Natumia simu mkuu wangu,acha maneno ya uzushi, tuma picha
Wakuu siku ya jana, mh Mwakyembe, amezuiliwa na wakazi wa Kyela kuingia stendi ya Kyela na kuzomewa na wakazi wa hapa wakidai aliwaahidi lami na hajatekeleza, toka juzi hakuna gari linaloingia stendi, natamani sana kuwatumia picha lakini nipo via mobile
Mwakyembe ni mtatanishi, si lolote si chochote.
Kwa hali ilivyo sasa hivi ndani ya CCM na ufahamu wa watu yakua wa CCM ni nani na nini?Hali hii itawakumba viongozi wengi wa CCM.CCM imevua ngozi ya kondoo sasa mambo yako wazi,na huu usanii wa kujivua magamba badala ya kuleta tija kwa CCM ndiyo unaitosa zaidi kwani watu wanashindwa kuelewa magamba ni yapi na kwa vile idadi kubwa ya viongozi wa CCM ni magamba kwa mtizamo halisi.Wananchi wanasubiri magamba ni yapi kwa mtazamo wa CCM,wakati CCM inaendelea kukaa kimya wananchi wana haki ya kumshuku kila kiongozi wa serikali ya CCM kwa sababu hawajui magamba ni yapi.Pili hata hao viongozi makini waliomo katika CCM ni vigumu kuwaamini kwa kukaakwao kimya miongoni mwa magamba na kujaribu kuturubuni kua wanachapa kazi.Jitihada zao nazifananisha na mtu anaejaribu kusukuma gari liende mbele akiwa amekaa ndani ya gari hilo wakati dereva wa gari hilo JK,amevuta breki ya mkono na kukanyaga breki ya mguu na utingo CCM kaweka kigingi.MUNGU IBARIKI TANZANIAKama Mwakyembe naye anazomewa sasa nani atabaki. Mbona maahadi yaliyomwagwa ni mengi mno, basi watazomewa wengi kwa kuwa sioni hizo ahadi zitatekelezwa japo nusu yake.
Kama kweli Mwakyembe amezomewa basi tatizo la CCM si ufisadi wa kuiba pesa za nchi tu bali na uongo pia. Ahadi za uongo ndizo zitakazoimaliza CCM 2015 si kingine.