kaleta dada mpya, kakaa kama wiki 1
yeye anashinda kazini.
Jioni karudi, dada kaja fungua geti kama kawaida.
akaingia chumbani kwa dada
anakuta shuka zimejaa damu tele

taharuki, kuna nini
pekua pekua wanagundua mtoto hai kaviringishwa kwenye mashuka.

Wanampeleka dispendary, wote wako safi.

Nini wafanye?
Wanaamua kumpa nafasi sababu hakuwa na pa kuanzia.
Dada anaendelea ka kazi na kichanga chake
kaishi nao zaidi ya 8years hadi alipoolewa.

Ila huyu mama alikuwa na watoto wote wako boarding, alihitaji mtu wa kulinda nyumba tu mchana.

Sasa wewe waweza muacha, kama una kifua ila kama huna basi arudi kwao.

Ila kabla hajarudi, hakikisha si wifi yako maana nalo lawezekana.

Mkalishe umweleze hali halisi na umshawishi asifanye jaribio la kutoa. Muulize baba mtoto ni nani, kutokea hapo sasa ndio utakuwa na cha kuamua ukiwa na details za kutosha.

Thanks, Kongosho; deep down namuonea sana huruma. I real wish anitrust na kuniambia ukweli ili nione jinsi ya kumsaidia!
 
Last edited by a moderator:
inategemea na tolerance yako.

Kuna mama jirani yangu ilikuwa hivi.

Kaleta dada mpya, kakaa kama wiki 1
yeye anashinda kazini.
Jioni karudi, dada kaja fungua geti kama kawaida.
akaingia chumbani kwa dada
anakuta shuka zimejaa damu tele

taharuki, kuna nini
pekua pekua wanagundua mtoto hai kaviringishwa kwenye mashuka.

Wanampeleka dispendary, wote wako safi.

Nini wafanye?
Wanaamua kumpa nafasi sababu hakuwa na pa kuanzia.
Dada anaendelea ka kazi na kichanga chake
kaishi nao zaidi ya 8years hadi alipoolewa.

Ila huyu mama alikuwa na watoto wote wako boarding, alihitaji mtu wa kulinda nyumba tu mchana.

Sasa wewe waweza muacha, kama una kifua ila kama huna basi arudi kwao.

Ila kabla hajarudi, hakikisha si wifi yako maana nalo lawezekana.

Mkalishe umweleze hali halisi na umshawishi asifanye jaribio la kutoa. Muulize baba mtoto ni nani, kutokea hapo sasa ndio utakuwa na cha kuamua ukiwa na details za kutosha.

Ama sio mke mwenzie? Manake mdogo wangu Eiyer nae simuamini sana.
shosti wangu alipataga surprise ya kupigiwa na dada kuwa anaumwa kumbe anajifungua. Shosti alikuwa na twins and another son (3 sons watundu kama wamelogwa!), na huyo dada ndo alikuwa anawamanage vizuri. Waliamua kukaa nae lakini baada ya mwaka dada akahamia kwa boifurendi cum huzbendi. Hadi leo kazi zikizidi anakuja kupigatafu.
tatizo kaunga anasema lifetsyle yake haimruhusu kulea (manake hapo unalea mama na mtoto). Ila seriously mizigo ya kubebeshana siifyagilii hata kidogo! Asipoapata lesson huyu anazaa na wa pili hapohapo
 
Last edited by a moderator:
Sorry wifi, nilidhani wewe ndo uko mwanza.
kama kuna mtu muambie amuangalie. Usiwashe sana moto, muambie unafikiria umsaidieje. Ukinyamaza she will be more devastated. Muambie maisha ni kujifunza kwa makosa.
next time unapata kicheche upike biriani utuite tuje kumfunda kama bi ponza wa clouds,lol

Ha ha ha.....will surely do that my wi; nawaaminia katika kufunda mabinti.
 
Kaunga, naelewa mdada ukikaa naye zaidi ya miaka mitatu kumuondoa inakuwa inasumbua achia mbali huyu ana mimba.

Bila kujua ni ya nani utakuwa na maswali, labda mpigie cousin wako umuulize pia.

King'asti, duh, Eiyer from virgin to makombe ya samaki???? Kweli kila mtu alizaliwa virgin lol

ila kweli kulea mtoto wa dada wa kazi yataka moyo sana, heri yao kama waliweza.
 
Last edited by a moderator:
Pole sana...Kama nduguyo anahusika basi inabidi umsaidie kwa namna moja au nyingine na kwa kuwa hauko tayari kulea basi hakuna jinsi bali kumuomba aondoke
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom