Baba Kikwete Jiuzulu Kulinusuru Tanzania!

Muke Ya Muzungu

JF-Expert Member
Jun 17, 2009
3,444
264
Shkamoo Baba,
-Natumai mu wazima nyote hapo magogoni, Mimi ni mzima wa afya pamoja na wanangu na namshukuru Mwenyezi Mungu kwa yote hasa uhai nikiwa huku mitaa ya changanyikeni. Kama mzazi na Rais wangu, kwa miaka zaidi ya tano tangu uingie madarakani, nimekuwa uraiani nikiangalia hali halisi ya nchi yetu, na napenda niwe mkweli kwa kukuletea taarifa ya ukweli ambayo wengi wanaokuzunguka wanakuficha. Ukweli ni Kwamba, hali ya watanzania ni mbaya.

Umasikini umelilemea taifa. Vilio na majonzi kila kona; Ufisadi katika kila nyanja, Rushwa iliyokithiri, Uonevu wa polisi na kutokuwepo haki mahakamani kwa walalahoi. Hakuna haki kwa masikini. Wenye madaraka wamewageuza wananchi kama watumishi wao. Jana nimepita pale hospitali yetu kuu ya muhimbili na ninasikitika kukutaarifu kwamba, hali ni mbaya, watu wanakufa. Jariku uende ujionee mwenyewe hali inavyotisha kutokana na mgomo wa madaktari. Kadhalika nimekuwa nikizunguka maofisini ambako nimekutana na viongozi wengi wa serikali na kusema kweli wameichoshwa na uongozi wako

-Baba, kumbuka kwenye kampeni yetu, tuliwaahidi watanzania maisha bora kwa kila mtanzania, kwa bahati mbaya hii ahadi imegeuka kuwa kinyume. Maisha magumu kwa kila mtanzania. Ninapotembea mitaani wale wote niliowapa Kanga na kofia nikiwaona najificha kwani ahadi nilizowapa nikinunua kura zao nimeshindwa kuzitimiza. Baba, siwezi kuendelea kujificha kutokana na aibu.Sehemu nyingine nazomewa. Hata marafiki zangu ambao ndiyo wengi waliokupigia kura hawataki kuniona. Hebu fikiria mama lishe siku moja alimmwagia shemeji yangu chai usoni aliposema kwamba " hii nchi bila CCM haitakuw ana muelekeo? Hii inaonyesha ni kiasi gani tumewachosha !


- Fanya ustaarabu ujiuzulu kuilinda Tanzania. Tunakoelekea ni kubaya, kwa heshima yako na hatima ya taifa, ni vyema zaidi uachie madaraka kuliko yakukute mabaya tusiyokutakia. Tafakari ugumu wa maisha unaomkabili raia wa kawaida. Nchi imelemewa na matatizo, Migomo ya wafanyakazi, vurugu za kisiasa ndani ya serikali na chama chako ni ishara tosha kwamba nchi HAITAWALIKI. Nje ya nchi tunazidi kujidhalilisha hasa ukizingatia matusi tunayomiminiwa tukiitwa MAZEZETA ombaomba. Kuachia madaraka siyo kushindwa bali ni kuonyesha ujasiri na uzalendo wa hali ya juu kwani utakuwa umeweka maslahi ya nchi mbele ya maslahi yako binafsi. Baba naomba uikomboe Tanzania kwa kujiuzulu. Asnate kunisikiliza

Bintiyo

 
Dada ujumbe mzito kweli kweli, tuombe mungu umfikie lakini kwa jinsi anavyopenda madaraka kama mwai wa kibaki sidhani barua yako ataishugulikia
 
eti maisha bora. muda wote unazunguka mitaani halafu unataka maisha bora. huu si uchizi. hata huko ulaya maisha bora hayaji kwa kuzunguka mitaani.
 
Kwa umaskini uliopa pale hazina, hata akijiuzulu sidhani kama kuna uwezo wa kufanya uchaguzi mkuu. Nashani yule Mnyukilia ataongoza mpaka 2015. Hakutakuwa na mabadiliko ya maana labda kwa kuwa ni Mzanzibari (kero za ''muungano'' zitapungua kwa upande wa visiwani na kuongezeka kwa Watanganyika)
 
Daaahhh, dada JichoD huu uchambuzi wako si matani jamani. Kama kweli kuna mtu anayejali kuli Magogoni basi pengine ujumbe huu utazingatiwa kwa kina na uzito unaostahili.
 
Kuna jamaa mmoja alinipigia simu akasema ikitokea ukasikia msafara wa Rais umelipuliwa na ukapiga simu yangu haipatikani basi ujue nimehusika! Hii ni kuonyesha jinsi gani watu wamechoka na huyu janga aitwae JK!
 
Jamani muogopeni Mungu, asilimia tisini ya matatizo yaliyopo sasa hivi Jk kayakuta, mfano ufisadi wote kwenye madini, umeme na Epa vimefanyika wakati wa Mkapa.Leo hii Jk anatupiwa lawama ambazo kimsingi kazikuta, sidhani hata kama angepewe nchi huyo Slaa wenu kama angeweza fanya chochote zaidi ya kusema kuwa ilani yetu iko hivi.
 
Dada ujumbe mzito kweli kweli, tuombe mungu umfikie lakini kwa jinsi anavyopenda madaraka kama Mwai wa Kibaki sidhani barua yako ataishugulikia

Mkuu, usimlinganishe hata kidogo Mwai Kibaki na Jakaya Kikwete. Kibaki ni bora mara asilimia (%) dhidi ya Kikwete.
Utasema wote walipora ushindi, sawa. Lakini gap alilokuwa nalo Odinga na Kibaki halifanani na la Dr Slaa na Kikwete.

Zaidi hapo, Kibaki ni bomba.
 
Let me just be a spectator in this big match between Janga la Kitaifa against the hungry citizens of the URT.
 
Mh hii ngumu kwa <jk na mawaziri wake...si umeona ishu za umeme zilivyowaweka pabaya Ngereja na Kigoma Mailima....leo hii kiko wapi, wanapeta tu...serikali ya kishkaji
 
mkweree huyu ninaye mfaham!!

thubutu....kwanza huko aliko anatuma sms kama si kupiga simu akiomba nchi zingine zimkaribishe ziara za kiserilika, ili akimbie matatizo hapa hote kwa kubuy time
 
Jamani muogopeni Mungu, asilimia tisini ya matatizo yaliyopo sasa hivi Jk kayakuta, mfano ufisadi wote kwenye madini, umeme na Epa vimefanyika wakati wa Mkapa.Leo hii Jk anatupiwa lawama ambazo kimsingi kazikuta, sidhani hata kama angepewe nchi huyo Slaa wenu kama angeweza fanya chochote zaidi ya kusema kuwa ilani yetu iko hivi.

Acha uongo wewe!!

Thibitisha kuwa Kikwete haja husika kwenye utiaji saini wa Mkataba wa Bulyanhulu uliopelekea watu kufa kwa risasi wengine kufukiwa wakiwa hai na wengine kukosa makazi hadi leo. Yeye alikuwa Waziri wa Nishati na Madini.

Thibitisha kuwa Kikwete hahusiki na kutiwa saini kwa Mkataba wa IPTL. Yeye alikuwa Waziri wa Nishati na Madini.

Thibitisha kuwa Kikwete hajahusika katika wizi wa fedha zetu zilizokuwapo Benki Kuu katika akaunti ya madeni ya nje (EPA) na kuzitumia kupitia Riz1 na katika kampeni za urahisi ili kupata Urais.

Thibitisha kuwa Kikwete hahusiki na Mkataba wa Richmond then Dowans. Yeye alikuwa Rais.

Eti enh! Hata tatizo la kufirisika serikali Mkapa kamsababishia.
 
Kelele!!!!!!!!!!!!

Jamani muogopeni Mungu, asilimia tisini ya matatizo yaliyopo sasa hivi Jk kayakuta, mfano ufisadi wote kwenye madini, umeme na Epa vimefanyika wakati wa Mkapa.

Leo hii Jk anatupiwa lawama ambazo kimsingi kazikuta, sidhani hata kama angepewe nchi huyo Slaa wenu kama angeweza fanya chochote zaidi ya kusema kuwa ilani yetu iko hivi.
 
99 % ya wantanzia wanapenda afanye hivyo ili tuweze kupata ahueni ya maisha maana maisha bora kwa kila mtanzania ya mekuwa kinyume chake
 
Back
Top Bottom