Zitto: Ufisadi ni agenda endelevu

Zitto: Ufisadi ni agenda endelevu

Nashangaa ktk nyuzi hizi wanazi wa Zitto hawasogei kutwa kuhangaika na UKAWA!!

Hata TVs sioni coverage yake... JF wana ACT wamemtelekeza kabisa mama Mghwira!!!

CC: MOTOCHINI Mkandara Kimweri
Unataka sisi tuseme nini? Mama Mgwira atajiuza mwenyewe kisiasa hatuwezi kumwekea maneno mdomoni. Uwezo wake mtaupima nyie wananchi wapiga kura, sisi tunachoweza kuzungumzia ni sera na mwelekeo wa ACT kama chama kilichobakia na dira ile ile ya mageuzi ya kifikra kupambana na UFISADI ambao ndio chachu ya maendeleo ya nchi yetu...

Hakuna mtu anayehangaika na UKAWA isipokuwa tunawaambia wananchi (sio UKAWA) tofauti baina ya chama kinachotaka kuleta mabadiliko nchini na chama ambacho kinaweka nguvu kubwa kuiondoa CCM madarakani kama ndio mabadiliko tayari hayo mengine yatajulikana huko mbele ya safari. Siwezi kutetea Upumbavu na Ulofa huo wa mabadiliko ni kuindoa CCM IKULU kuwa ndio mabadiliko wanayoyahitaji wananchi.

Mimi naamini ari ya kutaka mabadiliko inatokana na mageuzi ya kifikra kwanza kwa wananchi wenyewe kuwapa uwezo wa kuchambua pumba ndani ya mchele, uwezo wa kutambua kwamba mabadiliko ni matunda (results) ya uwekezaji wao na sio mtaji wa UKAWA kuingia IKULU. Kutambua kwamba siasa za UKAWA ni za kuelekea magogoni tu, sio siasa za kuijenga nchi ili mabadiliko yatokane na ridhaa yenu..wao wanadia mabadiliko hayo yatajulikana mbele ya safari.. Ahadi kama hizi sintozikubali asilan.

Aloandika ya Zitto hapo juu ndio msimamo wangu miaka yote kifikra maana ndio uhalisia uliopo, na sintoweka tumaini wala kuamini kwamba Tanzania inaweza kupata maendeleo kwa kuweka nguvu kubwa kuendelea kujaza maji ndoo ilotoboka!. Hata kama tuwe na mafuta, gas, Utalii na maliasili za kila namna, lakini maadam kama hatutatambua kwamba rasilimali kubwa ya nchi hii ni sisi wananchi wenyewe na kuwapa uwezo wa kutambua nafasi yao katia jamii tukawaachia MAFISADI waendelee kuweka mirija yao na kunyonya Uchumi wa taifa hili, basi watanzania wataendelea kuwa maskini hadi watie Akili. Utajiri ni matokeo ya uwekezaji kwa wananchi wenyewe.

Mimi nayaenzi maneno ya mwalimu hayati Nyerere alipokuja kututembelea hapa mwaka 1997 na sintosahau usia wake. Katika hotuba yake alisema wazi kwamba Tanzania haiwezi kuendelea hata tukivumbua mafuta ikiwa viongozi wake wamegubikwa na kashfa za RUSHWA...Na maneno yake yameendelea kuthibitika kila siku ya utawala na siasa za Bongo.
 
Back
Top Bottom