Zoezi la Uhakiki Wanachama ADC laendelea vyema. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zoezi la Uhakiki Wanachama ADC laendelea vyema.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by hasan124, Jul 11, 2012.

 1. hasan124

  hasan124 JF-Expert Member

  #1
  Jul 11, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 716
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Lile zoezi la Uhakiki Wanachama kwa chama cha ADC linaendelea vyema na kwa mafanikio. Zoezi Hilo lilianza mkoani Tanga jumapili ya tar.08-07-2012 likifunguliwa rasmi na msajili WA vyama vya Siasa NCHINI MHE. John Tendwa na kusifia namna Uongozi WA ADC CHINI ya MHE. Said Miraji (m/kiti TAIFA) ulivyojipanga kukamilisha kazi hiyo.
  Tar. 10-07-2012 ILIKUWA Zamu ya mkoa WA Mwanza ambapo kwa mujibu WA televisheni ya TAIFA TBC1 zoezi Hilo lilikamilika vyema ambapo wanachama zaidi ya 1000 walijitokeza kutoka wilaya za Nyamagana, Ilemela na Magu hivyo kuvuka kwa mbaaaali idadi ya wanachama 200 inayohitajika na Ofisi za Msajili WA chama Kisheria. Hali iliyopelekea Muwakilishi WA Msajili Kanda ya Ziwa kusajili wanachama 240.
  Zoezi hili linaendelea tena tar. 12-07-2012 huko Mkoani Mara CHINI ya usimamizi WA Kamishna WA ADC MHE. Jumanne Magafu na Pemba Visiwani CHINI ya Kamishna Said Seif sehemu inayoaminika miaka mingi kuwa ni ngome ya kisiasa ya chama cha wananchi CUF (INAYOLEGALEGA) na kuthibitisha Hilo katika jimbo moja tu la Wawi ADC kuna wanachama zaidi ya 1000 ambao wako Tayari kwa Uhakiki huo.
  Baada ya Pemba tar. 14-07-2012 itakua ni zamu ya Unguja, na utaratibu huo utaendelea hadi hitimisho mnamo tar.17-08-2012 JiJiNi Dar ES Salaam hivyo kufanya mwanzo mwema wa ile safari inayosubiriwa na wananchi wengi WA Tanzania ya kupata chama Mbadala WA CCM chenye Madhumuni ya:
  1. Kushika dola kwa njia halali na za kidemokrasia.
  2. Kujenga Umoja na Mshikamano imara kwa WaTanzania wote.
  3. Kujenga Uchumi imara na kulinda raslimali za Nchi kwa manufaa ya WaTanzania wote.
  4. Kupiga kwa nguvu zote aina zote za Ubaguzi na Ukandamizaji.
  5. Kuheshimu mikataba ya kimataifa inayohusu haki halisi za binadamu.

  ADC - DIRA ya Mabadiliko.
   
 2. Baba V

  Baba V JF-Expert Member

  #2
  Jul 11, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 19,507
  Likes Received: 169
  Trophy Points: 160
  Vizuri kumbe mkistuliwa mnastuka eeh! good ALL THE BEST!
   
 3. hasan124

  hasan124 JF-Expert Member

  #3
  Jul 11, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 716
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Teh teh! Pombekali sisi bado hatuna usajili WA kudumu sasa hatuna sababu ya kupigizana kelele weeeee! Ilhali fitna nyingi Nchi hii.....kuna wasiotutakia heri Kama hawa Ndugu zetu WA CUF ambapo juzi tukiwa Tanga kwa Kazi hiihii ya Uhakiki NAo wakamleta kiongozi wao mmoja anaitwa Khamis Hassan afanye anayoweza kufanya, tuliligundua Hilo na kumaliza zoezi letu vyema. Kama ambavyo maJuzi walivyotuma vibaraka wao maeneo ya Tandale kwa Tumbo kwa Mwenyekiti WA Mtaa anayefahamika kwa jina Tamim Tamim eti wananchi waandamane kumpinga hawafai....kisa? Ni kundi moja na MHE. HAMAD Rashid Mohamed (Mbunge). Lakini pia hawakufanikiwa, Fikiria MTU kachaguliwa na wananchi zaidi ya 750 awe kiongozi wao ninyi mnampelekea wahuni 20 tu na mabango wamtoe? Haiwezekani. Matokeo yake wakajikuta wamemjenga Tamim kisiasa zaidi kwani walipeleka hadi waandishi WA habari WA televisheni ambapo alipopewa nafasi ya kujibu HOJA tu ikadhihirika kwamba hawakuwa wamejipanga vyema hao waliotuma na waliotumwa.
  Subiri tukamilishe zoezi letu la Uhakiki then uhoji ufanisi wetu.
  ADC - DIRA ha Mabadiliko.
   
 4. TECHMAN

  TECHMAN JF-Expert Member

  #4
  Jul 11, 2012
  Joined: May 20, 2011
  Messages: 2,677
  Likes Received: 162
  Trophy Points: 160
  Wadau hebu mnijuze hii ADC ndo kitu gani ?
   
 5. Mzalendo JR

  Mzalendo JR JF-Expert Member

  #5
  Jul 11, 2012
  Joined: Jun 6, 2012
  Messages: 1,188
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  mmhhhh Do u ril exist?
   
 6. hasan124

  hasan124 JF-Expert Member

  #6
  Jul 11, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 716
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Alliance for Democratic Change....slogan "Dira ya Mabadilko" "Tumaini la Mtanzania" . Hatujaja kubwabwaja tumekuja kutenda zaidi.
  Madhumuni ya chama ni Kama nilivyoainisha kwenye POST yangu ya Utangulizi hapo juu.

  Note: Need we Say more.
   
 7. hasan124

  hasan124 JF-Expert Member

  #7
  Jul 11, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 716
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33

  Not a matter of xisting though we Yet 2own media company like Uhuru and Tanzania Daima but soon you'll realise the power.
   
 8. M

  Mbalinga JF-Expert Member

  #8
  Jul 11, 2012
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 1,380
  Likes Received: 407
  Trophy Points: 180
  Taarifa ni kuwa professor wa ukweli, Mh Ibrahim Harun Lipumba atahutubia mkutano mkubwa wa hadhara Jangwani tarehe 15/7/2012.
   
 9. hasan124

  hasan124 JF-Expert Member

  #9
  Jul 11, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 716
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hakika ni professor WA ukweli haswaaaa, nami namkubali mno kwenye sector ya Uchumi lakini sio Siasa ndio Maana anazama na CUF......sio vibaya sana kwani soon atabaki kuwa MSHAURI WA masuala ya Uchumi tu na si Siasa.
   
Loading...