zoezi la sensa aibu tupu!

nkisumuno

JF-Expert Member
May 22, 2012
208
72
Tangu jana huku Iringa zoezi la kuhesabu watu limesimama kutokana na ukosefu wa madodoso marefu. pamoja na serikali kujitapa kuwa vifaa vipo. wananchi wamehamasishwa na kuhamasika tatizo liko kwa serikali. vifaa havipo na sasa tumepata taarifa kuwa wanapiga fotokopi japo madodoso tuliambiwa yangesomwa na computer.

Maswali yangu ni haya:

Je sensa imekuwa ya dharura?

Je makarani wataongezewa muda na pesa baada ya muda uliopangwa kuisha?

Ni nani amekwamisha vifaa visifike mapema?

Hiiserikali ni nini inachoweza kukifanya kwa ufanisi pasipo manung'uniko?

sensa ni kila baada ya miaka kumi je iweje leo ionekane ni kitu cha dharura?

Kweli Serikali hii ya CCM hakuna dawa naamini wamegawanahela matokeo yake ndo haya hakuna pesa, vifaa.

Hata hawa waliofungwa waachiwe kwani hata wangekuwepo wasingehesabiwa maana vifaa havipo. waacheni hao mnawaonea bure.
 
Sensa na Mradi wa Vitambulisho vya Taifa ni another EPA, Richmond kwa vibosile wa serikali ya CCM. Hakuna hata jambo moja serikali ya CCM ilifanya/italifanya bira kuwa na kasoro zaidi ya 50%. Hii ni darili tosha kuwa CCM ni chanzo cha Umasikini wa wananchi na Nchi yetu.
2015 tujitokeze kwa wingi kutokomeza ADUI CCM
 
...Jamani, mbona hawa makarani hawajaja nyumbani kwangu wala mtaani kwangu wakati ktk mtaa wangu una kaya zaid ya 300 na leo ndo mwisho!?
 
Haka ka~nchi ni kaulaji kweli wewe subiri utasikia maelezo yatakayotolewa na NBS, (wataongeza muda ili wajilipe posho) la kushangaza tumeambiwa sensa hii imeandaliwa tangu 2002 na imeigarimu serikali 141 millioni (kama sijakosea).
 
Hata huku mkoani geita hasa wilayani mbogwe na bukombe ni uhuni mtu!,hata mabegi ya kubebea madodoso wanachangia watu wawili beg moja,muda umeisha madodoso hakuna,pesa zimeisha then tunaambiwa NIDA ITAFATIA,nan wa kutulipa Za nida?Uhuni mtupu!.Fulana za ccm kwenye kampeni hutapakaa hadi mashambani kwa kila baada ya miaka 5 ya uchaguzi,leo hii sare za sensa kwa miaka 10 tena kwa makarani hazipo,je inamaana kwamba chama cha mapinduzi kina pesa na ni cha maana kulko serikali yenyewe?Huu ni uhuni na uzembe wa hali wa juu.Tz bila ccm inawezekana timiza wajbu wako
 
Iringa ipi mkuu. Manispaa au IDC?
Tangu jana huku Iringa zoezi la kuhesabu watu limesimama kutokana na ukosefu wa madodoso marefu. pamoja na serikali kujitapa kuwa vifaa vipo. wananchi wamehamasishwa na kuhamasika tatizo liko kwa serikali. vifaa havipo na sasa tumepata taarifa kuwa wanapiga fotokopi japo madodoso tuliambiwa yangesomwa na computer.

Maswali yangu ni haya:

Je sensa imekuwa ya dharura?

Je makarani wataongezewa muda na pesa baada ya muda uliopangwa kuisha?

Ni nani amekwamisha vifaa visifike mapema?

Hiiserikali ni nini inachoweza kukifanya kwa ufanisi pasipo manung'uniko?

sensa ni kila baada ya miaka kumi je iweje leo ionekane ni kitu cha dharura?

Kweli Serikali hii ya CCM hakuna dawa naamini wamegawanahela matokeo yake ndo haya hakuna pesa, vifaa.

Hata hawa waliofungwa waachiwe kwani hata wangekuwepo wasingehesabiwa maana vifaa havipo. waacheni hao mnawaonea bure.
 
Haka ka~nchi ni kaulaji kweli wewe subiri utasikia maelezo yatakayotolewa na NBS, (wataongeza muda ili wajilipe posho) la kushangaza tumeambiwa sensa hii imeandaliwa tangu 2002 na imeigarimu serikali 141 millioni (kama sijakosea).

weka bilioni badala ya milioni utakuwa hujakosea
 
Mbona kwenye taarifa ya serikali kwenye vyombo vya habari inasema Zoezi la sensa linaendelea vizuri pamoja na changamoto ndogondogo? Tunaomba chombo huru kitakachofanya tathmini ya zoezi la sensa, vinginevyo tutadanganywa!
 
...Jamani, mbona hawa makarani hawajaja nyumbani kwangu wala mtaani kwangu wakati ktk mtaa wangu una kaya zaid ya 300 na leo ndo mwisho!?

waje kufanya nini si unaambiwa kuna walio vuta mshiko wakasepa....hata wakifika maswali yao ni kama maigizo eti unacheti cha kuzaliwa ,umri wako na kisomo kiasi gani.
hayo ndio matatizo ya kuchakachuwa kura utawala hauko kabisa japo walijichaguwa viongozi

Back
Top Bottom