Zuma amfukuza kazi waziri wa fedha Pravin Gordhan

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,411
_95401720_367645a1-173d-4385-9558-2019498acbc8.jpg

Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma amewafukuza kazi mawaziri wake kadhaa akiwemo Waziri wa fedha Pravin Gordhan pamoja na naibu wake Jonas Mkabisi ambao ndio waliokua sababu kuu ya kuwepo mabadiliko haya.

Taarifa kutoka ikulu ya Afrika Kusini zinasema Malusi Gigaba ameteuliwa kuwa waziri mpya wa fedha.

Takriban mawaziri 15 wametimuliwa katika kile kinachotajwa kama mshangao kwa serikali ya Zuma.

_95402045_8ffb6e27-e7e8-467a-9647-8a9c5629d7b9.jpg

Mapema wiki hii Gordhan aliamriwa kurudi nyumbani kutoka London alipokwenda kwa ziara ya kikazi, baada ya kutuhumiwa kuwa alikua akipanga njama za kuipindua serikali iliyopo madarakani.

Maafisa kadhaa kutoka chama tawala cha ANC wanapinga kuondolewa kwa Gordhan.

Chanzo: BBC
 
  • Thanks
Reactions: SDG

Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma amewafukuza kazi mawaziri wake kadhaa akiwemo Waziri wa fedha Pravin Gordhan pamoja na naibu wake Jonas Mkabisi ambao ndio waliokua sababu kuu ya kuwepo mabadiliko haya.

Taarifa kutoka ikulu ya Afrika Kusini zinasema Malusi Gigaba ameteuliwa kuwa waziri mpya wa fedha.

Takriban mawaziri 15 wametimuliwa katika kile kinachotajwa kama mshangao kwa serikali ya Zuma.

Mapema wiki hii Gordhan aliamriwa kurudi nyumbani kutoka London alipokwenda kwa ziara ya kikazi, baada ya kutuhumiwa kuwa alikua akipanga njama za kuipindua serikali iliyopo madarakani.

Maafisa kadhaa kutoka chama tawala cha ANC wanapinga kuondolewa kwa Gordhan.

Chanzo: BBC
Zuma anateua waziri wa fedha kutokana na matakwa ya Makaburu
 
Zuma hajui anachokifanya huyu jamaa kajitahidi kupiga kazi mpaka Rand ilipokua 17 against usd sasa ni 13.60 ngoja iporomoke tena akili imkae vizuri maana analazimisha mke wake agombee Urais katika ANC...
 
Back
Top Bottom