Zitto: Uuzaji benki ya NBC ulifanywa ovyo ovyo

Zitto: Uuzaji benki ya NBC ulifanywa ovyo ovyo

Magazetini

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2014
Posts
593
Reaction score
1,713
Zitto-29June2015.jpg

Kiongozi Mkuu wa chama hicho, Zitto Kabwe

Chama cha ACT-Wazalendo kimesema ili nchi iweze kujitegemea kiuchumi ni lazima benki kubwa zimilikiwe na Watanzania tofauti na ilivyo hivi sasa kwa benki hizo kumilikiwa na wageni huku ikitaka Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) irejeshwe kwa Watanzania.

Hayo yalisemwa mwishoni mwa wiki wilayani Muheza mkoani Tanga na Kiongozi Mkuu wa chama hicho, Zitto Kabwe katika mkutano wa hadhara.

Alisema utaifishaji wa mabenki uliofanyika mwaka 1967 na kuundwa kwa NBC, Benki ya Nyumba na Benki ya Maendeleo Vijijini ilikuwa ni maamuzi ya msingi kwa maendeleo ya nchi.

Alisema ubinafsishaji wa NBC na kuuawa kwa Benki ya Nyumba ilikuwa ni maamuzi yasiyo na msingi hali ambayo haijawahi kutokea katika nchi baada ya kupatikana uhuru.

Alibainisha kuwa malengo ya kujenga uchumi shirikishi wenye uhuru mkubwa katika soko la mitaji hayawezi kufikiwa bila ya kuwa na benki zinazomilikiwa na Watanzania wenyewe.

Alisema Chama cha ACT-Wazalendo kitahimiza. NBC kurejeshwa kwenye mikono ya Watanzania kwa kumilikiwa na serikali kwa asilimia 50, wananchi na taasisi za wananchi kupitia soko la mitaji nusu iliyobakia.

"Ubinafsishaji wa NBC ulifanywa holela na benki iliuzwa kwa bei ya kutupwa kimsingi, msimamo huu wa ACT -Wazalendo unaungwa mkono na kazi iliyofanywa na kamati ya Bunge ya PAC iliyoagiza ukaguzi maalumu kwenye mchakato wa ubinafsishaji wa Benki hiyo na hata Mwalimu Nyerere alikufa na kinyongo cha Benki hii," alisema Kabwe.

Alisema wakati NBC ikiwa inaendelea na shughuli zake kulitokea hasara ya dola za Kimarekani milioni 143 zilizotokana na mikopo iliyotolewa kwenye sekta ya usafirishaji.

Alisema mikopo hiyo ilikuwa ya kitapeli na serikali ilifidia hasara hiyo kwa kulipa nyongeza ya mtaji katika benki sawa na kulipia hasara ambayo waendeshaji wa benki hiyo waliifanya.

CHANZO: THE GUARDIAN
 
Media Tycoon, this guy is coming after you sasa. Kwenye hili lazima atakuchimbua na utapatikana, Watch out
 
Wakati mwengine lengo lake ni kufurahisha umati tu na ahadi zake zisizo tekelezeka bila hata ya kujua gharama halisi ya thamani za share zinazomilikiwa na kama serikari inaweza nunua let alone kuliendesha shirika la benki, ambapo wanadaiwa kila kona kwenye taasisi ya fedha,

Uwezi kuwaambia watu waendeshe benki bila ya kuwaambia kwanza wapunguze kukopa huko, hivi ata amefuatilia historia ya banking sector prior to privatizations na sababu zilizoua benki nyingi na kama tabia ya serikari imebadilika.
 
Analalamika nini wakati maswahiba wake ni ccm hao hao waliouza benki hiyo !
 
Akielezea kasoro alizoziona katika zoezi la ubinafsishaji lililofanyika wakati wa serikali ya Mkapa, Zitto Kabwe ametoa mifano mitatu iliyomtoa machozi akiwa mwenyekiti wa PAC.

1. NBC iliuzwa kwa tsh 15 bil huku ikiwa na tsh zaidi ya 100 bil katika akaunti zake. Tena na Majengo karibu nchi nzima.

2. Bodi ya Korosho iliuza kiwanda kwa mwekezaji ambacho hadi wanaenda kukagua mashine zilikuwa haxijawahi kuwashwa.

3. Serikali iliuza mashamba ya mpunga huko Kapunga Rice Project takribani hekta zake 4000 lakini wakajumlisha na hekta 500 za Kijiji kinyume cha sheria.

Zitto Kabwe amesema Azimio la Arusha ni muhimu hadi sasa japo linahitaji marekebisho ya hapa na pale.

Kabwe alikuwa akiongea kwenye kumbukizi la Mwalimu Nyerere.

Source: ITV

Maendeleo hayana vyama!
 
And now we are in Ubinafsishaji 2.0...,

Yajayo Yanatisha.
 
Azimi

Azimio la arusha linatatuaje yaliyoainishwa kama matatizo hapo juu? By the way si ACT walishakuja na azimio la Tabora? Au tunahitaji azimio jipya?
 
Mkapa ndie alianzisha matatizo yanayoligharimu taifa leo hii, huu upigaji uliotamalaki kila kona serikalini architect wake alikuwa Mkapa.

Hili lilianzia kwenye sera mbovu za ubinafsishaji, viongozi wakaanza kubinafsisha vitu kiholela bila kujali thamani yake ilimradi wao wapate chochote kutoka hapo.

Matokeo yake ndio 10% ikazaliwa, hii ikasambaa kwenye miradi mingine ikiwemo uchimbaji madini, viongozi wa CCM wakaigeuza nchi yetu shamba la bibi wakaanza kuitoa bure bila kujali umasikini uliotamalaki.

Mpaka leo bado tunalia na upigaji unaoendelea kufanywa huko serikalini kama Escrow, na miradi mingine wanayoingia na wazungu wasiyotaka kuweka mikataba yake wazi, ni wizi tu umetawala vichwa vya watawala wetu.
 
Akielezea kasoro alizoziona katika zoezi la ubinafsishaji lililofanyika wakati wa serikali ya Mkapa, Zitto Kabwe ametoa mifano mitatu iliyomtoa machozi akiwa mwenyekiti wa PAC.

1. NBC iliuzwa kwa tsh 15 bil huku ikiwa na tsh zaidi ya 100 bil katika akaunti zake. Tena na Majengo karibu nchi nzima.

2. Bodi ya Korosho iliuza kiwanda kwa mwekezaji ambacho hadi wanaenda kukagua mashine zilikuwa haxijawahi kuwashwa.

3. Serikali iliuza mashamba ya mpunga huko Kapunga Rice Project takribani hekta zake 4000 lakini wakajumlisha na hekta 500 za Kijiji kinyume cha sheria.

Zitto Kabwe amesema Azimio la Arusha ni muhimu hadi sasa japo linahitaji marekebisho ya hapa na pale.

Kabwe alikuwa akiongea kwenye kumbukizi la Mwalimu Nyerere.

Source: ITV

Maendeleo hayana vyama!
Hawa wanasiasa wanachezea na kuchanganya akili za watu kweli kweli!

Kwa nini anayazungumzia haya mambo wakati huu, ambapo tunajiandaa kunadiwa?
 
Mkapa ndie alianzisha matatizo yanayoligharimu taifa leo hii, huu upigaji uliotamalaki kila kona serikalini architect wake alikuwa Mkapa.

Hili lilianzia kwenye sera mbovu za ubinafsishaji, viongozi wakaanza kubinafsisha vitu kiholela bila kujali thamani yake ilimradi wao wapate chochote kutoka hapo.

Matokeo yake ndio 10% ikazaliwa, hii ikasambaa kwenye miradi mingine ikiwemo uchimbaji madini, viongozi wa CCM wakaigeuza nchi yetu shamba la bibi wakaanza kuitoa bure bila kujali umasikini uliotamalaki.

Mpaka leo bado tunalia na upigaji unaoendelea kufanywa huko serikalini kama Escrow, na miradi mingine wanayoingia na wazungu wasiyotaka kuweka mikataba yake wazi, ni wizi tu umetawala vichwa vya watawala wetu.
Kuna jambo la kujiuliza pia juu ya hii mali iliyogawiwa kwa bei chee.

Urusi nao walipitia hali kama hii, ndiyo ikawa mwanzo wa 'Oligarchy'. Wao angalau waliouziwa kwa bei chee, waliyatumia waliyouziwa kuzalisha mali na kuleta faidi kwa nchi ya Urusi.

Sisi mbona hawa waliouziwa waligeuza mali walizouziwa kuwa maghala, na kung'oa mashine kabisa? 'Oligarchy' wetu ni akina nani, Mo, Bakhresa, Rostam Azizi...?
 
Yes, "oligarchy" wetu ni hao uliowataja na wamepewa support kufanikisha malengo yao kupitia "system" waliyopo.

Kati ya hao uliowataja ukijaribu kuchunguza namna walivyoanza kupata mali zao utakuta wapo waliouza meno ya tembo, kukwepa kodi kwenye biashara zao, nk. na hii ni kupitia mahusiano yao na system waliyopo.

Kuhusu kwa nini Urusi wanafanikiwa sisi tunafeli ni mindset, povetry, umasikini umetutawala sana kuanzia wa kipato mpaka wa fikra. Hawa jamaa zetu japo wana mali lakini ukiangalia karibu yao wamezungukwa na nani utakuta ni familia zao, na ndugu na kidogo rafiki wa karibu.

Umasikini wa kipato nao unasababisha maendeleo kukwama, ndio unakutana na hizo 10% serikalini, na ajira za upendeleo zisizojali elimu, matokeo yake tunaishia kubakia na maghala na kun'gofoa hadi mashine kama ulivyosema, ilimradi kila mmoja kwenye "system" aambulie chochote.

Wakati wale kina Abramovich, Alisher Usmanov, Farhad Moshiri, na wengine ukiwatazama wametapakaa uwekezaji wao mpaka nje ya nchi zao, kote huko wanatengeneza mali kwa ajili ya nchi zao, sisi hapa kwetu hata wakitoka nje ya nchi wakawekeze, ujue wakirudi ndani watakwepa kulipa kodi kupitia "system", ujinga mtupu!.
 
Back
Top Bottom