Zuchu kamchamba sana Mama Dangote kwenye 40 ya mwanaye

Zuchu kamchamba sana Mama Dangote kwenye 40 ya mwanaye

Hance Mtanashati

JF-Expert Member
Joined
Sep 7, 2016
Posts
25,883
Reaction score
35,938
Nilivumilia sana kutoipost hii habari lakini mmmmmh hapana kwa kweli acha tu niseme 🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣

Haihitaji uwe na degree au masters kujua kile kichambo cha Zuchu kilikuwa kinamlenga mama dangote.

Kwanza chaguzi tu ya wimbo na namna alivyoimba kihisia ni jibu tosha kwamba lile dongo lilikuwa la mama dangote.

Zuchu aliimba kwa ustadi wa hali ya juu wimbo wa Aso kasoro ni Mungu , wimbo wa jahazi modern taarabu ulioimbwa na Fatma Mahmoud ukipenda muite Fatma Nyoro au Fatma mcharuko.

Zuchu bwana huu wimbo kautendea haki kwa 100% . Ni ngumu kuamini huu wimbo Zuchu ameimba live bila chenga chenga .

Kwa miaka kadhaa hata wale waimbaji wa jahazi walikuwa wanapata tabu sana kuimba nyimbo aliizoimba Fatma Nyoro kipindi ambacho Fatma amepata dharura ya kutofika kwenye show, Ila Zuchu ameweza kuliziba hilo pengo kwa kiasi kikubwa sana licha ya kutokuwa msanii wa taarabu.

Nadhani hiyo yote imetokana na usongo wa kumchamba mtu fudenge , aache kufatilia mapenzi ya watu kuingilia ingilia hovyo na kuleta maneno yaliyo jaa husuda ili kuwafarakanisha wapendanao.

😂😂😂😂😂😂😂😂😂

Japo mtoto kapewa jina la mama dangote ila kichambo kilikuwa palepale.🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
Eti "Nilivumilia sana kutoipost hii habari lakini mmmmmh hapana kwa kweli acha tu niseme 🤣🤣"
Watu wa dar bwana aisee
13732.jpg
 
Back
Top Bottom