Baba Kikwete Jiuzulu Kulinusuru Tanzania!

Shkamoo Baba,
-Natumai mu wazima nyote hapo magogoni, Mimi ni mzima wa afya pamoja na wanangu na namshukuru Mwenyezi Mungu kwa yote hasa uhai nikiwa huku mitaa ya changanyikeni. Kama mzazi na Rais wangu, kwa miaka zaidi ya tano tangu uingie madarakani, nimekuwa uraiani nikiangalia hali halisi ya nchi yetu, na napenda niwe mkweli kwa kukuletea taarifa ya ukweli ambayo wengi wanaokuzunguka wanakuficha. Ukweli ni Kwamba, hali ya watanzania ni mbaya.

Umasikini umelilemea taifa. Vilio na majonzi kila kona; Ufisadi katika kila nyanja, Rushwa iliyokithiri, Uonevu wa polisi na kutokuwepo haki mahakamani kwa walalahoi. Hakuna haki kwa masikini. Wenye madaraka wamewageuza wananchi kama watumishi wao. Jana nimepita pale hospitali yetu kuu ya muhimbili na ninasikitika kukutaarifu kwamba, hali ni mbaya, watu wanakufa. Jariku uende ujionee mwenyewe hali inavyotisha kutokana na mgomo wa madaktari. Kadhalika nimekuwa nikizunguka maofisini ambako nimekutana na viongozi wengi wa serikali na kusema kweli wameichoshwa na uongozi wako

-Baba, kumbuka kwenye kampeni yetu, tuliwaahidi watanzania maisha bora kwa kila mtanzania, kwa bahati mbaya hii ahadi imegeuka kuwa kinyume. Maisha magumu kwa kila mtanzania. Ninapotembea mitaani wale wote niliowapa Kanga na kofia nikiwaona najificha kwani ahadi nilizowapa nikinunua kura zao nimeshindwa kuzitimiza. Baba, siwezi kuendelea kujificha kutokana na aibu.Sehemu nyingine nazomewa. Hata marafiki zangu ambao ndiyo wengi waliokupigia kura hawataki kuniona. Hebu fikiria mama lishe siku moja alimmwagia shemeji yangu chai usoni aliposema kwamba " hii nchi bila CCM haitakuw ana muelekeo? Hii inaonyesha ni kiasi gani tumewachosha !


- Fanya ustaarabu ujiuzulu kuilinda Tanzania. Tunakoelekea ni kubaya, kwa heshima yako na hatima ya taifa, ni vyema zaidi uachie madaraka kuliko yakukute mabaya tusiyokutakia. Tafakari ugumu wa maisha unaomkabili raia wa kawaida. Nchi imelemewa na matatizo, Migomo ya wafanyakazi, vurugu za kisiasa ndani ya serikali na chama chako ni ishara tosha kwamba nchi HAIWATAWALIKI. Nje ya nchi tunazidi kujidhalilisha hasa ukizingatia matusi tunayomiminiwa tukiitwa MAZEZETA ombaomba. Kuachia madaraka siyo kushindwa bali ni kuonyesha ujasiri na uzalendo wa hali ya juu kwani utakuwa umeweka maslahi ya nchi mbele ya maslahi yako binafsi. Baba naomba uikomboe Tanzania kwa kujiuzulu. Asnate kunisikiliza

Bintiyo


Unafikiri ukimwamkia ndo atakusikiliza, we jua tu sikio lakufa halisikii dawa siku zote
 
Kwa nini Watanzania wote wakulalamikie wewe ! na hata ndani ya chama chako, ilo unabudi ujiulize.
 
Jamani muogopeni Mungu, asilimia tisini ya matatizo yaliyopo sasa hivi Jk kayakuta, mfano ufisadi wote kwenye madini, umeme na Epa vimefanyika wakati wa Mkapa.Leo hii Jk anatupiwa lawama ambazo kimsingi kazikuta, sidhani hata kama angepewe nchi huyo Slaa wenu kama angeweza fanya chochote zaidi ya kusema kuwa ilani yetu iko hivi.

Hata kama matatizo kayakuta mahakama zipo kwaajili ya kazi gani? Au nikwaajili ya wezi wa mitaani na siyo mafisadi? Yafaa ukiwa unajitetea au kumtetea ufikiri kwa kina
 
Hivi kile kikosi mia sitini na ngapi sijui kilichompa siku 100 bado hazijaisha?
 
Hivi kile kikosi mia sitini na ngapi sijui kilichompa siku 100 bado hazijaisha?

Walikuwa ni wanaharakati wakimtishia nyau, pia siku 100 hazijafika ngoja tusubiri. Lakini mkuu wewe hukuwemo kweli?
 
Jamani muogopeni Mungu, asilimia tisini ya matatizo yaliyopo sasa hivi Jk kayakuta, mfano ufisadi wote kwenye madini, umeme na Epa vimefanyika wakati wa Mkapa.Leo hii Jk anatupiwa lawama ambazo kimsingi kazikuta, sidhani hata kama angepewe nchi huyo Slaa wenu kama angeweza fanya chochote zaidi ya kusema kuwa ilani yetu iko hivi.

Matatizo ya Watz ni pamoja na wewe
 
Jamani muogopeni Mungu, asilimia tisini ya matatizo yaliyopo sasa hivi Jk kayakuta, mfano ufisadi wote kwenye madini, umeme na Epa vimefanyika wakati wa Mkapa.Leo hii Jk anatupiwa lawama ambazo kimsingi kazikuta, sidhani hata kama angepewe nchi huyo Slaa wenu kama angeweza fanya chochote zaidi ya kusema kuwa ilani yetu iko hivi.

Kweli kuna watu wengine wameridhika.Hivi kama matatizo umeyakuta si ndio kazi uliyoomba ya kuyaondoa?Hata angekuwa Slaa yuko Magogoni kama hali ingekuwa hivi angeulizwa 'ee Bwana unakotupeleka ndiko ulikoahidi?'
Hata hivyo sikulaumu mitizamo tunatofautiana na hata namna ya ku'react'.
 
Jk usijiuzulu acha waimbe wimbo huu kwa sauti ya juu au chini wasikilize wendawazimu hawa endelea kuongoza nchi tuko nyuma yako. Mungu akupe maisha marefu hadi mwaka 2015
 
Raia Mwema, how much do they pay to write such crap? You're persistently on the key board from morning to mid-night!

Does your prude got a price tag? I bet it must be as cheap as shits you always write.
 
Shkamoo Baba,
-Natumai mu wazima nyote hapo magogoni, Mimi ni mzima wa afya pamoja na wanangu na namshukuru Mwenyezi Mungu kwa yote hasa uhai nikiwa huku mitaa ya changanyikeni. Kama mzazi na Rais wangu, kwa miaka zaidi ya tano tangu uingie madarakani, nimekuwa uraiani nikiangalia hali halisi ya nchi yetu, na napenda niwe mkweli kwa kukuletea taarifa ya ukweli ambayo wengi wanaokuzunguka wanakuficha.
Ukweli ni Kwamba, hali ya watanzania ni mbaya.(wewe ndo unasema ukweli?)

Umasikini umelilemea taifa. Vilio na majonzi kila kona; Ufisadi katika kila nyanja, Rushwa iliyokithiri, Uonevu wa polisi na kutokuwepo haki mahakamani kwa walalahoi.(kushinda kipindi cha nyerere na mkapa mbona husemi) Hakuna haki kwa masikini. Wenye madaraka wamewageuza wananchi kama watumishi wao. Jana nimepita pale hospitali yetu kuu ya muhimbili na ninasikitika kukutaarifu kwamba, hali ni mbaya, watu wanakufa. Jariku uende ujionee mwenyewe hali inavyotisha kutokana na mgomo wa madaktari.(hata kipindi cha mkapa waligoma) Kadhalika nimekuwa nikizunguka maofisini ambako nimekutana na viongozi wengi wa serikali na kusema kweli wameichoshwa na uongozi wako(mzunguko wa kujiuza,kuzurura au umbeya)

-Baba, kumbuka kwenye kampeni yetu,(wewe ni cdm tena wa kule kaskazini) tuliwaahidi watanzania maisha bora kwa kila mtanzania, kwa bahati mbaya hii ahadi imegeuka kuwa kinyume. Maisha magumu kwa kila mtanzania. Ninapotembea mitaani wale wote niliowapa Kanga na kofia nikiwaona najificha kwani ahadi nilizowapa nikinunua kura zao nimeshindwa kuzitimiza. Baba, siwezi kuendelea kujificha kutokana na aibu.Sehemu nyingine nazomewa. Hata marafiki zangu ambao ndiyo wengi waliokupigia kura hawataki kuniona. Hebu fikiria mama lishe siku moja alimmwagia shemeji yangu chai usoni aliposema kwamba " hii nchi bila CCM haitakuw ana muelekeo?(kwa uongo haujambo peleka visa kama hivi kwa shigongo,utapata ulaji acha kubwabwaja)l Hii inaonyesha ni kiasi gani tumewachosha !


- Fanya ustaarabu ujiuzulu kuilinda Tanzania. Tunakoelekea ni kubaya, kwa heshima yako na hatima ya taifa, ni vyema zaidi uachie madaraka kuliko yakukute mabaya tusiyokutakia. Tafakari ugumu wa maisha unaomkabili raia wa kawaida. Nchi imelemewa na matatizo, Migomo ya wafanyakazi, vurugu za kisiasa ndani ya serikali na chama chako ni ishara tosha kwamba nchi HAIWATAWALIKI.(maneno ya slaa nawe umekopi nchi haitawaliki ungepata muda wa kutunga na kupost upuuzi kama huu)Nje ya nchi tunazidi kujidhalilisha hasa ukizingatia matusi tunayomiminiwa tukiitwa MAZEZETA ombaomba. Kuachia madaraka siyo kushindwa bali ni kuonyesha ujasiri na uzalendo wa hali ya juu kwani utakuwa umeweka maslahi ya nchi mbele ya maslahi yako binafsi. Baba naomba uikomboe Tanzania kwa kujiuzulu. Asnate kunisikiliza

Bintiyo (hana binti mjinga kama wewe)


chuki itawaua,bado mna hasira ya kushindwa uchaguzi,pamoja na kampeni za kidini
 
Yaani wewe ni mtu gani unayeshawishi watu watoke kwenye utawala wa Demokrasia waingie kwenye mapinduzi au udikteta? kuwa na subira... 2015 siyo mbali utapiga kura yako na kumweka unayemtaka na matatizo yako yote unayolalamikia yatakwisha.
 
choooooooooooooooonde chooonde! ulevi noooooooooooooooooooomaaaaaaaaaa!

Rais wa migomo umeniacha hoi. Kumbe hizi zitakuwa ni pombe si akili ya kawaida ya jichoD? Hata mimi nimeona tena si pombe ya kawaida itakuwa ni konyagi pori hii.
 
Hata kama matatizo kayakuta mahakama zipo kwaajili ya kazi gani? Au nikwaajili ya wezi wa mitaani na siyo mafisadi? Yafaa ukiwa unajitetea au kumtetea ufikiri kwa kina
Huyu jamaa Makupa amejipanga kubisha bila kutafakari hebu fikiria anasema matatizo ameyakuta inamaana yalikuwa yanajulikana na yeye Janga la Kitaifa aligombea urais ili aweze kuendeleza nchi ikiwa ni pamoja na kutatua matatizo hayo sasa kama alitaka atatue matatizo atakayo yasababisha yeye basi hatufai.JK anakila sababu yakulaumiwa kwa kushindwa kutimiza wajibu wa rais wa Tanzania, ana jeshi,uwt,takukuru,dpp, nk lakini havitumii kutatua matatizo yaliyopo zaidi ya kuflyNinaomba tupeleke bungeni muswada wa NO FLY ZONE kwa JK ili asitoke nchini atatue matatizo.
 
Unataka JK ajihuzuru wakati wewe ni mtoto wa mtu aliyefilisi moja ya mashirika ya umma inchini kwa kukwiba pesa nyingi, na kakusomesha shule nzuri, kazi nzuri hata nyanya tu unanunua Mlimani City hayo huyaoni ila unaona ya JK tu? Acha zako bana!
 
Back
Top Bottom