Ziwa Natron kutoka Arusha limekuwa makazi ya zaidi flamingio millions 3!

FM facts

Member
Mar 16, 2019
45
88
Sababu Kuu ya Ziwa hili Kuwa na Ndege wengi sana Aina ya Flamingo ni Kwasababu Katika Ziwa hili Kunapatikana Bakteria Wengi sana Wanaozaliana na Hii ni Kutokana na Ziwa Hilo kuwa na Chumvi Nyingi Hivyo Kuwafanya Flamingo Kupata Chakula Kingi cha Bakteria Hapo Pamoja na Wadudu Wengi Wanaokufa Kutokana na Chumvi Nyingi.

Sababu ya Pili ni Kwamba, Kutokana na Ziwa Natron Kuwa na Maji ya Chumvi nyingi Imepelekea Kuwa si Makazi Sahihi ya Wanyama Hatari wa Majini Kama Mamba, Nyoka N.K Hivyo Kuwa Sehemu salama kwa Flamingo Kujinafasi.

Kuna Baadhi ya Miezi Katika Ziwa Hili Huwa kunakua na joto kali Hadi Kufikia Nyuzijoto 60C, Hivyo Kupelekea Maji Kuanza Kuchemka (Ku-Evaporate) na Njia hii ndio Inayofanya Maji Kupungua Katika Ziwa hilo, Kwasababu Maji yanaingia tuu, Hakuna Sehemu Yanapotoka Nje.

Ziwa hili ni Fahari ya Tanzania, Linapatika Arusha Tanzania Kilomita Kadhaa Kutoka Monduli, Maji yake Yanatoka Katika Mto 'Ewaso Ng'iro' Uliopo Kenya na ni Ziwa Namba Moja Afrika Kati ya Maziwa Machache ya Maji Yenye Chumvi Likiwemo Ziwa Magadi Kutoka Kenya.

Ziwa Natron Ndio ziwa Kubwa Zaidi Afrika Kwa Maziwa yenye Maji ya Chumvi, Lina Ukubwa wa 1,040 km² Ambazo ni Karibia na Ukubwa Jiji lote la Dar es Saalam lenye Ukubwa wa 1,590 km² na Kuna Muda Maji ya Ziwa hili Hubadilika Rangi na Kuwa ya Pink! na ni Moja kati ya Maziwa 10 Makubwa Ya Chumvi Duniani.

Ziwa Natron Lina Kina cha Chini ya Futi 10 tuu na ni Moja kati ya Maziwa Maarufu Duniani lakini Watanzania Tunalichukulia Poa

Tufollow Instagram @fm_facts
flamingos.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jana niliona kwenye chaneli ya Tanzania ya utalii kuna miti wanatengeza na juu wameweka sehemu ya kutembelea unawaangalia ndege na chini kuna maji. ni pazuri sana

kitochi
 
Back
Top Bottom