Msanii
Platinum Member
- Jul 4, 2007
- 22,606
- 29,755
Wakati wa kutoa neno la shukrani, wanafamilia wawili wa Hayati Lowassa ambao ni Richard last born na Fredrick first born walisimama kutoa shukrani zao kwa waliohusika kushikamana na familia kuanzia ugonjwa hadi kukamilisha shughuli za mazishi ya mpendwa wao.
Katika neno la shukrani, waliishukuru serikali kwa kusimama nao muda wote kwenye kumuuguza na hata kumuenzi baba yao kwenye mazishi ya Kitaifa.
Pia waliwashukuru watu binafsi zikiwemo taasisi za kidini, madaktari na hata juhudi binafsi za Rais kuhakikisha Lowassa anapata kila msaada unaohitajika ikiwemo faraja.
Lakini kwenye shukrani zote, hakuna mahala ambapo Kikwete ama mwanafamilia yake kutajwa kuwa karibu na familia nyakati za kumuuguza baba yao kipenzi.
Tulimsikia mhe. Kikwete akizungumza pale Masaki alipokwenda kusaini daftari la maombolezo akisema, urafiki na ukaribu wao ulidumu hata baada ya ajali ya kisiasa ya Lowassa pale Bungeni.
Tunajifunza nini kwenye huu msiba hususan kauli za walioenda kuomboleza?