Haki, Haki, Haki! Serikali, Bunge na Mahakama hazina uwezo wala mamlaka ya kupora haki ya kuchagua na kuchaguliwa. Je, jicho ona litaliona hili?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,499
113,610
Wanabodi,

Kama kawa, kila nipatapo fursa, huja na makala zangu elimishi kuhusu Tanzania yetu zinazokwenda kwa jina la "Kwa Maslahi ya Taifa", kuzungumzia jambo lolote la kisiasa, kiuchumi na kijamii, makala ya leo ni muendelezo wa mfululizo wa makala za Ijue Katiba ya JMT-4, ikijikita kwenye Haki za Kikatiba za Mtanzania. Hizi ni haki mbalimbali zilizotolewa na katiba ya Tanzania kwa raia wa Tanzania.

Mada ya leo ni kuhusu Haki, Haki, Haki! Serikali, Bunge, Mahakama, hazina uwezo wala mamlaka ya kupora haki yeyote iliyotolewa na katiba, kwasababu katiba ni supreme na mihimili hiyo yote mitatu iko chini ya katiba!.

Mihimili miwili, Serikali na Bunge zimepoka haki ya Mtanzania kuchagua na kuchaguliwa zilizotolewa na Katiba ya JMT ya mwaka 1977, Serikali yetu na Bunge letu zilipata wapi uwezo na mamlaka ya kuzipora haki hizi?, ambapo mpaka hapa ninapoandika hapa, haki hizi bado zimeporwa!. Mtanzania hana haki ya kuchagua kiongozi anayemtaka, kwasababu haki ya kila Mtanzania kugombea imepokwa na kakikundi kadogo ka watu wanaoitwa chama cha siasa. Chama cha siasa ndio kimepewa mamlaka ya kuamua nani agombee na sio wagombea au wananchi, matokeo yake wananchi wanalazimishwa kuchagua viongozi walioletewa na vyama vya siasa kitu ambacho sio sahihi kabisa!, sio haki na ni dhambi!, usikute ndio sababu karma kila siku inawatafuna viongozi wetu!.

Rais Samia Suluhu, ni fursa, amekuja kwa kudra za Mwenyezi Mungu kuliishi jina lake la Suluhu kwa kuleta suluhu ya kweli ya mtanziko wa kisiasa unaolikabili taifa letu, ameonyesha kwa kauli na matendo anataka maridhiano ya kweli ndio maana amekubali kubadili sheria ni fursa ya kuzirejesha haki za msingi za Watanzania zilizoporwa, jee Rais Samia ataichangamkia hii fursa by practicing what she preaching? Au kwa vile aliyezipora haki hizo sio yeye, yeye kaingia kakutwa zimeishaporwa na sasa anafanya marekebisho cosmetics tuu ya sheria, lakini zile haki porwa za katiba, katiba, haziguswi?, hivyo kumaanisha she was just paying lip services by not practicing what she preaches?.

Huu ni muendelezo wa kumlilia mtu ili kumuonyesha jicho lake lione dhulma waliotendewa Watanzania, ambayo sasa inataka kujirudia kwenye hii sheria mpya ya uchaguzi. Je, tuendelee kupiga tuu kelele mwisho wa. Siku, jicho ona litaona, na sikio sikia litasikia, au huku ni kujifurahisha tuu na kujifariji tuu kwa kelele za mlango, lakini Jicho Ona limeisha ingia upofu na sikio sikia limeisha ingia uziwi?, hivyo hakuna kitachoonekana wala kitakacho sikika?.

Naomba kuanza bandiko hili kwa promo ya kipindi changu yenye nukuu ya Rais Samia akizungumzia Katiba sheria na Haki.

Hivyo hiki ninachokifanya hapa kwenye bandiko hili ndio huo utoaji wa elimu ya katiba sheria na utetezi wa haki za msingi za hawa binadamu wa Tanzania ambao haki zao zimepokwa na kuporwa na awamu zilizotangulia, ambapo wapokaji na waporaji karma imeisha washughulikia, hapa naandika ili kumsaidia kumfungua Mama jicho ona lione, na sikio sikia lisikie!

Haki ziko nyingi, lakini mimi nitajikita kwenye haki 4 Kuu za Mtanzania.
  1. Haki kuu ya kwanza ni haki ya uraia. Mtu yoyote akizaliwa ndani ya ardhi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mtu huyu anakuwa ni raia wa Mtanzania kwa kuzaliwa, haki hii ni haki ya kwanza ya msingi ambayo ni haki ya kuwa Mtanzania. Haki hii haiwezi kuondolewa na mamlaka yoyote, ila unaweza kuipoteza endapo utaukana Uraia wako. Hivyo ile sheria yetu ya kuwa mtu akichukua uraia wa nchi nyingine yoyote, anaupoteza Utanzania wake, ni sheria batili kinyume cha katiba, ila ubatili huu, haujabatilishwa kwasababu hakuna aliyefungua shauri mahakamani kuipinga.
  2. Haki kuu ya pili ni haki ya kuchagua iliyotolewa na ibara ya 5 ya katiba ya JMT. Haki hii ni kila raia wa Tanzania anapofikisha umri wa miaka 18, ana haki ya kuchagua kiongozi wake. Haki hii inatekelezwa kwa kila mtu kujiandikisha kupiga kura. Haki hii haiwezi kuondolewa na mamlaka yoyote. Kwa Tanzania, haki hii imefinyangwa finyangwa kwa baadhi ya watu kunyamaza haki hii, kwa kufungwa magezani, wagonjwa mahospitalini, na Watanzania walioko nje ya nchi. Kufuatia maendeleo makubwa ya Teknolojia, na andikishaji unaotumia BVR hivyo kwa kutumia biometric data, kitambulisho cha taifa au passport ambavyo vyote vina biometric data, vinaweza kutumika kuwawezesha Watanzania wote popote walipo kumchagua Rais wa Tanzania na rais wa Zanzibar popote pale walipo.
  3. Haki kuu ya tatu ni haki kuchaguliwa kupitia ibara ya 21 ya katiba ya JMT kwa mtu mwenye miaka 21, yuko huru kugombea nafasi yoyote ya uongozi kuanzia serikali za mitaa hadi serikali kuu. Haki hii ni haki ya msingi na haiwezi kuondolewa na mamlaka yoyote. Kwa Tanzania, haki hii ya kila Mtanzania ana haki ya kugombea nafasi yoyote ya uongozi na kuchaguliwa imefutwa kwa kuchomekewa shurti la kudhaminiwa na chama cha siasa. Shurti hili ni batili!.
  4. Haki ya Watanzania kuanzisha vyama na kujiunga na vyama vya siasa sio haki ya msingi, uhuru wa mtu kujiunga na chama cha siasa ni hiyari, hilarious hiyo ya kujiunga na vyama vya siasa na kuwa mwanachama wa chama cha siasa, hakiwezi kumuondolea Mtanzania haki yake ya msingi ya kuchagua na kuchaguliwa!.
  5. Serikali ya Tanzania, haiwezi kutunga muswada batili unaopora haki ya msingi ya mtu kuchagua na kuchaguliwa, na kumlazimisha lazima ajiunge na chama cha siasa. Shurti hili ni kinyume cha Ibara ya 11 ya katiba ya Tanzania. Serikali yetu imepeleka muswada batili wa kutunga sheria batili ya uchaguzi, yenye kipengele hicho kinyume cha katiba!.
  6. Bunge la Tanzania, likaupitisha ubatili huo wa serikali, kuwanyima haki Watanzania, na kutunga sheria batili ya uchaguzi yenye shurti la kudhaminiwa na chama cha siasa ndipo mtu ugombee uongozi. Bunge halina mamlaka hayo ya kuondoa haki ya kikatiba ya kila Mtanzania kuchagua na kuchaguliwa!.
  7. Mahakama Kuu ya Tanzania, kupitia kesi ya Mchungaji Mtikila, iliibatilisha sheria hiyo kuwa vipengele hivyo ni batili, Serikali ikakata rufaa ikashindwa.
  8. Serikali yetu ikafanya jambo la ajabu sana, ikauchukua ubatili huo na kuuchomekea ndani ya Katiba yetu kiubatili, kwa kufanya mabadiliko ya katiba kwa hati ya dharura, hivyo shurti la mgombea kudhaminiwa na chama cha siasa liko kwenye ibara 39 na 68 ya katiba ya JMT ya mwaka 1977.
  9. Mchungaji Mtikila, hakukubali katiba yetu inajisiwe, akafungua shauri jingine kupinga mabadiliko hayo ya katiba yetu ya kiubatili kuchomeka vipengele batili ndani katiba yetu. Mahakama Kuu ikampa ushindi na kutangaza mabadiliko hayo ya katiba ni batili, hivyo hukumu ya mahakama kuu bado inasimama!.
  10. Serikali yetu ikaomba mapitio, ndipo mahakama ya Rufaa ikakaa full bench chini ya majaji 7, na kupitisha uamuzi wa ajabu kabisa kuwahi kufanywa na Mahakama nchini, pale ilipotamka "The Court is Not The Custodian of The Will of The People"!, na kulirudisha suala hilo Bungeni!, Bunge mpaka leo, mpaka kesho, halijarekebisha ubatili huu hivyo huku ni kuwatendea dhambi kubwa Watanzania!.
  11. Kama serikali haina mamlaka ya kufuta haki iliyotolewa na katiba, Bunge halina mamlaka ya kutunga sheria batili inayokwenda kinyume cha katiba kwa kufuta haki hiyo, Mahakama ya Rufaa pia haikutimiza wajibu wake, kusema the court is not the custodian of the will of the people, wakati serikali imekiuka katiba kutunga muswada batili, Bunge likakiuka katiba kutunga sheria batili, na Mahakama Kuu kuutangaza tuu ubatili bila kuubatilisha ni kutotimiza wajibu wake kikamilifu, na kitendo cha Mahakama ya Rufaa kuligwaya Bunge katika ukiukwaji wa katiba, ni kutotimiza wajibu wake kikamilifu.
  12. Hii senema au kwa lugha watoto wa mjini, movie ya serikali yetu, kututungia sheria batili inayokwenda kinyume cha katiba ya JMT halafu Bunge letu Tukufu likatutungia sheria batili inayokwenda kinyume cha katiba ya JMT, inataka kujirudia kwenye hii sheria mpya ya uchaguzi, itakayosomwa Bungeni kwa mara ya pili, ni muendelezo wa ubatili ule ule ambao Mahakama Kuu iliisha ubatilisha, sasa sijui tunyamaze kimya na kulisubiria Bunge letu Tukufu litutungie sheria batili nyingine tena ndipo twende Mahakamani kuupinga ubatili, au tuendelee kupiga kelele labda lile jicho ona pia litauona ubatili huu, na sikio sikia litausikia ubatili huu?
Hitimisho
Mimi ni muumini wa kitu kinachoitwa karma, kinachotumia kanuni za Newton's laws of motion, kwa everything happens for a reason, no one knows kwanini ni Nyerere, Mkapa na Magufuli, na sio Mwinyi, Kikwete na sasa Samia, haki ninayoizungumza hapa ni haki kuu ya msingi, kuidhulumu ni dhambi kubwa! Kwa vile no-one knows kwanini wale, mimi muumini wa karma, ninawaambia it's karma! Kama Mama anaweza kuwarejeshea haki hii Watanzania, atabarikiwa sana, ila pia ili kumuepushia na bad karma, Mama asiruhusu kabisa dhulma hii kwa Watanzania ijirudie katika awamu yake.

Kwa vile matatizo makubwa ya siasa zetu yako kwenye katiba, tulianza mfumo wa vyama vingi kwa katiba ya chama kimoja, ili kuwatendea haki Watanzania, tufanye kwanza mabadiliko madogo ya katiba, minimum reforms pia kuondoa dhulma hii, kisha ndipo tufanye mabadiliko ya Sheria ziwe ni sheria za haki.

Toka Rais Samia ameingia madarakani ile March 21, 2021, mimi tuu mwenyewe, nimelisemea jambo hili la hitaji la mabadiliko ya katiba, sheria na haki kwa kupandisha mabandiko zaidi ya 50!
  1. Ukosekanaji wa Haki kwenye Mhimili wa Mahakama, kunaweza kuwa kunachangiwa na Majaji/Mahakimu wenye uwezo mdogo kubaini haki?
  2. Rais Samia, sio malaika ni binadamu anaweza kukosea. Tusimlaumu, kumshutumu na kumponda kwa makosa ya kukoseshwa. Tumvumilie tumpe muda
  3. Asante Rais Samia kwa kuwasisitiza watendaji wa vyombo vya haki kuwa haki sio hisani, bali ni stahiki. Watende haki, tubadili Katiba kurudisha haki
  4. Psychoanalysis Trends za Viongozi Wetu, Humbleness ya Rais Samia ni Bonafide Genuine, ni asili yake, ni nature yake, ndivyo alivyo, Ila...
  5. Mwaka 2021 ulikuwa ni Mwaka wa Majanga kwa Tanzania. Mwaka 2022 uwe Mwaka wa Mabadiliko, Watanzania tubadilike! Happy New Year!
  6. Asante sana Rais Samia kwa kuliponya Taifa. Umeonesha kwa kauli na matendo; tunajenga nyumba moja, hakuna sababu ya kugombea fito!
  7. Haki Huinua Taifa! Rais Samia kwa Kauli na Matendo ameonesha ni mtu wa Haki. Akitekeleza hili kama alivyosema, atabarikiwa, Tanzania itabarikiwa
  8. Samia ni mpango wa Mungu kwa Tanzania: Kwa hili atabarikiwa, Taifa litabarikiwa. Asante Mungu kwa Samia, Mungu mbariki Samia, Mungu ibariki Tanzania!
  9. Mgombea Kudhaminiwa na Chama ni Ubatili Uliochomekwa Kiubatili na Bunge Letu Ndani ya Katiba Yetu!. Tuache Ubatili Huu Uendelee Ndani ya Katiba Yetu?
  10. Je Wajua kuna Fupa Fulani la Dhulma kwa Watanzania, Liliwashinda Nyerere, Mwinyi, Mkapa, Kikwete na Magufuli, Jee Mama Samia Ataliweza Fupa Hili?.
  11. Kwa Kauli Hii, Rais Samia atabarikiwa sana kuliko Rais mwingine yeyote! Huu ni wema mkubwa kabisa kuwahi kuwa Rais yeyote ukimuondoa Nyerere
  12. Je, jicho la Rais Samia litauangazia Ubatili huu ndani ya Katiba yetu unaopora Haki ya Msingi, uliochomekewa kibatili ili kuuhalalisha?
  13. Asante Mungu kwa Rais Samia: Ni Msema Kweli na Mtenda Kweli, Ni Msema Haki na Mtenda Haki. Je, Ataruhusu Ubatili Huu Kuendelea Ndani ya Katiba Yetu?
  14. Tum-judge Rais Samia kwa mawazo, maneno, na matendo yake ya sasa akiwa ni Rais wa JMT na siyo kwa alivyokuwa VP!
  15. "Ombeni Mtapewa", "Tafuteni Mtapata", "Bisheni Hodi Mtafunguliwa" Je, Wajua Kuna "Kauli" na "Kauli Umba" Ambazo Huumba? Shuhudia
  16. Kumuenzi Baba wa Taifa: CCM, Serikali, Viongozi na Watanzania kwa Ujumla. Je, tunamuenzi kwa Mawazo, Maneno na kwa Vitendo? Tunamuishi?
  17. Should We Demand More Right to Information Kwenye Teuzi za Key Posts? Ziwe Endorsed na Bunge With Security of Tenure? Mawaziri Wasiwe Wabunge?
  18. Katiba ni Sheria Mama. Sheria Yoyote Kinyume na Katiba ni Batili. Wanasheria Wetu, Waliwezaje Kufanya Madudu Haya Kuchomeka Batili Ndani ya Katiba?
  19. Ijue Katiba ya JMT-1: Katiba ni nini, ya nani, ya kazi gani? Msemo "Katiba ndio kila kitu" Una maana gani? Katiba ina umuhimu gani?
  20. Ajabu Hii ya Haki Iliyotolewa na Ibara Moja ya Katiba, Kuporwa na Ibara Nyingine, Ilifanyika Vipi Huku Tuna Washeria Manguli, Wabobezi na Wabobevu?
  21. Madudu haya ya ajabu ya kisheria yaliweza kufanyika vipi wakati tuna Wanasheria?
  22. Amri Kuu Kuliko Zote ni Upendo! Mpende Mungu, Ipende Nchi, Wapende Viongozi, Mpende Jirani Yako Kama Nafsi Yako!. Jirani yako ni Nani?, Unampenda?
  23. Asante Rais kuruhusu mikutano, tunakuomba uruhusu haki nyingine ambayo imeporwa ya Watanzania wote kuchagua na kuchaguliwa
  24. Anayekuja pasi na hodi, huondoka pasi kuaga. Kuzuiwa bila kifungu, kuruhusu bila Kifungu. Ni hisani ya Rais Samia. Haki kuhisaniwa hadi lini?
  25. Mahali ni pazuri ndugu wanapokaa, wakipata vema na kupendana. Tulikotoka ni kugumu, tunakokwenda ni kurahisi, kuzuri! Heri ya Mwaka Mpya wahusika wote
  26. Watanzania ni maneno maneno na kulialia, Vitendo 0. Katiba ni maneno tu! Je, 2023 tuendeleze maneno matupu na kulialia au tubadilike tufanye kitu?
  27. Miaka 61 ya Uhuru: Japo Tumefanikiwa sana kielimu, shule, vyuo na wasomi (Madaktari na Maprofesa kibao), mbona bado adui ujinga yupo? Tunakwama wapi?
  28. Hongera Sana Rais Samia kwa Miaka Miwili Madarakani. Japo Umefanya Mengi, Makubwa, Mazuri, Lakini Bado! Linalowezekana Leo, Lisingoje
  29. Wanawake Wana Akili Kuliko Wanaume? Hata kwenye Siasa na Uongozi, Wanawake Wameonyesha Uwezo Kuliko Wanaume
  30. Ili kupata Viongozi Bora baadae, Watanzania tujifunze kuwasoma watu kwa asili zao. Mjue Samia alivyo kwa asili yake
  31. Siasa za Kijungu Jiko, Penye Uzia, Penyeza Rupia!. Hakuna Mkate Mgumu Mbele ya Chai!, Hata Uwe Mgumu Vipi, Mbele ya Chai/Rupia, Lazima Utalainika!
  32. Kuelekea Siku ya Wanawake Duniani: Je Wajua Kuna Wanawake Wana Uwezo Mkubwa Kuliko Wanaume ila Wamekuwa Wanabaniwa!. Hata Huyo Kuonyesha Uwezo na ...
  33. Je, kuna kazi za kike na za kiume? Fupa hili lililowashinda wanaume wanne, mwanamke mmoja ataliweza?
  34. Katiba Yetu Ina Matobo: Serikali Ikikosea, Inashitakika. Je, Bunge na Mahakama Zinapowakosea Watanzania Kama Makosa Haya Tunawashitaki Wapi?
  35. Je, Wajua? Mhimili wa Mahakama Usipotenda Haki Unaweza Kushitakiwa? Pongezi Jaji Mkuu wa Kusisitiza Usuluhishi na Sio Kukimbilia Kufungua Kesi
  36. Je, Wajua, kuna 2 Types of Leaders. Born Leaders na Manmade Leaders. Je, Wajua tutamfaidi zaidi Rais Samia 2025-30 kuliko sasa?
  37. Katiba mbovu, sheria mbovu, mikataba mibovu. Leo tumetozwa zaidi ya Tsh. Bilioni 260. Kufanywa kichwa cha Mwendawazimu hadi lini?
  38. Bunge, Serikali na Mahakama, Sio Mungu, Sio Malaika, Zinaweza Kukosea!. Zinapokosea, Zina Wajibu Kurekebisha na Kutenda Haki, Vinginevyo Karma Will Do
  39. Heshima kitu cha bure! Kwanini Rais Samia, japo sio lazima apendwe na wote lakini ni lazima aheshimiwe na wote? Akosolewe kwa staha na asitukanwe!
  40. Jaji Mugasha Apewe Maua Yake Kupinga Uvunjifu wa Katiba Ukomo wa CJ, ila Mbona Hili ni Dogo Tuu, Kubwa ni Katiba Yetu Imenajisiwa! Why Wako Kimya?!.
  41. Kwa la Bandari, Pongezi TLS. Katiba yetu imenajisiwa. Bunge limetunga Sheria batili. Haki za Watanzania zimeporwa. Kwanini TLS wamenyamaza kimya?
  42. https://www.jamiiforums.com/threads/watanzania-ni-watu-wa-ajabu-wanapigiaje-kelele-jambo-dogo-la-bandari-lakini-mambo-muhimu-ya-msingi-kama-katiba-na-uhuru-wao-wapo-kimya.2111266/
  43. Mabadiliko ya Sheria Bila Mabadiliko ya Katiba,Sawa na Kula Bila Kunawa!. Je Watanzania Tuna Haraka Sana na Uchaguzi Hadi Tukimbilie Kula Bila Kunawa?
  44. Pongezi Rais Samia, Serikali, Kukubali Kubadili Sheria ya Uchaguzi, Tume Huru ya Uchaguzi!. Tuanze na Katiba Kwanza Ndipo Sheria Au?.
  45. Prof. Lipumba: Nina Matumaini Makubwa na Rais Samia, Chaguzi Zijazo Zitakuwa Huru na Haki!, Mambo ya 2019/2020 Yasijirudie!
  46. Juma Duni "Babu Duni" Mwenyekiti, ACT Wazalendo; ACT Tumefarijika Sana na Rais Samia Kubadili Sheria, Tunaomba Ratiba ya Utekelezaji
  47. Face 2 Face with Zitto Kabwe, Kiongozi Mkuu wa ACT Wazalendo: "Tunafanya Politics of Engagement kwa kuwa Pragmatic on What is Possible"
  48. JNICC: Mkutano wa Baraza la Vyama vya Siasa na Wadau wa Demokrasia Kutathmini Utekelezaji wa Mapendekezo ya Kikosi Kazi na Hali ya Siasa Nchini
  49. Watanzania tutaendelea kusubiri mpaka lini Bunge likitunga Sheria batili na kuuchomekea ubatili huo ndani ya Katiba yetu? Tufanye nini?
  50. Ijue Katiba kwa Jicho la Mtunga Katiba: Mtunga Katiba alimaanisha nini aliposema "Katiba ni Sheria Mama"? Ni kweli Katiba ni Sheria Mama?
  51. Ijue Katiba ya JMT kwa Jicho la Mtunga Katiba: Watanzania Tusishabikie Uhaini. Hukuna Uhaini wa Kauli na Maneno, Uhaini ni Mipango na Matendo
  52. Mnaonaje Uchaguzi wa Serikali za Mtaa Ufanywe Siku Moja na Uchaguzi Mkuu na Usimamiwe na Tume Huru ya Uchaguzi? Samia Atabarikiwa Sana!
  53. Wajua japo Rais ni sehemu ya Bunge, bado hana mamlaka ya kuliingilia Bunge? Ili kufuta IGA ya DPW, Rais anapaswa kulivunja Bunge?
  54. Je, umefika wakati kutimiza Uzalendo wa kweli wa kwenda kwenye Serikali moja?
  55. Asante Rais Samia kwa Muswada huu. Umuhimu wa mabadiliko ya Katiba kabla ya Sheria hii bado ni muhimu sana. Huu ni uchambuzi Wangu - Part 1
  56. Je Wajua Muswada Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani 2023 ni Batili?. Ni Mvinyo wa Zamani, Kwenye Chupa Mpya?. Why Ubatili Huu?!.
  57. Madudu ya ajabu ya ubatili wa Katiba yetu, mabadiliko "fake" ya sheria na Tume ya Uchaguzi, Rais Samia asilaumiwe kwasababu yeye sio mwanasheria!.
  58. Tujifunze kuwa na Shukrani kwa Madogo ili Tupatiwe Makubwa!. Japo Tulitaka Kikubwa, Tumepewa Kiduchu!, Tukipokee Tushukuru, au Tususe Kudai Kikubwa?.
  59. Lile fupa lililowashinda marais wanaume 4, rais mwanamke 1 aligegeda kama mlenda!. Miswada 3 ya ukombozi mpya wa taifa letu yatua bungeni asubuhi hii
  60. Mabadiliko ya Sheria ya Uchaguzi: Je Tupige Ndege Wawili kwa Jiwe Moja kwa Uchaguzi Serikali za Mitaa/Mkuu, Ufanyike Siku Moja au Tuendeleze Mazoea?
  61. Licha ya Mapungufu, Sheria Mpya ya Uchaguzi Pia ina Mazuri Yake!, Imerejesha Mamlaka ya Uchaguzi kwa Wananchi, Hakuna Kupita Bila Kupingwa!.
  62. Ili kuisaidia nchi na kumsaidia Rais Samia, je tumfanyie an honest MTR based on SMART Objectives za tulipotoka, tulipo to determine tunapokwenda?
  63. Tuombe Mwaka 2024 Uwe ni Mwaka wa Mageuzi ya Kweli ya Kidemokrasia ya Kweli Tanzania!, Tume Huru, Uchaguzi Huru na wa Haki!. Happy New Year!
  64. Kufanya Kosa, Si Kosa, Kosa Kurudia Kosa!. Sheria ya Uchaguzi ni Kosa!, Kwanini Tunarudia Kosa?!. Haki Sii Hisani ni Stahiki!. Bunge Tutendeeni Haki!
  65. Rais Samia Japo Si Mwanasheria, Lakini Anaijua Katiba ni Sheria Mama Yenye Haki Zote Ndani ya JMT. Je Aruhusu Haki Hizi Ziporwe Tena? Au, Azirejeshe?.
Mungu Ibariki Tanzania

Paskali.
 
Wanabodi,

Kama kawa, kila nipatapo fursa, huja na makala zangu elimishi kuhusu Tanzania yetu zinazokwenda kwa jina la "Kwa Maslahi ya Taifa", kuzungumzia jambo lolote la kisiasa, kiuchumi na kijamii, makala ya leo ni muendelezo wa mfululizo wa makala za Ijue Katiba ya JMT-4, ikijikita kwenye Haki za Kikatiba za Mtanzania. Hizi ni haki mbalimbali zilizotolewa na katiba ya Tanzania kwa raia wa Tanzania.

Mada ya leo ni kuhusu Haki, Haki, Haki! Serikali, Bunge, Mahakama, Hazina Uwezo Wala Mamlaka ya Kupora Haki ya Kuchagua na Kuchaguliwa zilizotolewa na Katiba ya JMT ya mwaka 1977. Serikali yetu na Bunge letu lilipata wapi uwezo na mamlaka ya kuzipora haki hizi?, ambapo mpaka hapa ninapoandika haki hizi bado zimeporwa! Kubadili Sheria ni fursa ya kuzirejesha haki zilizoporwa, jee tutachangamkia fursa? Au kwa vile aliyezipora sio yeye, yeye kaingia kakutwa zimeishaporwa na sasa anafanya marekebisho mengine yoyote, ila kuhusu katiba, isiguswe?

Huu ni muendelezo wa kumlilia mtu ili kumuonyesha jicho lake lione dhulma waliotendewa Watanzania, ambayo sasa inataka kujirudia kwenye hii sheria mpya ya uchaguzi. Je, tuendelee kupiga tuu kelele mwisho wa. Siku, jicho ona litaona, na sikio sikia litasikia, au huku ni kujifurahisha tuu na kujifariji tuu lakini Jicho Ona limeisha ingia upofu na sikio sikia limeisha ingia uziwi?, hivyo hakuna kitachoonekana wala kitakacho sikika!.
Naomba kuanza bandiko hili kwa promo ya kipindi changu yenye nukuu ya Rais Samia akizungumzia Katiba sheria na Haki.
View: https://youtu.be/ZJIKhnZCf04?si=X2_XiivL4eD6OhBq hivyo hiki ninachokifanya kwenye bandiko hili ndio huo utoaji wa elimu ya katiba sheria na utetezi wa haki za msingi za hawa binadamu wa Tanzania.

Haki ziko nyingi, lakini mimi nitajikita kwenye haki 4 Kuu za Mtanzania.
  1. Haki kuu ya kwanza ni haki ya uraia. Mtu yoyote akizaliwa ndani ya ardhi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mtu huyu anakuwa ni raia wa Mtanzania kwa kuzaliwa, haki hii ni haki ya kwanza ya msingi ambayo ni haki ya kuwa Mtanzania. Haki hii haiwezi kuondolewa na mamlaka yoyote, ila unaweza kuipoteza endapo utaukana Uraia wako. Hivyo ile sheria yetu ya kuwa mtu akichukua uraia wa nchi nyingine yoyote, anaupoteza Utanzania wake, ni sheria batili kinyume cha katiba, ila ubatili huu, haujabatilishwa kwasababu hakuna aliyefungua shauri mahakamani kuipinga.
  2. Haki kuu ya pili ni haki ya kuchagua iliyotolewa na ibara ya 5 ya katiba ya JMT. Haki hii ni kila raia wa Tanzania anapofikisha umri wa miaka 18, ana haki ya kuchagua kiongozi wake. Haki hii inatekelezwa kwa kila mtu kujiandikisha kupiga kura. Haki hii haiwezi kuondolewa na mamlaka yoyote. Kwa Tanzania, haki hii imefinyangwa finyangwa kwa baadhi ya watu kunyamaza haki hii, kwa kufungwa magezani, wagonjwa mahospitalini, na Watanzania walioko nje ya nchi. Kufuatia maendeleo makubwa ya Teknolojia, na andikishaji unaotumia BVR hivyo kwa kutumia biometric data, kitambulisho cha taifa au passport ambavyo vyote vina biometric data, vinaweza kutumika kuwawezesha Watanzania wote popote walipo kumchagua Rais wa Tanzania na rais wa Zanzibar popote pale walipo.
  3. Haki kuu ya tatu ni haki kuchaguliwa kupitia ibara ya 21 ya katiba ya JMT kwa mtu mwenye miaka 21, yuko huru kugombea nafasi yoyote ya uongozi kuanzia serikali za mitaa hadi serikali kuu. Haki hii ni haki ya msingi na haiwezi kuondolewa na mamlaka yoyote. Kwa Tanzania, haki hii ya kila Mtanzania ana haki ya kugombea nafasi yoyote ya uongozi na kuchaguliwa imefutwa kwa kuchomekewa shurti la kudhaminiwa na chama cha siasa. Shurti hili ni batili!.
  4. Haki ya Watanzania kuanzisha vyama na kujiunga na vyama vya siasa sio haki ya msingi, uhuru wa mtu kujiunga na chama cha siasa ni hiyari, hilarious hiyo ya kujiunga na vyama vya siasa na kuwa mwanachama wa chama cha siasa, hakiwezi kumuondolea Mtanzania haki yake ya msingi ya kuchagua na kuchaguliwa!.
  5. Serikali ya Tanzania, haiwezi kutunga muswada batili unaopora haki ya msingi ya mtu kuchagua na kuchaguliwa, na kumlazimisha lazima ajiunge na chama cha siasa. Shurti hili ni kinyume cha Ibara ya 11 ya katiba ya Tanzania. Serikali yetu imepeleka muswada batili wa kutunga sheria batili ya uchaguzi, yenye kipengele hicho kinyume cha katiba!.
  6. Bunge la Tanzania, likaupitisha ubatili huo wa serikali, kuwanyima haki Watanzania, na kutunga sheria batili ya uchaguzi yenye shurti la kudhaminiwa na chama cha siasa ndipo mtu ugombee uongozi. Bunge halina mamlaka hayo ya kuondoa haki ya kikatiba ya kila Mtanzania kuchagua na kuchaguliwa!.
  7. Mahakama Kuu ya Tanzania, kupitia kesi ya Mchungaji Mtikila, iliibatilisha sheria hiyo kuwa vipengele hivyo ni batili, Serikali ikakata rufaa ikashindwa.
  8. Serikali yetu ikafanya jambo la ajabu sana, ikauchukua ubatili huo na kuuchomekea ndani ya Katiba yetu kiubatili, kwa kufanya mabadiliko ya katiba kwa hati ya dharura, hivyo shurti la mgombea kudhaminiwa na chama cha siasa liko kwenye ibara 39 na 68 ya katiba ya JMT ya mwaka 1977.
  9. Mchungaji Mtikila, hakukubali katiba yetu inajisiwe, akafungua shauri jingine kupinga mabadiliko hayo ya katiba yetu ya kiubatili kuchomeka vipengele batili ndani katiba yetu. Mahakama Kuu ikampa ushindi na kutangaza mabadiliko hayo ya katiba ni batili, hivyo hukumu ya mahakama kuu bado inasimama!.
  10. Serikali yetu ikaomba mapitio, ndipo mahakama ya Rufaa ikakaa full bench chini ya majaji 7, na kupitisha uamuzi wa ajabu kabisa kuwahi kufanywa na Mahakama nchini, pale ilipotamka "The Court is Not The Custodian of The Will of The People"!, na kulirudisha suala hilo Bungeni!, Bunge mpaka leo, mpaka kesho, halijarekebisha ubatili huu hivyo huku ni kuwatendea dhambi kubwa Watanzania!.
  11. Kama serikali haina mamlaka ya kufuta haki iliyotolewa na katiba, Bunge halina mamlaka ya kutunga sheria batili inayokwenda kinyume cha katiba kwa kufuta haki hiyo, Mahakama ya Rufaa pia haikutimiza wajibu wake, kusema the court is not the custodian of the will of the people, wakati serikali imekiuka katiba kutunga muswada batili, Bunge likakiuka katiba kutunga sheria batili, na Mahakama Kuu kuutangaza tuu ubatili bila kuubatilisha ni kutotimiza wajibu wake kikamilifu, na kitendo cha Mahakama ya Rufaa kuligwaya Bunge katika ukiukwaji wa katiba, ni kutotimiza wajibu wake kikamilifu.
  12. Hii senema au kwa lugha watoto wa mjini, movie ya serikali yetu, kututungia sheria batili inayokwenda kinyume cha katiba ya JMT halafu Bunge letu Tukufu likatutungia sheria batili inayokwenda kinyume cha katiba ya JMT, inataka kujirudia kwenye hii sheria mpya ya uchaguzi, itakayosomwa Bungeni kwa mara ya pili, ni muendelezo wa ubatili ule ule ambao Mahakama Kuu iliisha ubatilisha, sasa sijui tunyamaze kimya na kulisubiria Bunge letu Tukufu litutungie sheria batili nyingine tena ndipo twende Mahakamani kuupinga ubatili, au tuendelee kupiga kelele labda lile jicho ona pia litauona ubatili huu, na sikio sikia litausikia ubatili huu?.
Hitimisho
Mimi ni muumini wa kitu kinachoitwa karma, kinachotumia kanuni za Newton's laws of motion, kwa everything happens for a reason, no one knows kwanini ni Nyerere, Mkapa na Magufuli, na sio Mwinyi, Kikwete na sasa Samia, haki ninayoizungumza hapa ni haki kuu ya msingi, kuidhulumu ni dhambi kubwa!. Kwa vile no-one knows kwanini wale, mimi muumini wa karma, ninawaambia it's karma!, kama Mama anaweza kuwarejeshea haki hii Watanzania, atabarikiwa sana, ila pia ili kumuepushia na bad karma, Mama asiruhusu kabisa dhulma hii kwa Watanzania ijirudie katika awamu yake, tufanye kwanza mabadiliko madogo ya katiba, kuondoa dhulma hii, kisha ndipo tufanya mabadiliko ya Sheria ziwe ni sheria za haki.

Wasalaam.
Paskali.

upotoshaji wa wazi uliowasilishwa kwa umahiri mkubwa lakini bila umakini, na mwalimu wa sheria, muandishi hodari wa habari, msomi na kada wa chama tawala CCM ..

nasita na kuona haya ku-criticize haki hadi haki kwa heshima na stahaha tu...

bandiko elimishi la leo ni fujo na ni aina ya maandamano ya kisayansi ya kugomea kambi au kutafuta sababu au njia ya kukimbia Kambi au familia ilokuzaa, kukulea na kukukuza 🐒

Nachelea kusema, siungi mkono upotoshaji huu japo ni wa kiungwana...
 
Wanabodi,

Kama kawa, kila nipatapo fursa, huja na makala zangu elimishi kuhusu Tanzania yetu zinazokwenda kwa jina la "Kwa Maslahi ya Taifa", kuzungumzia jambo lolote la kisiasa, kiuchumi na kijamii, makala ya leo ni muendelezo wa mfululizo wa makala za Ijue Katiba ya JMT-4, ikijikita kwenye Haki za Kikatiba za Mtanzania. Hizi ni haki mbalimbali zilizotolewa na katiba ya Tanzania kwa raia wa Tanzania.

Mada ya leo ni kuhusu Haki, Haki, Haki! Serikali, Bunge, Mahakama, Hazina Uwezo Wala Mamlaka ya Kupora Haki ya Kuchagua na Kuchaguliwa zilizotolewa na Katiba ya JMT ya mwaka 1977. Serikali yetu na Bunge letu lilipata wapi uwezo na mamlaka ya kuzipora haki hizi?, ambapo mpaka hapa ninapoandika haki hizi bado zimeporwa! Kubadili Sheria ni fursa ya kuzirejesha haki zilizoporwa, jee tutachangamkia fursa? Au kwa vile aliyezipora sio yeye, yeye kaingia kakutwa zimeishaporwa na sasa anafanya marekebisho mengine yoyote, ila kuhusu katiba, isiguswe?

Huu ni muendelezo wa kumlilia mtu ili kumuonyesha jicho lake lione dhulma waliotendewa Watanzania, ambayo sasa inataka kujirudia kwenye hii sheria mpya ya uchaguzi. Je, tuendelee kupiga tuu kelele mwisho wa. Siku, jicho ona litaona, na sikio sikia litasikia, au huku ni kujifurahisha tuu na kujifariji tuu lakini Jicho Ona limeisha ingia upofu na sikio sikia limeisha ingia uziwi?, hivyo hakuna kitachoonekana wala kitakacho sikika!
Naomba kuanza bandiko hili kwa promo ya kipindi changu yenye nukuu ya Rais Samia akizungumzia Katiba sheria na Haki.

Hivyo hiki ninachokifanya kwenye bandiko hili ndio huo utoaji wa elimu ya katiba sheria na utetezi wa haki za msingi za hawa binadamu wa Tanzania.

Haki ziko nyingi, lakini mimi nitajikita kwenye haki 4 Kuu za Mtanzania.
  1. Haki kuu ya kwanza ni haki ya uraia. Mtu yoyote akizaliwa ndani ya ardhi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mtu huyu anakuwa ni raia wa Mtanzania kwa kuzaliwa, haki hii ni haki ya kwanza ya msingi ambayo ni haki ya kuwa Mtanzania. Haki hii haiwezi kuondolewa na mamlaka yoyote, ila unaweza kuipoteza endapo utaukana Uraia wako. Hivyo ile sheria yetu ya kuwa mtu akichukua uraia wa nchi nyingine yoyote, anaupoteza Utanzania wake, ni sheria batili kinyume cha katiba, ila ubatili huu, haujabatilishwa kwasababu hakuna aliyefungua shauri mahakamani kuipinga.
  2. Haki kuu ya pili ni haki ya kuchagua iliyotolewa na ibara ya 5 ya katiba ya JMT. Haki hii ni kila raia wa Tanzania anapofikisha umri wa miaka 18, ana haki ya kuchagua kiongozi wake. Haki hii inatekelezwa kwa kila mtu kujiandikisha kupiga kura. Haki hii haiwezi kuondolewa na mamlaka yoyote. Kwa Tanzania, haki hii imefinyangwa finyangwa kwa baadhi ya watu kunyamaza haki hii, kwa kufungwa magezani, wagonjwa mahospitalini, na Watanzania walioko nje ya nchi. Kufuatia maendeleo makubwa ya Teknolojia, na andikishaji unaotumia BVR hivyo kwa kutumia biometric data, kitambulisho cha taifa au passport ambavyo vyote vina biometric data, vinaweza kutumika kuwawezesha Watanzania wote popote walipo kumchagua Rais wa Tanzania na rais wa Zanzibar popote pale walipo.
  3. Haki kuu ya tatu ni haki kuchaguliwa kupitia ibara ya 21 ya katiba ya JMT kwa mtu mwenye miaka 21, yuko huru kugombea nafasi yoyote ya uongozi kuanzia serikali za mitaa hadi serikali kuu. Haki hii ni haki ya msingi na haiwezi kuondolewa na mamlaka yoyote. Kwa Tanzania, haki hii ya kila Mtanzania ana haki ya kugombea nafasi yoyote ya uongozi na kuchaguliwa imefutwa kwa kuchomekewa shurti la kudhaminiwa na chama cha siasa. Shurti hili ni batili!.
  4. Haki ya Watanzania kuanzisha vyama na kujiunga na vyama vya siasa sio haki ya msingi, uhuru wa mtu kujiunga na chama cha siasa ni hiyari, hilarious hiyo ya kujiunga na vyama vya siasa na kuwa mwanachama wa chama cha siasa, hakiwezi kumuondolea Mtanzania haki yake ya msingi ya kuchagua na kuchaguliwa!.
  5. Serikali ya Tanzania, haiwezi kutunga muswada batili unaopora haki ya msingi ya mtu kuchagua na kuchaguliwa, na kumlazimisha lazima ajiunge na chama cha siasa. Shurti hili ni kinyume cha Ibara ya 11 ya katiba ya Tanzania. Serikali yetu imepeleka muswada batili wa kutunga sheria batili ya uchaguzi, yenye kipengele hicho kinyume cha katiba!.
  6. Bunge la Tanzania, likaupitisha ubatili huo wa serikali, kuwanyima haki Watanzania, na kutunga sheria batili ya uchaguzi yenye shurti la kudhaminiwa na chama cha siasa ndipo mtu ugombee uongozi. Bunge halina mamlaka hayo ya kuondoa haki ya kikatiba ya kila Mtanzania kuchagua na kuchaguliwa!.
  7. Mahakama Kuu ya Tanzania, kupitia kesi ya Mchungaji Mtikila, iliibatilisha sheria hiyo kuwa vipengele hivyo ni batili, Serikali ikakata rufaa ikashindwa.
  8. Serikali yetu ikafanya jambo la ajabu sana, ikauchukua ubatili huo na kuuchomekea ndani ya Katiba yetu kiubatili, kwa kufanya mabadiliko ya katiba kwa hati ya dharura, hivyo shurti la mgombea kudhaminiwa na chama cha siasa liko kwenye ibara 39 na 68 ya katiba ya JMT ya mwaka 1977.
  9. Mchungaji Mtikila, hakukubali katiba yetu inajisiwe, akafungua shauri jingine kupinga mabadiliko hayo ya katiba yetu ya kiubatili kuchomeka vipengele batili ndani katiba yetu. Mahakama Kuu ikampa ushindi na kutangaza mabadiliko hayo ya katiba ni batili, hivyo hukumu ya mahakama kuu bado inasimama!.
  10. Serikali yetu ikaomba mapitio, ndipo mahakama ya Rufaa ikakaa full bench chini ya majaji 7, na kupitisha uamuzi wa ajabu kabisa kuwahi kufanywa na Mahakama nchini, pale ilipotamka "The Court is Not The Custodian of The Will of The People"!, na kulirudisha suala hilo Bungeni!, Bunge mpaka leo, mpaka kesho, halijarekebisha ubatili huu hivyo huku ni kuwatendea dhambi kubwa Watanzania!.
  11. Kama serikali haina mamlaka ya kufuta haki iliyotolewa na katiba, Bunge halina mamlaka ya kutunga sheria batili inayokwenda kinyume cha katiba kwa kufuta haki hiyo, Mahakama ya Rufaa pia haikutimiza wajibu wake, kusema the court is not the custodian of the will of the people, wakati serikali imekiuka katiba kutunga muswada batili, Bunge likakiuka katiba kutunga sheria batili, na Mahakama Kuu kuutangaza tuu ubatili bila kuubatilisha ni kutotimiza wajibu wake kikamilifu, na kitendo cha Mahakama ya Rufaa kuligwaya Bunge katika ukiukwaji wa katiba, ni kutotimiza wajibu wake kikamilifu.
  12. Hii senema au kwa lugha watoto wa mjini, movie ya serikali yetu, kututungia sheria batili inayokwenda kinyume cha katiba ya JMT halafu Bunge letu Tukufu likatutungia sheria batili inayokwenda kinyume cha katiba ya JMT, inataka kujirudia kwenye hii sheria mpya ya uchaguzi, itakayosomwa Bungeni kwa mara ya pili, ni muendelezo wa ubatili ule ule ambao Mahakama Kuu iliisha ubatilisha, sasa sijui tunyamaze kimya na kulisubiria Bunge letu Tukufu litutungie sheria batili nyingine tena ndipo twende Mahakamani kuupinga ubatili, au tuendelee kupiga kelele labda lile jicho ona pia litauona ubatili huu, na sikio sikia litausikia ubatili huu?
Hitimisho
Mimi ni muumini wa kitu kinachoitwa karma, kinachotumia kanuni za Newton's laws of motion, kwa everything happens for a reason, no one knows kwanini ni Nyerere, Mkapa na Magufuli, na sio Mwinyi, Kikwete na sasa Samia, haki ninayoizungumza hapa ni haki kuu ya msingi, kuidhulumu ni dhambi kubwa! Kwa vile no-one knows kwanini wale, mimi muumini wa karma, ninawaambia it's karma! Kama Mama anaweza kuwarejeshea haki hii Watanzania, atabarikiwa sana, ila pia ili kumuepushia na bad karma, Mama asiruhusu kabisa dhulma hii kwa Watanzania ijirudie katika awamu yake, tufanye kwanza mabadiliko madogo ya katiba, kuondoa dhulma hii, kisha ndipo tufanya mabadiliko ya Sheria ziwe ni sheria za haki.

Wasalaam.
Paskali.

Tunataka katiba na si viraka kwenye katiba, uoga wa kuwa na katiba ni dalili za uovu uliomo mioyoni mwao, katiba ni ya wote haichagui haibagui ila viraka vinachagua na kubagua.
 
Back
Top Bottom