Zuma anatua Tanzania, tunasahauri nini juu ya huyu nguli wa siasa?

WAZIWAZI

JF-Expert Member
Mar 10, 2014
1,815
1,575
Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma anatarajiwa kuzuru nchini Tanzania hii leo katika ziara ya rasmi ya siku tatu kufuatia mwaliko wa rais John Pombe Magufuli.

Akizungumza na vyombo vya habari siku ya Jumatatu Waziri wa maswala ya kigeni nchini Tanzania Augustine Mahiga alisema kuwa ziara hiyo inalenga kuimarisha uhusiano wa kibiashara mbali kuangazia maswala mbali mbali ya maendeleo.

Rais Zuma ataandamana na mawaziri sita pamoja na wafanyibiashara kadhaa kutoka Afrika Kusini.

Atakuwa nchini humo kuanzia tarehe 10 hadi 13 akitarajiwa kufanya mazungumzo na mwandalizi wake rais Magufuli katika ikulu ya rais.

Kulingana na Mahiga kiwango cha biashara kati ya mataifa hayo mawili kimeongezeka kutoka dola milioni 803 mwaka 2006 hadi dola bilioni 2.2 2016 hatua iliobuni ajira 20,916.

Swali kama mwana JF ni kipi cha muhimu kifanyike katiaka mazungumzo yao ili nchi yetu isonge.


Chanzo BBC-Swahili
 
Wafanyabiashara wa south walikuja wakafanya yao wakaondoka, jamani sie kweli shamba la bibi.
 
Wazungumzie pia utaratibu wa kuwaondoa watanzania wanaoishi South Africa bila kuzingatia Sheria hata kwa walioingia kihalali
 
Me nadhan kwasasa tumeshachelewa kuwashaur nn cha kuongea, i guess tayar wana agenda zao, labda tushaur kwajil ya safar nyingne kama atakuja
 
Back
Top Bottom