Zuzu agoma kurudi Tanzania

ng'wanankamba

JF-Expert Member
Dec 15, 2010
345
118
ZUZU ALIGOMA KURUDI TANZANIA BAADA YA LIKIZO YAKE MAREKANI KWA MJOMBA WAKE. MJOMBA WAKE AKAMUULIZA "MPWA KWANINI USIRUDI TANZANIA THEN UTAKUJA HUKU UKIMALIZA FORM 6?" ZUZU AKASEMA "UNCLE KWA MAJIBU HAYA KWENYE DALADALA kwa MWAKA 2011 UNGEKUWA WW UNGETAMANI KURUDI TANZANIA?".... Zuzu akachukua diary yake na kuanza kumusomea.

TAREHE 16/02/2011
ZUZU: "Nyimbo gani mnapiga?!? Wekeni nyimbo za yesu.."
Konda: "Vunga wewe, Yesu bado hajatoa album..."
********************************
TAREHE 05/4/2011
ZUZU: "Kuna Kiti au unasema panda tu!?"
Konda: "We taahira nini, hao wengine wamekalia ndoo?! "
*******************************
TAREHE 28/06/2011
ZUZU: "Embu punguzeni sauti ya redio..."
Konda: "Sheria za nchi tu ziko za kutosha, tusikilize na zako!?"
*******************************
TAREHE 4/07/2011
ZUZU: "Bwana ondoa gari joto sana!!"
Konda: "Uctuzingue wewe, shuka upande fridge...."
******************************
TAREHE 10/9/2011
Konda: "kaka, kuna siti pale nyuma,ingia...."
ZUZU: "Siwezi kaa siti za nyuma..."
Konda: "Kwenda zako wewe, sio muendaji!!! Kwani za nyuma ziko nje ya gari?!"
********************************
TAREHE 16/10/2011
ZUZU: "Konda unanibana bwana..."
Konda: "Zinabanana ndizi haziongei, kama ulitaka kujiachia c ungekoni treni pekeyako!!!"
*******************************
TAREHE 16/11/2011
ZUZU: "Kuna kiti?! Kama hamna sipandi..."
Konda: "Mpuuzi kweli, wa wapi wewe... Kama ulikuwa unaogopa kukosa kiti c ungebeba chako!!?"
********************************
ZUZU; "nihamishie hukuhuku nisome hakuna shida"
 
Hii nayo ni marudio japo mtoaji ameitoa kwa jina la zuzu.

Tena ilikuwa hapa mwezi uliopita tu na hakika ukifungua page ya pili baada ya hii ya kwanza itakuwepo. tujitahidi kusoma kwanza post zilizopo sio kurudiarudia tu jamani.

ZuKU
 
Back
Top Bottom