Viongozi, kuweni wazalendo na hakikisheni nchi inajengwa vizuri

Pantosha

JF-Expert Member
Sep 22, 2022
348
462
Nchi hujengwa na Wananchi wenyewe. Hali ni tofauti kwa bara langu la Afrika ya watu weusi.

Nimezunguka nchi yangu na kujionea kwa macho yangu maisha ya watanzania wengi. Kusema ukweli, kazi ya kuijenga nchi bado tunayo.

Barabara mbovu
Nyumba za makazi mbovu
Vumbi kila kona
Nzi na mbu
Uchafu
Miundombinu ya maji taka

Hali ni mbaya zaidi katika jiji la Dar es salaam.

Wito wangu kwa viongozi wote: “Kuweni wazalendo na hakikisheni inajengwa vizuri”.
 
Wewe unasema tujenge Nchi wakati viongozi wanadai wanaifungua Nchi utadhani Nchi ilikuwa LOCK UP!!
 
Leo nilikuwa na muendelezo wa kufuatilia jamii ya kiAfrica (watu weusi)..nikawa nashangaa kwanini Haiti ilipata uhuru 1814 ikaitawala hadi jirani yake Dominica Republic.

Ila kwasasa maendeleo ya jirani ya Haiti ambao ni Dominica Republic ni makubwa sana kuliko Haiti. Wananchi wamekuwa wazamiaji kwenda kutafuta maisha kwa nchi jirani.

Baada ya wananchi wa Haiti kuzamia Dominica, mwaka 2010 walirudishwa nyumbani Haiti zaidi ya wazamiaji 160,000 ilionekana hakuna faidi wanaongeza zaidi ya kutaka kusababisha fujo na kuongeza umaskini tu.

Jamii ya watu weusi tunahitaji mjadala mkubwa sana kuhusiana na uwezo wetu wa kujitambua, kama ni chakula au Mila zetu ndo chanzo cha udumavu wa fikra itambulike ili tuondokane na mnyororo huu wa kutojitambua.

Jana nilikuwa naangalia makala kuhusiana na kiwanda cha kutengeneza magari kule Casablanca Morocco nikawa najiuliza ata mradi wa mwendokasi inatushinda kukiendesha kuwa hatuna uwezo au?

Je, tafiti inaonesha shida ni zipi?

Nikiangalia makazi ya watu weusi kule TEXAS Marekani bado inanipa picha kuwa bisingizio dhidi ya ukoloni siyo sahihi tena.
 
Nchi hujengwa na Wananchi wenyewe. Hali ni tofauti kwa bara langu la Afrika ya watu weusi.

Nimezunguka nchi yangu na kujionea kwa macho yangu maisha ya watanzania wengi. Kusema ukweli, kazi ya kuijenga nchi bado tunayo.

Barabara mbovu
Nyumba za makazi mbovu
Vumbi kila kona
Nzi na mbu
Uchafu
Miundombinu ya maji taka

Hali ni mbaya zaidi katika jiji la Dar es salaam.

Wito wangu kwa viongozi wote: “Kuweni wazalendo na hakikisheni inajengwa vizuri”.
Viongozi wapo busy na mapambio na mapambio kwa bi mkubwa.
 
Nchi hujengwa na Wananchi wenyewe. Hali ni tofauti kwa bara langu la Afrika ya watu weusi.

Nimezunguka nchi yangu na kujionea kwa macho yangu maisha ya watanzania wengi. Kusema ukweli, kazi ya kuijenga nchi bado tunayo.

Barabara mbovu
Nyumba za makazi mbovu
Vumbi kila kona
Nzi na mbu
Uchafu
Miundombinu ya maji taka

Hali ni mbaya zaidi katika jiji la Dar es salaam.

Wito wangu kwa viongozi wote: “Kuweni wazalendo na hakikisheni inajengwa vizuri”.
Watakwambia Fanya kazi hakuna mwaka hauna maisha magumu.....sasa unajiuliza mbona nafanya kazi sana hadi Jasho la Chumvi?

Wanataka nitoke damu ndio wajue nafanya kazi?
 
Afrika tunazingua hadi wazungu wanatamani watutawale upya. Tunaonekana tupo hopeless

Back
Top Bottom