Baba Kikwete Jiuzulu Kulinusuru Tanzania!

Shkamoo Baba,
-Natumai mu wazima nyote hapo magogoni, Mimi ni mzima wa afya pamoja na wanangu na namshukuru Mwenyezi Mungu kwa yote hasa uhai nikiwa huku mitaa ya changanyikeni. Kama mzazi na Rais wangu, kwa miaka zaidi ya tano tangu uingie madarakani, nimekuwa uraiani nikiangalia hali halisi ya nchi yetu, na napenda niwe mkweli kwa kukuletea taarifa ya ukweli ambayo wengi wanaokuzunguka wanakuficha. Ukweli ni Kwamba, hali ya watanzania ni mbaya.

Umasikini umelilemea taifa. Vilio na majonzi kila kona; Ufisadi katika kila nyanja, Rushwa iliyokithiri, Uonevu wa polisi na kutokuwepo haki mahakamani kwa walalahoi. Hakuna haki kwa masikini. Wenye madaraka wamewageuza wananchi kama watumishi wao. Jana nimepita pale hospitali yetu kuu ya muhimbili na ninasikitika kukutaarifu kwamba, hali ni mbaya, watu wanakufa. Jariku uende ujionee mwenyewe hali inavyotisha kutokana na mgomo wa madaktari. Kadhalika nimekuwa nikizunguka maofisini ambako nimekutana na viongozi wengi wa serikali na kusema kweli wameichoshwa na uongozi wako

-Baba, kumbuka kwenye kampeni yetu, tuliwaahidi watanzania maisha bora kwa kila mtanzania, kwa bahati mbaya hii ahadi imegeuka kuwa kinyume. Maisha magumu kwa kila mtanzania. Ninapotembea mitaani wale wote niliowapa Kanga na kofia nikiwaona najificha kwani ahadi nilizowapa nikinunua kura zao nimeshindwa kuzitimiza. Baba, siwezi kuendelea kujificha kutokana na aibu.Sehemu nyingine nazomewa. Hata marafiki zangu ambao ndiyo wengi waliokupigia kura hawataki kuniona. Hebu fikiria mama lishe siku moja alimmwagia shemeji yangu chai usoni aliposema kwamba " hii nchi bila CCM haitakuw ana muelekeo? Hii inaonyesha ni kiasi gani tumewachosha !


- Fanya ustaarabu ujiuzulu kuilinda Tanzania. Tunakoelekea ni kubaya, kwa heshima yako na hatima ya taifa, ni vyema zaidi uachie madaraka kuliko yakukute mabaya tusiyokutakia. Tafakari ugumu wa maisha unaomkabili raia wa kawaida. Nchi imelemewa na matatizo, Migomo ya wafanyakazi, vurugu za kisiasa ndani ya serikali na chama chako ni ishara tosha kwamba nchi HAIWATAWALIKI. Nje ya nchi tunazidi kujidhalilisha hasa ukizingatia matusi tunayomiminiwa tukiitwa MAZEZETA ombaomba. Kuachia madaraka siyo kushindwa bali ni kuonyesha ujasiri na uzalendo wa hali ya juu kwani utakuwa umeweka maslahi ya nchi mbele ya maslahi yako binafsi. Baba naomba uikomboe Tanzania kwa kujiuzulu. Asnate kunisikiliza

Bintiyo


Ushauri mzuri ila bado sijaona mbadala, kwa wote wanaotajwa tajwa ni afadhali sana ya ****** kuliko wao.
 
Nasikitika sana kuona kuwa nchi yetu sasa imekuwa ya 'kila mtu na lwake'. Huyu jamaa ameingia madarakani kwa ujanja na hila nyingi ili aweze kujinufaisha yeye na familia yake. Laiti mngejua utajiri mkubwa aliojilimbilikizia yeye na familia yake bila shaka mngelia machozi. Huyu hana uzalendo na nchi hii na wala hakulilia urais ili kuwatumikia watanzania, bali kukidhi matakwa yake binafsi. Angalia jinsi watanzania walio wengi wanavyotaabika na yeye wala hajali.
 
Back
Top Bottom