ACT Tanzania wamepata wapi pesa za promo star Tv?

1. Ambacho hakina Mbunge hata mmoja,
2. Hakina Ruzuku yoyote,
3. Hakina wafadhili wanaotambulika wanaokifadhili,
4. Chenye wanachama wachache wengi wakiwa ni vijana wa mitaani wasio na mbele wala nyuma kwa maana ya kutokuwa na ajira,
5. Ambacho hakijawahi hata siku moja kuchangisha Wanachama wake pesa kwaajili ya kugharamia vikao katika Hotel za gharama zenye hadhi ya nyota tano sambamba na Mikutano ya ndani na ile ya hadhara,
6. Hakijawahi kuomba mchango kwa wanachi ili kusaidia kuweza kujiendesha,

Je chama hiki kinafadhiliwa na nani au kinatoa wapi fedha za
1. Kuendesha vikao katika hoteli za gharama zenye hadhi ya nyota tatu mpaka tano,
2. Kuendesha mikutano ya ndani na ile ya hadhara,
3. Kugharamia Usafiri na Malazi kwa baadhi ya maofisa na viongozi wa chama,
4. Kulipia Kodi ya pango katika ofisi zake,
5. Kuprint Mabango, T-Shirts, Kofia, Skafu, Vipeperushi, Kadi nk..?¿!¡..

Usisahau hiki ni chama ambacho waasisi na viongozi wake wakuu ni wale waliofukuzwa kutoka katika chama kikuu cha upinzani nchini, chama ambacho Kiongozi wake mkuu ndiye mwenye mamlaka kuliko mwenyekiti!
Kuuliza sio ujinga.

COPY & PASTE

Haitaji kutumia nguvu nyingi kujuwa chama cha ACT Tanzania ni cha mafisadi na majambazi kama alivyokwisha kukiri mwenyekiti wao Limbu.

Nasema hivi maana haiwezekani hata kidogo "eti baada tu ya Zitto kuchukuwa kadi waanze promo kwenye Tv kana kwamba wanapata ruzuku.

Kama sio wezi na matapeli wamepata wapi pesa za matangazo ya kila wakati Star tv?

Mbona kabla ya Zitto hatukuona matangazo hayo?

Tutafakari sura hizi mbili ambazo ACT Tangazo inazo kwa sasa,kabla ya Zitto kujiunga na baada ya kujiunga.

Hadi mtakapozinduka kuwa wanafunzi wa vyuo na shule wamefunga shule hakuna chakula,Ofisi za serikali hakuna hela,walimu hawalipwi stahiki zao ili Act isaidie kuimega na kuiua chadema!
 
Hadi mtakapozinduka kuwa wanafunzi wa vyuo na shule wamefunga shule hakuna chakula,Ofisi za serikali hakuna hela,walimu hawalipwi stahiki zao ili Act isaidie kuimega na kuiua chadema!

Baadhi ya wazee wastaafu hawajalipwa pensheni zao.
 
kuna uzi umetolewa haraka wa zito kumtumia sms mwigulu kuomba aongezewe fungu ...mods wametoa haraka sana hapo ndio nnapopata shaka...ukiwekwa uzi wa kiongozi yeyote wa cdm humu kutuhumiwa kupokea rushwa au chochote mods wanaacha lakini issue yoyote ikimuhu zito wanaitoa haraka ........mods waachieni watu wajadili la sivyo msiweke habari yeyote inayohusu tetesi humu ndani jukwaa mnaliharibu wenyewe

Habari za kuondoa nyuzi, hata za uzushi, inaondoa ukweli wa kaulimbiu ya "We dare go speak openly".

Mtu unapokuwa unachangia kwa kutiririka halafu unakuta uzi hmefunhwa inavunja mogo wa kuendelea kuchangia.

Kuondoa nyuzi ni censorship. Kama tumekomaa tunatakiwa kuweza kupinga uongo kwa ukweli, si kwa kuondoa nyuzi.
 
Naona pesa wanapewa na wanachama wao. Na mwanzo ni lazima kuwepo moyo wa kujitolea kama vile CDM waliyofanya ili mwisho chama kimilikiwe na wenye chama.

Ni mwanachama gani anaweza kutoa mchango wa kugharamia Malipo ya boda boda, vikao katika mahoteli mbali mbali, malezi ya viongozi, usafiri, posho kwa viongozi na nk.. Na ukizingatia hiki ni chama cha wanyonge (yaani masikini)?

Zitto yeye ni mzalendo na katika account yake kuna mil 18 tu.. Sasa pesa za kufanya hii kufuru inatoka wapi? Kumbuka h
 
Mwanachama mwenye uwezo. Jambo usilolijua ni kama usiku wa giza, wenye imani haba tulia. Chama kinaenda.

Haya mnyouliza, ndo CCM wanauliza CDM nani anawafadhili, hii ndo inaitwa hofu. Msihofu, siasa haina mmiliki, mkikuta mwingine anainuka kwa kutumia udhaifu wenu ndo mjue mnakua pia.

Ni mwanachama gani anaweza kutoa mchango wa kugharamia Malipo ya boda boda, vikao katika mahoteli mbali mbali, malezi ya viongozi, usafiri, posho kwa viongozi na nk.. Na ukizingatia hiki ni chama cha wanyonge (yaani masikini)?

Zitto yeye ni mzalendo na katika account yake kuna mil 18 tu.. Sasa pesa za kufanya hii kufuru inatoka wapi? Kumbuka h
 
kuna uzi umetolewa haraka wa zito kumtumia sms mwigulu kuomba aongezewe fungu ...mods wametoa haraka sana hapo ndio nnapopata shaka...ukiwekwa uzi wa kiongozi yeyote wa cdm humu kutuhumiwa kupokea rushwa au chochote mods wanaacha lakini issue yoyote ikimuhu zito wanaitoa haraka ........mods waachieni watu wajadili la sivyo msiweke habari yeyote inayohusu tetesi humu ndani jukwaa mnaliharibu wenyewe

Habari za kuondoa nyuzi, hata za uzushi, inaondoa ukweli wa kaulimbiu ya "We dare go speak openly".

Mtu unapokuwa unachangia kwa kutiririka halafu unakuta uzi hmefunhwa inavunja mogo wa kuendelea kuchangia.

Kuondoa nyuzi ni censorship. Kama tumekomaa tunatakiwa kuweza kupinga uongo kwa ukweli, si kwa kuondoa nyuzi.

Kuna ukweli ndani yake.. Hata tumezoea Dr. Slaa kuitwa mzinzi sijawahi ona Moderator wanaondoa neno Mzinzi, Rais Kilaza, sijawahi ona wanaondoa neno kilaza, Mbowe kuitwa kengeza sijawahi ona modarater anaondoa neno kengeza na msururu ni mrefu... Je kigezo gani nimetumika kuondoa neno M.sa.liti?

Pili ninapenda kujua ni kwanini M.awio na Mwa.ha.lisi yamefutwa? Kumbuka wateja wakuu wa huu mtandao ni sie wanachama na ugomvi wa maboss wa JF, hauna nafasi katika jukwaa hili.. Ni haki yetu kujua kwanini haya maneno ni marufuku kutumika humu ndani je ni matusi???Na ni kwanini mtu mmoja atuamulie sie wanachama ni nini cha kuandika na nini cha kuacha hali sio matusi...
Invisible , Paw
 
Mwanachama mwenye uwezo. Jambo usilolijua ni kama usiku wa giza, wenye imani haba tulia. Chama kinaenda.

Haya mnyouliza ndo CCM wanauliza ka CDM nani anawafadhili, hii ndo inaitwa hofu. Msihofu, siasa haina mmiliki, mkikuta mwingine anainuka kwa kutumia udhaifu wnundo mjue mnakuwa pia.

?????????????Nani mfadhili wa ACT? ndo swali hilo..
 
Udanganyifu ni dhambi kubwa sana na haivumiliki kwa Mungu hata kwa binadamu yoyote,Hivi ni kwanini ACT wameamua kuwadanganya watanzania kwa kiwango kikubwa namna hii?
Walianzia Songea Iringa na sasa Morogoro kesho tunajuwa watakuwa Pwani.Wapi pesa hizi ACT wamepata?
Chadema walianza harakati za siasa miaka 20 iliyopita lakini nguvu ya kufanya mikutano yao mikubwa na mfulilizo mkoa kwa mkoa waliweza miaka 7 mpaka 10 baada ya kuanzishwa kwake,Hivyo hivyo kwa CUF mbona UDP APPT UPDP Na vyama vingine hatuoni nguvu yao?Japo tunajuwa wapo kwenye siasa kwa miaka mingi tu....
Narudi kuuliza kama ambavyo wapenda demokrasia wenzangu walivyowahi kuuliza bila majibu yenye afya.
1.Ni nini vyanzo vya mapato ya ACT iliyoanza mwezi huu?
2.Wapi ACT mnapata pesa za kuzunguka nchi nzima? Mwl.Kaijage na Zitto Majibu haya yakijibiwa kwa ufasaha nipo tayari kuamini act sio tawi la Ccm na nitaunga mkono harakati zenu kwa moyo mkunjufu kama mpenda mabadiliko wa nchi hii.
 
Last edited by a moderator:
Ulizia Chadema pesa walizopewa na Sabodo kujenga visima na makao makuu zimeishia wapi?
 
Back
Top Bottom