Kwasababu
Ukiwa na wake zaidi ya mmoja
1.probability ya kupata ukimwi ni almost 1. Na ndio maana unaona sie waafrika tumeathirika kwa ukimwi sana.
2.kwa vile condom ni culture ya mzungu, probability ya kuitumia kwa mtu mwenye mtazamo tofauti ni ndogo na pia uzazi wa mpango ni culture ya mzungu vilevile probability ya ku-praktsi ni ndogo sana, hivyo basi probability ya kupata watoto beyond of control ni kubwa sanaaaaaa almost 1.
3.Kutoka na point ya 2, probability ya kushindwa kuwahudumia walio ktk pointi ya 2 ni kubwa,kielim,kiafya na kimiundo mbinu.
4.Kutokana na pointi 3, probability ya kuwa masikini ya watu kutoka pointi 2 ni kubwa mno almost 1.
5.kutokana na pointi 1 hadi 4 kinachopatikana ni kizazi cha kulalama tu ,kilicho masikini wa kutupwa hata kuwanunulia nguo za shule watu wa pointi 2 hakiwezi, na kikitegemea serikali yao ndo ifanye hivyo.
Point no. 1:
ukiwa na wake: Mke, awe mmoja, wawili mpaka kikomo cha wanne (kwa waislamu) au zaidi ya idadi hiyo kwa mujibu wa vikomo vya mila za hao wengine wasio waislamu, hufanywa kimaadili kwa misingi ya mila/sharia husika. Ni tofauti kabisa na zinaa (mwanamke na mwanamme wasiooana) na aina nyengine za maasi ya kiuvundo pale spirituality inapotenganishwa na jimai (sex), mfano sodomites na lesbianisms.
Vitendo hivyo wanavyovipiwa debe na hao wazungu na kuigwa kama mitindo na baadhi ya wapuuzi miongoni mwetu, ndivyo vilivyo/vinavyochangia kuenea kwa maradhi ambayo vizazi vyetu vilivyopita hawakuwahi ku-experience kama vile ukimwi na mengineyo kinyume na takwimu zako za kipuuzi na kukosa kwako heshima juu ya taasisi za kimaadili kama ndoa, iwe ya mke mmoja au mitara. Taasisi takatifu ya Ndoa ni victim tu katika hili, na haina mchango wowote katika kusababisha wala kueneza maradhi-adhabu ya zinaa kama ukimwi, n.k. Washutumiwa kwa haya ni Zinaa na uchafu mwengine wa liwati. Jua vizuri tofauti hizi.
Ama kuhusu sisi waAfrika kuwa waathirika sana ni kwasababu ya kwamba daima mwenye kuiga upumbavu basi ni mpumbavu zaidi, na athari za upumbavu humkumba zaidi aliye bora katika upumbavu. Ashakumu si matusi, sisi kupenda kuiga maadili ya kipumbavu ya kizungu (zinaa, liwati nk kuwa mambo ya kawaida badala ya kuwa maasi ya nadra) utatufanya kuwa mbele zaidi kiupumbavu kuliko waanzilishi wa upumbavu.
Pointi no. 2:
Uzazi wa mpango ni culture ya mzungu: Hii ni absolute crap. Kwa mujibu wa maadili yangu mimi, na mimi ni Mtz labda tu tofauti na baadhi waTz wenzangu wengine wasio waislamu, ni kwamba mimi ni miongoni mwa waTZ walioukubali uislmau na kuwa muislamu na kujaribu niwezavyo kuufuata. Uzazi wa mpango (sio kuzuia kizazi) ni jambo lililo ndani ya uislamu. Misingi, taratibu na mipaka ya uzazi wa mpango iliyo ndani ya uislamu (tofautisha na uarabu) ni bora zaidi kuliko ile inayoletwa na mzungu ambazo zimekoza mwelekeo na kuwa ni
kuzuia uzazi kutokana na hiyana(selfishness), unbilief (ukosefu wa imani), greed (uroho), maonyesho, majigambo badala ya ukweli wa mambo (fashion badala ya reality)na kuleta maradhi mapya katika jamii. Jaribu wewe kuhesabu na kupima faida (zipo, sikatai kwa maana wao vilevile ni binadamu) zake na hasara zake uone mwenyewe kama una macho ya imani, elimu, busara na hekima za kibinadamu na makusudi ya kuwepo kwetu ulimwenguni.
Chemsha bongo/scenario/hypothesis:
"Matumizi na ufahamu wa faida na matumizi ya condom worldwide yameongezeka maradufu ukilinganisha na miaka ya 70s' na 80's. Kinyume na matarajio yaliyokusudiwa idadi ya wanaoambukizwa virusi vya ukimwi na kufa kutoka na maradhi yatokanayo ime/inaongezeka maradufu vilivile. Bila ya kutaka figures, hii ni reality unless hukubaliani nayo. Vile vile idadi ya watu (world population) ina/imeongezeka. Kwanini hivi kitakwimu???"