Zuchu adhihirisha hofu yake ya kuachwa na kujihami kwa kwikwi

Judithkaunda

Member
Aug 21, 2022
90
228
Habari Wana JF,
Mimi ni shabiki na mpenzi wa mziki mzuri haijalishi kaimba nani na kwa lugha gani.

Kwangu Zuchu ni msanii mwenye kipaji na sauti nzuri, lakini Leo nataka tuongelee huu wimbo wake mpya wa KWIKWI. Nadhani watu wanaucheza sana kuliko kusikiliza ujumbe wake

Haya ni baadhi ya maneno kwenye nyimbo hiyo,

Tena uzikumbuke ahadi, zile ulizonigea,
Mapenzi vita wee ndo gadi vipi utanitetea?
Usiruhusu wadangaji, wakaanza kukuzoea,
Unawajua mafisadi watapata chakunisemea.
Akili itazunguka ukiniacha mwenzako,
Maana nitaumbuka yote kwa ajili yako.

Zuhura namuelewa sana, kaamua KUJIHAMI mapema. Si unajua kuna tofauti kati ya kudate na kudate na msanii maarufu?

Embu vaa viatu vyake, karibu Taifa zima linajua anadate na Nasibu, na mapenzi yao yanaonekana na kuongelewa kila kona MTANDAONI, na siku akiachwa Taifa zima litajua.

Lazima kilio chake kiwe na KWIKWI nyingi sana😭.

Unakumbuka maneno gani umewahi kumwambia mpenzi wako Ili asikuache?

Au wewe ndiyo wale mnaouliza
"Kwani kuachana shingapi?"

Ni follow my friend tubadilishane mawazo.
 
Zuchu ndio mega supastaa wa kike east africa kwa sasa.

Hii couple ni kama jay z na beyonce knowles
 
Back
Top Bottom