Zoezi la Uhakiki wa TIN, Katika hili TRA itafeli

Zoezi la Uhakiki wa TIN, Katika hili TRA itafeli

Ya ni kweli kiongozi... tra kwa kukurupuka ndo wenyewe...

Kusema ukweli ni kwamba uongozi wa TRA una walakini ukiangalia kwenye mambo mengi wanaifanya kazi ya upatikanaji wa mapato ya serikali kuwa mgumu wenye kuighalimu serikali fedha nyingi kutokana na ukosefu wa ubunifu, chukua mifano midogo kabisa:
  • Zoezi lao la ubadilishaji wa namba za pikipiki na bajaji kutoka T 000 XXX kwenda MC 000 XXX wamefanikiwa kwa kiasi gani? mbona hawajitokezi kwenye vyombo vya habari kutangaza kuwa zoezi hilo limefanikiwa kwa 100%? kwanini hizo TIN zisihakikiwe wakati wa ku-renew hizo leseni badala ya kuanza kuwavuruga watu,
  • Hivi utaamini hadi leo hii kuna baadhi ya maeneo hapa nchini yapo magari yanatumia reg numbers z TZ na yanafanya kazi kwa mida maalumu,
  • Hivi kwa mtazamo wa wazi kabisa, ukusanyaji wa mapato ya road licence ni rahisi kwa njia ya kukimbizana na watumiaji wa barabara njiani kuliko kutoza kwenye mafuta ambako kila chombo cha moto kinalipia tozo automatikally
Personally ningeishauri serikali kutazama upya utendaji kazi wa hii mamlaka, inapenda kufanya kazi kwa kutumia mechanical approach badala ya njia rahisi zenye ufanisi, unless watuambie kuwa through hizo traditional methods maafisa wananufaika kimtindomtindo.
 
Nchi hii kila kitu ni kukurupuka tu.

Walichotakiwa kufanya ni: -

1. Uhakiki ufanyike wakati wowote au pale mteja anapokwenda kupata huduma husika.

2. Kuwe na tin ya aina moja tu, sio udereva wala biashara

3. Uhakiki ufanyike kwa njia ya mtandao.
Ili na mtandaoni nadhani lingekuwa rahisi zaidi
 
Tin yangu nilikatiwa tanga na sasa niko uhamishoni mwanza. Biashara tanga inaendelea na nimekuwa nalipa kodi nikiwa huku mwanza. Sasa natakiwa niende Tanga nikahakikiwe. Nani atanilipia hiyo nauli au tutakatana kwenye mapato? TRA hawana upeo hata kidogo wanajiwaza wao tu. Addresdls za makazi za nini wakati tunahamahama. Sasa mwanza nimefungua biashara. Anwani yangu au plot namba yangu ni ipi na mimi ni mpangaji na nikistaafu narudi kwetu mbeya?
 
Mkuu na mie nainshu kama yako TIN yangu niliikatia kilimanjaro biashara zangu zipo Dar na Shinyanga mie mwenyewe nipo kigoma na huku nategemea kufungua biashara soon
Makazi yangu kwa sasa ni kahama na kilimanjaro nishahamishwa kabisa sitegemei kurudi na nikienda ni kwa ajili ya kulipia mapato tu Sasa kama wanaandika anuani za makazi mie nitastahili mkoa wangu wa kodi kuwa kilimanjaro kweli
Maana anuani ya makazi kwa sasa ni tofauti na hapo awali
 
Ukichukua TIN hua unasema unaenda kuifanyia nini, na pia hua unaweka details zako kua wewe ni mkazi wa wapi.
Sasa inawezekana umehama, matumizi ya TIN yamebadilika au hata umefariki. So wanataka kubaki na valid and updated TINs
Na TIN za biashara ambao quarterly wanakwenda kulipa kodi unahakiki nini? Kama kuna swali si aulizwe akienda kulipa kodi? Hapa kuna kitu hakiko sawa
 
Wadau za Wikiend,

Leo Jumapili asubuhi hii nimemsikiliza Afisa wa Elimu kwa Mlipa Kodi wa TRA Bwana Isihaq Shariff akihojiwa na mtangazaji wa TV1 Ndg. Mukhsin Mambo amesema kua lengo la uhakiki wa TIN ni kwa ajili ya Watanzania WOTE wenye hizi TIN bila kujali kua wanazitumia kwa ajili ya gani. Ameelezea kua wanaohitajika kuhakiki ni wale wenye TIN za Biashara na zisizo za Biashara.

Nimefikiria kuhusu hii issue naona kama TRA kama vile wameshindwa kupanga, hivyo wanapanga kushindwa. Maana kuna kundi kubwa la watu wana hizi TIN lakini hawajijui kama wanailiki TIN. Hawa ni MADEREVA. Dereva yoyote mwenye Valid Driving License basi lazima atakua anamiliki TIN atake asitake. Lakini ni Dereva gani mwenye TIN ambae alishawahi kupewa Certificate yake wakati anapewa Driving License yake?? Je pale kwenye Dirisha au Dawati la TRA wanapotoa Driving Licence hua wanaambia madereva kua wao madereva ni wamiliki pia wa TIN ya TRA??

TIN hii kwa madereva hua haiandikwi kwenye Driving License ile kadi, bali pale mwanzo wakati anakata kwa mara ya kwanza na labda akapewa ile Temporary License ya karatasi ndio ataiona hiyo namba, je ni Dereva gani Mzoefu ambae anayo ile Temporary aliyopewa mara ya kwanza na bado anaitunza mpaka leo anaitunza?? Hata kama atakua anaitunza je anaweza kua anajua kama na yeye anahitajika kujihakiki na ile namba ndio inahusika?? Kwa elimu ipi iliyotolewa??

Idadi ya madereva au wamiliki wa Driving License ni kubwa sana, hasa tukiangalia magari yanayopita barabarani na kuweka foleni kuanzia asubuhi mpaka usiku ni ishara kua waendeshaji wa hayo magari wana valid Driving License (assumption) na wako wengi, je ni wote wanajua kwamba Leseni zao zina TIN hivyo wanahitaji kujihakiki??

Na ikitokea Madereva wengi wasijihakiki kutokana na kutokujua na hivyo kupelekea kufutwa kwa TIN zao kwenye system, TRA na serikali hawaoni kwamba wakati wa Ku-Renew hizo leseni itakua mvurugano mkubwa sana??

Mi nadhani TRA na serikali inabidi itoe ufafanuzi kua uhakiki wa hizi TIN unahusisha pia watu wote WENYE LESENI ZOZOTE ZA UDEREVA ili kuweza kupata idadi kamili ni wangapi wenye hizi TIN, otherwise iseme tu kua inahitaji TIN zile za Biashara tu ndio zihakikiwe. Lasivyo basi watakua wameshindwa kupanga, hivyo wanapanga kushindwa...!!!!
Umejaribu kufafanua kwa kirefu kuhusu hili ila jambo la kushangaza umewalenga madriver bila kufanya research ambacho ninaweza kukuambia madriver wengi hasa wanaotumia leseni zao kama ndio njia ya ajira,
Na hao ndio wengi huko kwenye ofisi za uhakika wa tin kuliko hata hao wafanya biashara.
 
Mkuu,
Simaanishi hao madereva unaowasema wewe wenye kutumia Udereva kama ajira, ingawa nina uhakika nao wapo kwenye mkubo huu.
Ninao wazungumzia mimi mfano kama uko Dar es Salaa tafuta kiti/kigoda kaa pale Morocco traffic light upande wa Ghorofa za NHC zinapojengwa, anza kuhesabu Porte, Passo, Vitz, IST, ISIS, Rav4, Xtrail, Altezza, Carina, etc za watu binafsi zinazopita pale kuelekea na/au kutoka Mjini. Hawa wengi wao wanachojua ni ku-renew tu Driving Licence iki expire, hawajui au hawakubuki kama wao ni wamiliki wa TIN na hata ukiwaambia kwenye kadi ya gari wakuonyeshe TIN inakaa wapi hawatokuambia,

Maombi ya TIN ili kusajili gari zao TRA walimuachia kazi hiyo Clearing Agent kwa ujira wa Tshs 20,000/= na pengine walipewa namba tu, au certificate kama kweli ipo basi imefungiwa kwenye file la gari kabatini pengine wanadhani ni mmojawapo ya import procedure.

Otherwise kama wana TIN za udereva basi nazo zilipatikana kiagumashi na so long as wao ni waajiriwa, wanachojua wao mambo ya TIN ni ya wafanyabiashara, sio wao. Hawa wako wengi sana na ndio naowazungumzia
 
Bado napingana na wewe pia kwenye hilo sio wengi kwa kiasi unachokisema kwa maana ya wengi wanatumia tin namba yao ya gari mpk kwenye leseni na wengi pia wanatumia hiyo hiyo ya biashara kwa leseni
 
Bado napingana na wewe pia kwenye hilo sio wengi kwa kiasi unachokisema kwa maana ya wengi wanatumia tin namba yao ya gari mpk kwenye leseni na wengi pia wanatumia hiyo hiyo ya biashara kwa leseni
Mkuu fanya reseach yako mwenyewe kwa kuwauliza washkaj zako wanaoendesha magari binafsi kama wanajua TIN
 
Back
Top Bottom