Ziwa Victoria linapigania uhai wake

Wickama

Platinum Member
Joined
Mar 8, 2009
Posts
1,577
Reaction score
1,365
Wanajamvi, Ziwa Victoria ndilo ziwa kubwa kuliko yote hapa barani Africa. Theluthi moja ya wakazi wa nchi za Kenya Uganda na Tanzania wanaishi kulizunguka na kuendesha maisha kutokana na ziwa hili. Lakini hivi kwa sasa ziwa hili linapigania uhai wake. Tatizo ni magugu maji. Japokuwa hivi karibuni kumeelezwa kuwa serikali zetu zinajitahidi kuyaangamiza (Hatua zatakiwa kuchukuliwa kulinusuru ziwa Victoria - china radio international) hali niliyoishuhudia kwenye pwani ya jiji la Kisumu inatia wasiwasi. Sijui katika nchi zingine hali iko vipi. Hapa nabandika picha nilizopiga nikiwa juu ya eneo husika ili tuchangie mawazo:

1. Haya magugu yapo ndani ya ziwa kama kilometer 3 toka jiji la Kisumu

​
2. Hapa ni jirani na kiwanja cha ndege cha Kisumu, mahali hapo kuna uoshaji wa magari kwa wingi na vibanda vingi vya kina mama lishe. Kwa sasa hakupitiki ila sehemu ndogo inayoonekana

​
3. Eneo unaloliona kijani lote limeathirika na magugu

​

My take: Hili ziwa linahitaji serious efforts kulinusuru vinginevyo maisha ya wakazi wanaolizunguka na hata ekolojia yake itaharibika sana. Wakati wa kuwa tegemezi na misaada ya nje ili kulinusru nadhani umepita, umefika wakati juhudi zetu wenyewe East Africa zilinusuru ziwa letu.

Where did we go wrong?
 
Shukran kwa taarifa mkuu. Mikakati ya nguvu inatakikana hapa baina ya hizi serikali tatu otherwise maisha ya wavuvi
katika maeneo yalopakana na hili ziwa yatakua taabu bin balaa!

Shukran kwa taarifa mkuu. Mikakati ya nguvu inatakikana hapa baina ya hizi serikali tatu otherwise maisha ya wavuvi
katika maeneo yalopakana na hili ziwa yatakua taabu bin balaa!

Hivi hayo magugu maji hayawezi kutumika kama malighafi ya kutengenezea bidhaa zozote au kutumika kama malisho kwa wanyama? Tunahangaika na mapigano ya wafugaji na wakulima huenda hayo madude ni malisho swaafi kabisa kwa 'vitoweo'.
 
Kuna jamaa alikua na mpango wa kuanzisha bio-gas na haya magugu na sijui iliishia vipi tena. Unajua serikali
zetu kama hamna ulaji basi ujue hapatofualiwa kitu hapo.

God save us!
 
Watu Lake Victoria Environmental Management Project wana kazi gani??
 
cha muhimu ni kuangalia, wakenya eneo lao la ziwa ni dogo sana, mipaka yetu ikae vilevile, lisije ziwa likawa linaisha upande wao wao wakawa wanasogea kwenye ziwa upande wa tz. TPDF wawe makini kama ziwa lao hawatalisafisha litaisha lote. kwa tz na uganda magugu maji yapo lakini eneo letu bado kubwa sana sio sawa na kenya.
 
Misri na Sudan wako katika honeymoon nini? Waje kuyatoa hayo magugu maji vinginevyo no lake victoria no Nile no Egypt.

Mpeni taarifa Mh.Membe awapelekee hao jamaa anaowapigania.
 
Hivi hayo magugu maji hayawezi kutumika kama malighafi ya kutengenezea bidhaa zozote au kutumika kama malisho kwa wanyama? Tunahangaika na mapigano ya wafugaji na wakulima huenda hayo madude ni malisho swaafi kabisa kwa 'vitoweo'.
MPUNGA, Kwa kweli navyoelewa, kwa upande wa Uganda kulikuwa na juhudi za kuyavuna (physically) na kuyatumia haya magugu kama mali ghafi ya baadhi ya vitu kama mikeka na kama namna hiyo (kwa watu binafsi) lakini miaka ya hivi karibuni hata hizo juhudi hazisikiki tena. Na hata wao bado wanalia na tatizo hili National Geographic's Strange Days on Planet Earth . Invaders . Lake Victoria's Water Hyacynth Problem | PBS sielelewi kwa upande wa Tz na Kenya juhudi zimefikia wapi
 
Last edited by a moderator:
Watu Lake Victoria Environmental Management Project wana kazi gani??

Mkuu hao LVEMP II ni mtambo Wa kula fedha za wafadhili tu hakuna la maana linalofanyija! Miradi yote inayopitia serikalini huwa ni ulaji fedha za wafadhili tu! Jamaa wanaofanya kwenye huo mradi wanashindana kujenga mahekalu tu na kuopoa mabibi walonona kama kina charminglady! kazi tunayo kwa kweli. Pia kuna kitu kinaitwa ECOVIC Wote hawa wanahusika na uendelezaji Wa ziwa Victoria lakini hatuoni chochote!
 
Hivi hayo magugu maji hayawezi kutumika kama malighafi ya kutengenezea bidhaa zozote au kutumika kama malisho kwa wanyama? Tunahangaika na mapigano ya wafugaji na wakulima huenda hayo madude ni malisho swaafi kabisa kwa 'vitoweo'.
Ni chakula safi kwa nguruwe. Vijana wanaolia ajira kila siku wasaidiwe na serikali kuanzisha miradi ya ufugaji pembezoni mwa ziwa, watasaidia kupunguza tatizo hili.
 
Nasikia haya magugu yalipandikizwa na mtu
 
Mkuu kumbe ndivyo ilivyo eeeh.... Ngoja nikatafute kazi hapo may be nami nitakula walau kwa urefu wa kamba yangu!

Poor Tanzania yangu.........
 
Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…