Zoezi la BVR Ilala maandalizi yake utata mtupu

kyalankota

JF-Expert Member
Joined
Jul 27, 2014
Posts
2,594
Reaction score
1,463
Zoezi la uandikishaji wa wapiga kura kwa njia ya teknolojia ya kisasa ya BVR kwa Wilaya ya Ilala limeanza na dosari kwa sintofamu ya majina ya waliochaguliwa kama BVR Kit Operators na waandishi wasaidizi baada ya usaili kuwa na usiri mkubwa wa namna ya kuyaona ili wahusika wajue wamepangwa kata gani kwa ajili ya zoezi litakaloanza tarehe 16 july wiki ijayo!

Wilaya zingine za Kinondoni na Temeke tayari wameshabandika kwenye Kata zao na tarehe za kufanya semina kwa ajili ya maelekezo namna ya uandikishaji imeshapangwa kuwa ni tarehe 13 na 14 wiki ijayo.

Inasemekana kuna namna inafanyika kimyakimya kuwapa taarifa wale wanaohitajika kwa lengo maalum kwa ajili ya maslahi ya watu fulani.

Sasa hii ni hatari.
 
  • Thanks
Reactions: jme
Hii ni kweli kabisa kuna njama zinaendelea chini kwa chini. Mfano kata ya segerea ambayo ipo ndani ya ilala haijabandika majina hadi sasa. Ukiwauliza wanakwambia usiku tembelea ilala blogu kutawekwa majina!

Hata hiyo ilala blogu sio wote wanaoifahamu! Taifa hili lina watu wengi wenye njaa sana kiasi kwamba kila kitu kinafanyika kwa ubabaishaji usio na tija!
 
Hii nchi hakika ni ya maghumashi sana!
Binafsi nimeshakata tamaa na huenda nikashindwa kupiga kura japo naendelea kufanya kila liwezekanalo haya yasitokee.
Kilichonifariji ni jana kwenye mdahalo pale msemaji mmoja alipotanabaisha kuwa wazee wanaoongozwa na Mzee Warioba watakumbukwa na kuenziwa na vizazi vya Watanzania huku kundi lingine linaloongozwa na Mzee Lubuva litalaaniwa na vizazi vyao.

Hii ni kweli kabisa kuna njama zinaendelea chini kwa chini. Mfano kata ya segerea ambayo ipo ndani ya ilala haijabandika majina hadi sasa. Ukiwauliza wanakwambia usiku tembelea ilala blogu kutawekwa majina!

Hata hiyo ilala blogu sio wote wanaoifahamu! Taifa hili lina watu wengi wenye njaa sana kiasi kwamba kila kitu kinafanyika kwa ubabaishaji usio na tija!
Hiyo blog ya Ilala pia hakuna kitu na wanampango wasiweke huko ili mambo wafanye wanavyojua wao.
 
Mimi nisipochaguliwa kuwa BVR Operator, nitahakikisha hadi mwisho ninajiridhisha kuwa wote waliochaguliwa wananizidi kwa vigezo. Kwa kuanzia tu, ninayo matokeo ya watu wote tuliofanya mtihani wa practical uliofanyika pale DIT, na kwa bahati nzuri nilipata 100%. Kukitokea zengwe lolote nitakinukisha na lazima mtu aondoke
 
Mkuu ni PM na mimi matokeo...tuunganishe nguvu hawa watu bana!
 
utaratibu wao n mbovu..ndo maana wameshindwa kutoa mapema.majibu ya usaili

Binafsi nimeshakata tamaa na huenda nikashindwa kupiga kura japo naendelea kufanya kila liwezekanalo haya yasitokee.
Kilichonifariji ni jana kwenye mdahalo pale msemaji mmoja alipotanabaisha kuwa wazee wanaoongozwa na Mzee Warioba watakumbukwa na kuenziwa na vizazi vya Watanzania huku kundi lingine linaloongozwa na Mzee Lubuva litalaaniwa na vizazi vyao.

Nimefanya intelijensia yangu nimeshagundua na nimebaini kuwa majina tayari yapo kwa watendaji kata sababu ya kutobandika haijafahamika inawezekana ni kwa maelekezo maalum kwa malengo maalum ya watu fulani. Na haifahamiki kama watabandika au la.

Cha kufanya kama ni mmoja wao au ndugu yako mwambie aende kwa mtendaji kata akomae naye majina yapo wanatembea nayo. Fanya hima wajulishe na wengine.
 
Hawa wanataka rushwa hvoo yaani was ajabu Sana'a hawaridhikii na wwalchopataa.. Wanataka watuchakachue hawaa
 
Wakuu mwenye habari yoyote kuhusu semina ya bvr kit operators kwa manispaa ya ilala?
 
Back
Top Bottom