Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoa wa Mwanza imewaachia huru washtakiwa 81 kati ya 84 akiwemo Diana Bundala maarufu 'Mfalme Zumaridi' kwenye kesi namba 12/2022.
Katika kesi hiyo Zumaridi na wenzake walikuwa wanakabiliwa na shtaka la kufanya kusanyiko lisilo halali, kosa wanalodaiwa kulitenda nyumbani kwa mhubiri huyo mtaa wa Buguku kata ya Buhongwa jijini Mwanza.
Akisoma uamuzi huo leo Jumanne Desemba 5, 2022, Hakimu Mkazi Mwandamizi wa mahakama hiyo, Clescensia Mushi amesema mahakama imejiridhisha pasi na shaka kuwa washtakiwa walioachiwa huru hawakuguswa na vipengele vinavyotakiwa kuthibitisha makosa ya jinai.
Chanzo: Mwananchi