Zoom Tanzania na Brighter Monday zinatengeneza matangazo feki ya Ajira.

Kheri Hansen

JF-Expert Member
Jan 20, 2018
1,025
1,235
Nisipoteze muda kuandika sana au kuunda logic, swallow it or spit it.

Mitandao ya ajira hapa Tanzania, hasa Zoom Tanzania na Brighter Monday inalaghai watu/watafuta ajira kwa post za ajira mpya kila siku. Kumbe wanavitengo/watu maalumu wa kugenerate au kutengeneza post feki za nafasi za kazi.

Binafsi ni muhanga kwa miaka 4 mfululizo hadi nimekuja kuujua huu ukweli mchungu. coz ilibidi hadi nizitembelee hizo ofisi live na kuunda urafiki na wafanyakazi. Wanajinasibu kama Recruitment Agencies na kwamba wana nafasi ya ushawishi kwa Employers...ni uhuni na utapeli mtupu, na Email applications zozote wanazoziforwad kwa Employers zinaishia kwenye Junk au Spam boxes.

Wanajiingizia kipato kwa 'on-click ads', viewers per page na hot linking, yaani kadiri uanvyoenda kucheki post mpya za nafasi za kazi, ndio unawaingizia hela na sahau kuhusu ajira, utasubmit kila siku.

Mnaotafuta ajira kupitia mitandao hii chukueni tahadhari, bora bundle lenu mpoteze JF au LinkedIn.

OVA
 
Sio mara zote. My last two jobs nilipata kupitia zoom.
Ili usifall victim wa hicho unachokisema hakikisha una apply zile kazi ambazo Shirika/Office wameweka adress yao so uki apply unatuma application yako moja kwa moja kwa wahusika na sio middleman (recruiting agencies). Ukituma via middle man na wao hua wanazichambua hazifiki au unakuta wana previous applications for the similar post hivyo hizo zinapewa priority.
Kwa kifupi omba kazi ambayo mwajiri ameweka adress /link yake. Ukiona ile wameweka sijui apply here au on behalf of client achana nazo.
All the best
 
Hebu nisaidie hili hilo shirika wameamua applications zipitie Brighter Monday si ni lazima uitume huko?
 
Back
Top Bottom