Dodoso za sensa, shiriki kikamilifu kwa maendeleo ya nchi yetu

Rashda Zunde

Senior Member
May 28, 2022
199
231
Ndugu zangu naomba niwataarifu kuwa Sensa ya Watu na Makazi 2022 itahusisha madodoso manne:
1: Dodoso la Jamii
2: Dodoso la Sensa ya Watu na Makazi
3: Dodoso la Makundi Maalum
4: Dodoso la Majengo

1. Dodoso la Jamii litaanza kwa kumuhoji mwenyekiti au mjumbe wa kitongoji au mtaa juu ya uwepo wa huduma za kijamii ktk eneo lake. Kama zipo basi karani atambatana na kiongozi wa kitongoji au mtaa kwenda kwa mkuu wa taasisi husika kwenda kumuhoji mambo anuai yahusuyo huduma hiyo. Huduma za kijamii ni kama vile soko, maeneo ya huduma za afya, elimu, mitandao ya mawasiliano na taasisi za dini kwa maana ya misikiti na makanisa. Pia litahoji vitu kama mabadiliko ya tabianchi, matukio mbalimbali katika eneo husika n.k.

Dodoso la jamii litahojiwa siku 2 kabla ya siku ya sensa. Yaani litaanza kuhojiwa tarehe 21 hadi 22 Agosti 2022.

2. Dodoso la Makundi Maalum
Katika kuhakikisha kila mtu anahesabiwa na anahesabiwa mara moja tu basi hata watoto wa mitaani ambao hawana makazi, wasafiri ambao walilala stendi, makambi ya wavuvi na wachoma mkaa n.k. wote watahesabiwa kwa kutumia Dodoso la makundi maalum. Makundi haya yatajumuisha pia Askari wetu ambao siku ya sensa itawakuta wakiwa wanalinda mipaka ya nchi yetu. Makarani watakuwepo maeneo ya makundi maalumu saa sita usiku. Yaani, Dodoso hili litaanza kuhojiwa saa sita usiku wa tarehe 23/08/2022.

3. Dodoso la Sensa ya Watu na Makazi

Hili linaitwa Dodoso kuu. Linakadiriwa kuwa na maswali 100. Ni mengi lakini hayachoshi maana ni mahojiano ya ana kwa ana (face - to - interview).
Dodoso hili litahojiwa kwa kila kaya.

Hapa naomba nifafanue maana ya kaya. Kaya ni mtu au watu ambao huwa wanaishi pamoja na kula pamoja. Kaya sio sawa na familia. Familia huwa ni ya watu wenye undugu, lakini kaya inajumuisha watu wote wanaoishi na kula pamoja hata kama hawana undungu.

Kwenye Dodoso la Sensa ya Watu na Makazi ndipo pana swala la kuhesabu watu waliolala kwenye kaya siku ya kuamkia siku ya Sensa (23/08/2022).

Nani ahesabiwe na nani asihesabiwe?

Nani ahesabiwe?
Kila aliyelala na kuamkia siku ya sensa tarehe 23 Agosti 2022 ndani ya mipaka ya Tanzania. Hii haijalishi uraia wake, ilimradi tu amelala na kuamkia nchini Tanzania.

Hapa ifahamike kuwa uhesabuji utaanza saa sita kamili usiku, tarehe tarehe 23/08/2022. Hivyo chukulia kama picha inapigwa muda huo kuchukua sura za binadamu walio hai. Hivyo kila binadamu aliye hai atakayetokea kwenye picha hiyo ndio atahesabiwa. Hapa sasa inakuja hoja tunazotakiwa kuzikumbuka.

Je, tutahesabu mtoto aliye tumboni. *Hapana maana kwenye picha hataonekana.

Je tutahesabu maiti ya aliyefariki saa tano na dakika 59 usiku? *Hapana hatuta mwesabu.
Lakini mtoto aliyezaliwa saa tano na dakika 59 atahesabiwa.

Mtoto aliyezaliwa saa sita na dakika moja hapaswi kuhesabiwa maana amezaliwa baada ya saa sita usiku.

Mtu aliyefariki saa sita na dakika moja anapaswa kuhesabiwa maana amefariki baada ya saa sita usiku tarehe 23.

Kwa hiyo Wasiotakiwa kuhesabiwa ni kama hao niloanza kuwataja watoto waliozaliwa baada ya saa sita na waliokufa kabla ya saa sita. Na wote ambao hawakuwa nchini usiku wa kuamkia siku ya Sensa.

4. Dodoso la Majengo
Hili ni dodoso la mwisho katika mfululizo na ni la mwisho kuhojiwa baada ya dodoso la SENSA ya Watu na Makazi. Hapa serikali inataka kujua tu takwimu za majengo na hali ya umiliki pamoja na thamani ya jengo SI kwa madhumuni ya kuuza hapana. Bali kwa ajili uandaaji wa kanzi data na Mambo mengine yahusuyo Sera.

Sensa ya mwaka huu ni ya kidijitali. Inapokea na kuchambua taarifa Kwa haraka kupitia mfumo wa kompyuta. Hivyo tuwe tayari kuhesabiwa.

Wengine watasema watakuwa kwenye majuku yao. Tujitahidi kuwaeleza kuwa wsiache kufanya kazi zao bali tuwaambie kuwa, Wahakikishe wanaaacha majina matatu, taarifa za tarehe za kuzaliwa taarifa za hali ya ndoa, elimu paomoja na uhamaji wa watu wote walioamkia kwenye kaya zao siku kuamkia siku ya sensa.
 
A
Ndugu zangu naomba niwataarifu kuwa Sensa ya Watu na Makazi 2022 itahusisha madodoso manne:
1: Dodoso la Jamii
2: Dodoso la Sensa ya Watu na Makazi
3: Dodoso la Makundi Maalum
4: Dodoso la Majengo
Asante kwa maelezo mafupi yaliyoeleweka. Tujiandae Kuhesabiwa.
 
A
Ndugu zangu naomba niwataarifu kuwa Sensa ya Watu na Makazi 2022 itahusisha madodoso manne:
1: Dodoso la Jamii
2: Dodoso la Sensa ya Watu na Makazi
3: Dodoso la Makundi Maalum
4: Dodoso la Majengo
Asante kwa maelezo mafupi yaliyoeleweka. Tujiandae Kuhesabiwa.
 
Ndio maana serikali inasisitiza watu washiriki kikalifu ili makarani wapate data sahihi.
Walio pata Elimu ni makarani wanao hesabiwa ni raia ambao inawezekana bado hawajapata Elimu sahihi ya sensa

Kuna mahitaji selikari ilihitaji kuyaanda mapema kabla ya zoezi husika

Watu wanamashaka na maswali husika kulingana na mifumo ya uendeshwaji wa selikari zetu usio tabirika

Watu wanaona baadhi ya maswali yanalenga kuwaongezea mzigo wa tozo na maisha kuwa magumu zaidi

Kunahitajika ufafanuzi wa uhakika kaajiri ya kuondoa mkanganyiko
 
Wito wangu serikali iwaongeze posho makarani kazi yao ni ngumu sana.
 
3. Dodoso la Sensa ya Watu na Makazi. Hili linaitwa Dodoso kuu. Linakadiriwa kuwa na maswali 100. Ni mengi lakini hayachoshi maana ni mahojiano ya ana kwa ana (face - to - interview).
Dodoso hili litahojiwa kwa kila kaya.
Maswali 100 yasichoshe?! Acha mzaha.
 
100 qn wengi watakimbiwa na wahesabiwaji, mi wanikute asubuhi kabla sijatoka kwenda kwa mangi 🍻🍺
 
4.Dodoso la Majengo. Hili ni dodoso la mwisho katika mfululizo na ni la mwisho kuhojiwa baada ya dodoso la SENSA ya Watu na Makazi. Hapa serikali inataka kujua tu takwimu za majengo na hali ya umiliki pamoja na thamani ya jengo SI kwa madhumuni ya kuuza hapana. Bali kwa ajili uandaaji wa kanzi data na Mambo mengine yahusuyo Sera.
... tozo ingine on the making! Mambo yahusuyo sera yameonekana kwenye majengo tu na sio maeneo mengine kama makaburi, n.k?
 
Ni watu wangapi wanaojishughulisha na Kilimo? Ni watu wangapi wanaohitaji mbolea ya Ruzuku? Ni mtu mwenye takwimu pekee anayeweza kujibu maswali haya muhimu kwaajili ya mipango ya kimaendeleo.

Siku ya tatu sasa, baada ya zoezi la Kitaifa la Sensa ya watu na makazi kuanza rasmi na mfano kutolewa na Rais wetu Mh. Samia Suluhu Hassan. Sensa ni suala la kitaifa lenye manufaa mengi kwa wananchi kama vile;

1. Kuiwezesha serikali kupanga mipango mbalimbali ya kimaendeleo kwa kuzingatia idadi halisi ya wananchi.

2. Kuiwezesha serikali kutambua makundi maalum na kaya zenye mahitaji maalum ili ziweze kusaidiwa kwa weledi.

3. Kuiwezesha serikali kuwa na mipango endelevu kutokana na kuweza kuwa na taarifa zenye uwezo wa
kutambua ongezeko la watu kwa muda wa miaka ijayo.

4. Kuiwezesha serikali kuwa na takwimu muhimu kwaajili ya uwekezaji na biashara katika maeneo mbalimbali ya nchi.

5. Kuiwezesha serikali kutambua changamoto mbalimbali za wananchi kama vile uhitaji wa makazi mapya na huduma za kijamii.

Ni jukumu la kila mwananchi kushiriki kikamilifu katika zoezi hili muhimu linaloendelea nchi nzima. Shime tushikamane kuhakikisha zoezi hili linafanikiwa kwa zaidi ya asilimia mia moja.
 
Back
Top Bottom