Zitto: Zambia na Congo ndio wanatumia bandari kwa 73% nashangaa reli inapelekwa kusiko na mizigo

Zito ana hoja. Reli ingeenda mpaka mipaka ya Zambia, Kongo, Malawi tungekuwa na uhakika wa kupokea na kusafirisha mizigo ya nchi zote hizi. Na hii ingesababisha mapato ya bandari kuongezeka sana , pamoja na mapato mengine. Na huenda tungeivutia na Zimbabwe pia

Hela ya ujenzi wa reli ingerudi haraka na kutumika Kwa shughuli zingine za maendeleo kama ujenzi wa reli ya kati

Kwa sasa itachukua muda mrefu zaidi kurejesha gharama za ujenzi wa reli hii tunayoijenga.

Safi sana zito Kwa kuliona hili
Mkuu hivi reli ya TAZARA si ipo inahudumia kanda hiyo na pale Mbeya kuna dry port!
 
Jamani tuulizieni, huku kwetu MNAnje nanyumbu sgr inatufikia lini? Itasaidia sana kuturahisishia usafirishaji wa kuipeleka korosho yetu kiwandani India.

Na washawasha!
 
Kama ni hivyo na ulikuwepo kwenye PAC, mbona hukuzungumzia TAZARa ifanye kazi hiyo atleast at 70% kwenda Juu, si ingpunguza malorry au na wewe unapewa % inayolipwa kwa wenye malory? Halafu Kigoma si ni karibu na east congo? au hutaki Kigoma iwe kama Dubai? au tuseme kitovu cha biasha za wa Congo na nchi nyingine jirani.
zitto amewahi kuwa mwenyekiti wa PAC atuambie 73% ni mingapi inaenda zambia na ngapi congo? kwa hiyo ya congo % ngapi inapita rusomo % inapita tunduma na % inapita ujijvinginevyo ni porojo tu,
 
Yaani anaona mizigo ni ya kwenda zambia na kongo tu? Mizigo ya mikoa ya kati magharibi na kanda ya ziwa? Pia rwanda burundi na uganda?
Hizo rwanda na burundi, kama ka wilaya ka kaliua ndo unategemea wapitishe mizigo kwenye reli? Foolish ideas!
 
tuanzie hapa kwani ni wapi kuna watumiaji wengi wa treni,kgm to tabora au mwanza to tabora. Mimi naona hii reli inajengwa kisiasa tu. Mimi naona tunajenga reli kuelekea mwanza kwa lengo la kuua bandari ya kigoma
 
Unasemaje? Umesoma jiografia vzr?
 
tuanzie hapa kwani ni wapi kuna watumiaji wengi wa treni,kgm to tabora au mwanza to tabora. Mimi naona hii reli inajengwa kisiasa tu. Mimi naona tunajenga reli kuelekea mwanza kwa lengo la kuua bandari ya kigoma
Reli ya kati ilianza kujengwa na mjerumani 1905 .Akaimalizia muingereza baada ya vita kuu ya kwanza.
Ilikuwepo tangu enziii. SBB za kiuchumi na kiutawala. Kusafirisha malighafi kutoka bara kuja bandarini DSM. Pamba,chumvi, kahawa,ngombe, katani,
 
Nimeshakupa hiyo mifano, ni kwa nini Mzungu alijenga Reli ktk Mtwara Bandarini kwenda Nachingwea? Au Reli ya Tanga-KLM-Arusha kwa akili yako haikupaswa kujengwa?
Na kama unatumia fedha za nchi yako kujenga Reli kwa ajili ya nchi za kigeni kesho wakigoma kutumia Reli yako nani anatailipia hiyo gharama?

Unajua kwa nini Reli ya tazara imekufa? Kama haujui nitakusaidia, imekufa kwa sababu ilijengwa kwa ajili ya matumzi ya Wachina na Zambia, Wachina walitaka kusafirisha Shaba ktk Zambia kwenda kwao kupitia Bandari yetu, lkn wkt huo nchi ya Zambia ilikuwa na ishu na nchi jirani kama AK, leo hii ishu zimekwisha na nchi ya Zambia pia inatumia bandari za nchi nyingine, na hiyo ndiyo sababu kubwa ya reli ya Tazara kufa,, sasa kama tungukuwa tumeijenga kwa fedha zetu nani angelipa hilo deni?
Barbarosa una hoja ila haujatulia. Tulia utaeleweka na watu watachangia vizuri Ukiwa na mihemuko unakuwa unstable na ingekuwa ni ngumi ungepigwa hata na mtoto. Reli Nachingwea Mpaka Mtwara tayari wazungu waliangalia soko la nje kwani mizigo ikifika mtwara tayari imefika kwenye soko lolote duniani kupitia bahari ya hindi. The same applies to Arusha Moshi Tanga access na mataifa mengine ni bahari.
 
Ndiyo wachumi wetu wa daraja la kwanza...na bado unasikia wanapuuzia mikakati ya rais kunusuru uchumi wetu! Nuru ya chama cha ACT inafifia kifikira...! Yaipasa kusisimuliwa iweze kutoa mwanga mkali bila mawaa!
 
Mama Anna Ngwira bora ajirudie zake ccm tu,
 
tuanzie hapa kwani ni wapi kuna watumiaji wengi wa treni,kgm to tabora au mwanza to tabora. Mimi naona hii reli inajengwa kisiasa tu. Mimi naona tunajenga reli kuelekea mwanza kwa lengo la kuua bandari ya kigoma
Fallacy argument
 
Hamuwezi kumuelewa Zito ,hoja yake inamashiko sana katika ujenzi was uchumi imara.Reli kwa ajili ya social service ingeweza kujengwa kwa pesa ya ndani ambayo ingepatikana kutokana na ongezeko la mapato ambayo tungepata baada ya kuboresha Zambia - Congo line.
Zito hapendi rwanda na hampendi kabisa kagame hilo liko wazi sio siri. Nadhani zitto atakuwa mhutu mwenye msimamo mkali aliyezaliwa na aliyekulia Tanzania
 
Back
Top Bottom