Ziwa Tanganyika, ni mlango wa Kuzimu

Ziwa Tanganyika, ni mlango wa Kuzimu

Nataka kuwa mwanasiasa, napanga kwenda huko ili wasije wakanichinje kama kuku. Nikitoka huko nitazidi kuzingatia kuwa " maisha ni mchezo".
 
Ziwa Tanganyika linasifika sana kwa urefu Wa kina chake, dagaa watamu wasio na mchanga, samaki aina ya migebuka, meli ya MV Lihemba na fukwe zake nzuri zenye mchanga mweupe zinazozungukwa na milima yenye uoto mbichi Wa kijani kibichi.

Mbali ya sifa hizo pia Ziwa Tanganyika linasifa nyingine tofauti kwenye ulimwengu Wa kiroho. Ziwa Tanganyika ni mlango Wa kuzimu.
Wachawi wote NGULI Wa Sumbawanga, Kigoma na Congo ambayo zamani ilijulikana kama Zaire hutoka katika ziwa hili.

Uchawi Wa Gamboshi umetokea ndani ya ziwa hili. Uchawi Wa Wamanyafu nao mizizi yake ni kwenye hili ziwa.

Ili kuweza kwenda kuzimu unahitajika kuwa na mtaalam mzoefu ambaye atakuombea kibali cha kwenda huko.
Miongoni mwa mahitaji muhimu ya safari yako ni mayai saba viza, mbuzi mweupe au mweusi asiye na doa wala baka lolote, kucha za bundi, manyoya ya shingoni ya kipanga Aziz na vitu vingine utakavyoambiwa na kiongozi wako.
Mv LIEMBA itapendeza zaidi.
Iliunganishwa na mjerumani kabla ya vita vya dunia na wakati wa vita mjerumani akaizamisha kwa kusudi la kuificha, baada ya vita ikaibuliwa ikiwa nzima kabisa, hawa ni watu wenye akili zilizopitiliza! Meli hiyo inafanya kazi mpaka sasa sema tu haiko kwenye mikono salama, sisi ni waharibifu.
 
Back
Top Bottom