ZoomTanzania.com ina boa na iache ukiritimba! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

ZoomTanzania.com ina boa na iache ukiritimba!

Discussion in 'Nafasi za Kazi na Tenda' started by Mlengo wa Kati, Nov 16, 2011.

 1. Mlengo wa Kati

  Mlengo wa Kati JF-Expert Member

  #1
  Nov 16, 2011
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 2,733
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Tovuti ya www.zoomtanzania.com ambayo imekua inatoa matangazo ya kazi imekua ina ficha anuani(email) za kazi husika ili muombaji aombe! Badala yake wameweka utaratibu amboa haueleweki eti utume kwenye kijedwali chao wa zoomtanzania halafu wao ndio wanawatumia sehemu husika walio tangaza kazi!
  My take:
  Binafsi ina niboa sana na ninashindwa kuelewa kwanini wafiche email za sehemu ilipotangazwa kazi badala yake wao wamebuni utaratibu wa muombaji aombe kwenda zoomtanzania na zoomtanzania ndio waitume kule! Huu ni ukiritimba na ina boa sana! Hata kama mko kwa ajiri ya Commission lakini utaratibu wenu una boa sana!
   
 2. shizukan

  shizukan JF-Expert Member

  #2
  Nov 16, 2011
  Joined: Jan 16, 2011
  Messages: 1,158
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Umeona eeh! Na hako kajedwali hakaruhusu kutuma zaidi ya attachment 4, sasa hapo kuna CV, Covering letter, sasa anza vyeti. Huo ni ufukunyuku wa kiswahili. Acha tuamini kuwa hawako kama serikali ya Tanzania, basi watatusikia na watalifanyia kazi, vinginevyo naungana mkono na mguu na Mlengo wa kati=INABOA
   
 3. king'amuzi

  king'amuzi JF-Expert Member

  #3
  Nov 16, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 613
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  ndiyo utaratibu wao kwani wewe unawalipa kwa kukutangazia kazi na kukutumia application zako? kama unawalipa malalamiko yako ni ya msingi kama no jaribu kuwa mstaarabu maana hapo ndipo wanapopata commission zao.
   
 4. CtVKiLaZA

  CtVKiLaZA JF-Expert Member

  #4
  Nov 16, 2011
  Joined: Sep 13, 2011
  Messages: 305
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Waweke hizo email ili iwe rahisi kutama. Mi sioni kama ni sawa kutuma maombi kupitia zoomTz. Wekeni mambo hadharani
   
 5. T

  Tsidekenu Senior Member

  #5
  Nov 16, 2011
  Joined: May 7, 2009
  Messages: 141
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Apart from this, mimi naona kama wanawamislead watu; listen to this,

  Hii inamaanisha kuwa watu wote walioapply kupitia wao cv zao hazijafika kwetu. Nawashauri tu watafuta kazi kuwa careful na haya makampuni ya siku hizi.
   
 6. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #6
  Nov 16, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  huwa nawaita madalali wa kazi
  Kuwa makini
   
 7. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #7
  Nov 16, 2011
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 0
  Hiyo ni njia ya kuongeza Trafick kwenye tovuti husika lakini wangeweka anuani kamili ingekuwa bora zaidi bila kuondoa zile zilizowekwa kwenye tangazo ambazo labda ziko kwenye magazeti na sehemu nyingine lakini pia kuna makosa wanayafanya kwenye matangazo yao kuelekeza mtu kwenda kwenye tovuti ambazo hazihusiani na zoomtanzania kwa ajili ya kufanya applications
   
 8. Shut Down

  Shut Down Member

  #8
  Nov 16, 2011
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamani eleweni..huo utaratibu unavuia/avoid sana sparming msg....!!thtz the main reason behind.

  NB: Kazi za kutuma kwenye email ni ngumu sana, its better ukatuma hard copy.
   
 9. kaygeezo

  kaygeezo Senior Member

  #9
  Nov 17, 2011
  Joined: Jul 31, 2008
  Messages: 194
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mitandao mingi ya kazi haswa wale wanaofanya kazi ya recruitment(kama huamini anza kufanya application za kimataifa) huwa hawaweki address ya muhusika(mwenye kazi) ,lakini mbona kazi nyingi za zoom zinatangazwa pia katika mitandao yetu mingine na address zipo?..cheki na huko acha kulalama ,.Pale zoom hata ukiweka tangazo unauza pipi kama email yako hujaiweka sehemu nyingine( say kwenye body field) zaidi ya ile sehemu yao ya email..haitoonekana. Security kwanza...
  ushauri: wenye kazi/au hata wewe tumia zoom na post kwenye ile sehemu ya free na email husika iweke wazi kwenye body ,sio tu kwenye field ya email. Otherwise me zoom nawakubali kama eBay vile....OVA!
   
 10. shizukan

  shizukan JF-Expert Member

  #10
  Nov 17, 2011
  Joined: Jan 16, 2011
  Messages: 1,158
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Hivi wewe, teknolojia imekukosea nini mpk utushauri wote tuikimbie wakati wenzako inatusaidia? Kutuma Hard-Copy maana yake, uanze kuprint, ununue stamp halafu uelekee iliko posta kupost na huo ni utaratibu wa kale wenye mlolongo mrefu. Kama kwako kutuma e-mail ni kazi mimi mwenzio ndio easiest way, just sitting here and post directly to the target. Hapa tunazungumzia tabia mbaya ya zoom na sio ipi ni njia sahihi. Tangu January nimetuma application zaidi ya 55, nikiwa sina kazi unategemea 1400 ya stamp, nauli ya kwenda posta, gharama za kurpint na kutoa kopi mavyeti yangu 8 nitaviweza vipi na kipato sina?

  Mawazo mabaya kabisa kuwahi kuyasikia mwaka huu
   
 11. shizukan

  shizukan JF-Expert Member

  #11
  Nov 17, 2011
  Joined: Jan 16, 2011
  Messages: 1,158
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Mimi hata sijakuelewa unaongea nini, naona maelezo meengi lkn yako kama sigara kali, hayaeleweki nyuma wapi mbele wapi
   
 12. Kwamex

  Kwamex JF-Expert Member

  #12
  Nov 17, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 378
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Jaribu kucopy CV, vyeti e.t.c kwenye Ms Word na itaenda kama attachment 1 na katika mpango safi, nadhani hata unayemtumia haitampa tabu kufunguafungua mafile mengi....Ila Zoom wanasaidia kutuletea matangazo ila sasa wao kuwa kizingiti cha maombi ya kazi kuwafikia walengwa nadhani ni TATIZO.
   
 13. kaygeezo

  kaygeezo Senior Member

  #13
  Nov 17, 2011
  Joined: Jul 31, 2008
  Messages: 194
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  pole...maelezo yangu ni mengi ila hayafanani na sigara kali bwana......
  kwa ufupi ni kwamba
  1.hata mitandao ya nje(mingi tu) ya ajira huwa hawaweki address za watangaza kazi.
  2.nafasi za kazi zinazotangawa zoom kwa bahati nzuri zipo pia mitandao mingine ambayo wao hupost free so address zipo wazi kabisa
  3.wewe ukiona tangazo kwingine lipost zoom kwenye free adverts na zile contacts ziweke kwenye sehemu ya ujumbe(ie ukiweka sehemu maalum ya contacts hatutaziona).
  kama una swali uliza ,
  zoom nawaunga mkono tu....
   
 14. shizukan

  shizukan JF-Expert Member

  #14
  Nov 17, 2011
  Joined: Jan 16, 2011
  Messages: 1,158
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Nimekusoma injinia, umeongea solution wise. Tena itanisaidia kuwalazimisha waajiri kuvitizama vyeti kwa mtiririko ninaoutaka mimi. Thank you sana!
   
 15. CtVKiLaZA

  CtVKiLaZA JF-Expert Member

  #15
  Nov 17, 2011
  Joined: Sep 13, 2011
  Messages: 305
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Nilifanya application kupitia ZoomTz, lakini baadae nilitumiwa email na organisation husika, kuwa attachment zangu hawajazipata. Hivyo nitume tena. Tangu cku hiyo cjarudia tena ku apply kutumia ZoomTz.
   
 16. t

  totolucky JF-Expert Member

  #16
  Nov 18, 2011
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 1,013
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 133
  Habari wana JamiiForums,

  Tumepokea malalamiko na maswali mengi sana kuhusu kwa nini hatuoneshi email address za waajiri ili wanaotafuta kazi watume maombi moja kwa moja. Wengine wanafikiria kuwa tunafanya hivyo maana tunataka / tunapata ‘Commission' kutoka kwa waajiri. Ni matumaini yetu maelekezo yafuatayo yatasaidia kuondoa utata uliopo.

  Kwanza kabisa, ZoomTanzania HATUTOZI kiasi chochote kile kwa ajili ya mtu kupost nafazi za kazi. Sisi tunatoa huduma hii BURE KABISA kwa waajiri na wanaotafuta kazi. Karibu Listings zetu zote ni bure, isipokuwa FEATURED BUSINESS LISTINGS [BUSINESS DIRECTORY LISTING], ambazo ni hiari kwa Biashara mbalimbali. Mapato makubwa ya ZoomTanzania yanatokana na kuuza nafasi za matangazo (banner ads) kwa makampuni mbalimbali. Mfano mzuri ni matangazo ya Tigo, Zantel, CFAO na mengine yaliyopo kwenye website yetu.

  Pili, tunaficha email za waajiri kwa sababu hivyo ndivyo wanavyopenda waajiri wengi. Ieleweke kuwa, hatufichi email kwenye nafazi za kazi tu, bali post zote zinazowekwa kwenye website yetu. Hii ni kawaida kabisa kwa website nyingi zilizotengenezwa mahsusi kwa ajili ya kutafuta kazi sehemu nyingi ulimwenguni. Kama tutaziweka email address ili zionekane, basi tutakumbwa na tatizo kubwa la programs kama "Spiders" na "Crawlers" ambazo utembelea kurasa zote za website yoyote ile, na hata yetu au yako, ili "kukusanya" email addresses ambazo zipo kwenye site hiyo. Ukipenda kupata taarifa zaidi juu ya suala hili waweza kujisomea mwenyewe kwenye link hii > Spambot - Wikipedia, the free encyclopedia.

  Baada ya email hizi kukusanywa, huwa zinauzwa kwa makampuni ambayo huzitumia email hizo kutuma SPAM zenye ujumbe kuhusu Viagra, Pornography na SCAM nyingine mbalimbali. Kwa hiyo, tusingezificha email, ni waajiri wachache sana ndo wangekubali kupost nafasi za kazi kwenye website yetu, na sisi tusingekuwa na kazi nyingi za ku-review na kuwajulisha kila siku.

  Mwisho kabisa, kumekuwa na malalamiko kuwa "attachments" hazifiki. Asilimia 99.999% ya email zote zinazotumwa kwa waajiri, huwa zinafika na attachments. Katika miezi 18 iliyopita na katika maelfu za nafasi za kazi zilizowekwa kwenye website yetu, tumepata malalamiko kutoka kwa waajiri 3 tu ambao walitutaarifu kuwa walikuwa hawapokei attachments. Hili si tatizo la system yetu, tatizo hili ni la ‘Security settings' za email ya mwajiri ambazo huzificha attachments. Mmoja wa waajiri alitupa email mbadala ya Gmail, ambayo tulipoitumia alianza kupokea email zenye attachments vizuri bila matatizo. Waajiri wengine wawili hawakutupa email mbadala, hivyo ilitulazimu kuzifuta kazi zao kutoka kwenye site yetu.

  Tunafanya kazi kubwa sana kuwaletea nafasi nyingi za kazi kila siku. Kama umekuwa unatuma maombi mengi ya kazi bila kuitwa kwenye mahojiano, kuna uwezekano mkubwa sana kuwa hauna vigezo vinavyohitajika kwa ajili ya hiyo nafasi au kuna watu wengine wengi waliotuma maombi ambao wana vigezo zaidi yako. Waajiri wengine huweka hili wazi kabisa, kuwa watawataarifu wale tu watakaokuwa ‘short-listed'. Lazima tuelewe kuwa kuna watu wengi sana wanaotafuta ajira kuliko nafasi za kazi zilizopo nchini Tanzania, hivyo kuna ushindani mkubwa sana katika kutafuta kazi. Wale wote ambao wanajua kuji-‘promote' vizuri na wanaotuma maombi kwa nafasi zile tu ambazo wana vigezo nazo, wana nafasi kubwa sana ya kupata kazi kuliko wale wasioweka jitihada katika barua za maombi na kufuata maelekezo ya mwajiri. Mtu mwenye vigezo na anayeweza kujieleza vizuri ndiye mwenye nafasi nzuri ya kuitwa kwenye mahojiano na kupata kazi.

  Kama jitihada zako za kutafuta kazi hazijakusaidia kupata nafasi ya mahojiani, sisi tunapendekeza usome mwongozo ambao tumeuandaa ili kukusaidia kukuongezea mafanikio katika kupata kazi > ZoomTanzania | Job Seekers Guide. Ukisoma mwongozo huu kwa makini na kuzingatia mafundisho yake, utajiongezea nafasi ya kupata kazi nzuri.
   
 17. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #17
  Nov 18, 2011
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,921
  Likes Received: 454
  Trophy Points: 180
  We bwana unachekesha sana....unapenda sana ease go....simply sitting, unatuma CV sio...dah huu umaskini huu, haya bana!!
  NB: Ujue kazi ikitangazwa basi we jua kwamba kila mwenye PC na laptop ataaply for simply sitting and send.
  Sasa hapo utakuta email zaidi ya 1000 zinahitaji kufunguliwa, kuzidownload na kuzipitia....nani atafanya hiyo kazi??
  Ni bora ufunguae bahasha 1000 kuliko kufungua, kudownloa na kuzioma softcopy ya CV (ambazo zaidi ya 1000)
  Think.
   
 18. CtVKiLaZA

  CtVKiLaZA JF-Expert Member

  #18
  Nov 18, 2011
  Joined: Sep 13, 2011
  Messages: 305
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  naona ICT iko mbele yako. Tena umbali mrefu sana.
   
 19. Kwamex

  Kwamex JF-Expert Member

  #19
  Nov 18, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 378
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kiongozi usitukane wakunga na uzazi ungalipo.
   
 20. a

  ammablaze Member

  #20
  Feb 4, 2012
  Joined: Jan 27, 2012
  Messages: 35
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Shizukan , Ebwana tunashukuru kwa ufafanuzi, coz wengine tulishaanza kukata tamaa
   
Loading...