Shark
JF-Expert Member
- Jan 25, 2010
- 29,936
- 30,051
Wadau za Wikiend,
Leo Jumapili asubuhi hii nimemsikiliza Afisa wa Elimu kwa Mlipa Kodi wa TRA Bwana Isihaq Shariff akihojiwa na mtangazaji wa TV1 Ndg. Mukhsin Mambo amesema kua lengo la uhakiki wa TIN ni kwa ajili ya Watanzania WOTE wenye hizi TIN bila kujali kua wanazitumia kwa ajili ya gani. Ameelezea kua wanaohitajika kuhakiki ni wale wenye TIN za Biashara na zisizo za Biashara.
Nimefikiria kuhusu hii issue naona kama TRA kama vile wameshindwa kupanga, hivyo wanapanga kushindwa. Maana kuna kundi kubwa la watu wana hizi TIN lakini hawajijui kama wanailiki TIN. Hawa ni MADEREVA. Dereva yoyote mwenye Valid Driving License basi lazima atakua anamiliki TIN atake asitake. Lakini ni Dereva gani mwenye TIN ambae alishawahi kupewa Certificate yake wakati anapewa Driving License yake?? Je pale kwenye Dirisha au Dawati la TRA wanapotoa Driving Licence hua wanaambia madereva kua wao madereva ni wamiliki pia wa TIN ya TRA??
TIN hii kwa madereva hua haiandikwi kwenye Driving License ile kadi, bali pale mwanzo wakati anakata kwa mara ya kwanza na labda akapewa ile Temporary License ya karatasi ndio ataiona hiyo namba, je ni Dereva gani Mzoefu ambae anayo ile Temporary aliyopewa mara ya kwanza na bado anaitunza mpaka leo anaitunza?? Hata kama atakua anaitunza je anaweza kua anajua kama na yeye anahitajika kujihakiki na ile namba ndio inahusika?? Kwa elimu ipi iliyotolewa??
Idadi ya madereva au wamiliki wa Driving License ni kubwa sana, hasa tukiangalia magari yanayopita barabarani na kuweka foleni kuanzia asubuhi mpaka usiku ni ishara kua waendeshaji wa hayo magari wana valid Driving License (assumption) na wako wengi, je ni wote wanajua kwamba Leseni zao zina TIN hivyo wanahitaji kujihakiki??
Na ikitokea Madereva wengi wasijihakiki kutokana na kutokujua na hivyo kupelekea kufutwa kwa TIN zao kwenye system, TRA na serikali hawaoni kwamba wakati wa Ku-Renew hizo leseni itakua mvurugano mkubwa sana??
Mi nadhani TRA na serikali inabidi itoe ufafanuzi kua uhakiki wa hizi TIN unahusisha pia watu wote WENYE LESENI ZOZOTE ZA UDEREVA ili kuweza kupata idadi kamili ni wangapi wenye hizi TIN, otherwise iseme tu kua inahitaji TIN zile za Biashara tu ndio zihakikiwe. Lasivyo basi watakua wameshindwa kupanga, hivyo wanapanga kushindwa...!!!!