nngu007
JF-Expert Member
- Aug 2, 2010
- 15,860
- 5,803
MJADALA kuhusu hatma ya kampuni ya Meremeta iliyokuwa inamilikiwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) sasa utarejeshwa tena bungeni katika kikao cha Bunge linaloanza Aprili mwaka huu mara baada ya Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali kukamilisha uhakiki wa hesabu za matumizi ya kampuni hiyo.
Maelekezo ya Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma, Zitto Kabwe, yamethibitisha hivyo.
Meremeta ni moja ya makampuni yaliyotuhumiwa na Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willbrod Slaa, kwamba yalifanya wizi mkubwa wa fedha za umma lakini Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, katika Bunge lililopita alizima mjadala juu ya suala hilo akidai kuwa hiyo ilikuwa ni kampuni ya jeshi na kwamba masuala yanayogusa usalama wa nchi hayawezi kujadiliwa hadharani.
Hata hivyo, Pinda alionekana dhahiri kuwa alikuwa akificha ukweli.
Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC), Zitto Kabwe (CHADEMA), alisema kamati yake imeitaka ofisi ya Msajili Hazina kuhakikisha inatoa ushirikiano kwa CAG ili kukamilisha utarabu wa kufanya hesabu maalum kwa kampuni hiyo kwa haraka.
Alisema kamati yake ilitoa maagizo kwa CAG kufanya kazi ya ukaguzi lakini kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa katika taarifa yake Msajili Hazina hajatoa ushirikiano wala majibu juu ya hatua hiyo.
Kufuatia hali hiyo kamati hiyo imelazimika kutaka maelezo ya kina kwa nini hesabu hizo hazijakalimika kwa mujibu wa sheria.
Tunahitaji Bunge la Aprili suala la Meremeta liwe limekwisha na kama serikali haitaki kufanya hivyo kupitia kamati yetu tutawaeleza wananchi nini kinachoendelea, Bunge ni chombo chenye mamlaka ya kuisimamia serikali kwa asilimia mia moja
Tunahitaji mgodi wa Buhemba, wapewe Stamico lakini kwa sasa huwezi ukawakabidhi kitu ambacho hakijafanyiwa uhakiki wa hesabu zake kwa Meremeta serikali ilikuwa ikimiliki hisa asilimia mia moja, alisema Zitto.
Kampuni ya Meremeta, ambayo inadaiwa haijasajiliwa chini ya Ofisi ya Hazina kama kampuni au shirika, ilichota malipo tata zaidi ya sh bilioni 215 zilizolipwa na Benki Kuu (BOT) kwa Kampuni ya Nedcor Trade Service, baada ya udhamini wa kampuni yenye hisa ya Triennex (PTY) limited ya Afrika Kusini.
Hata hivyo, alisema kamati hiyo inahitaji kufahamu hatma ya uuzwaji wa hisa za kampuni ya Zain kwenda kampuni ya simu ya Airtel.
Alisema kwa mujibu wa maelezo inaonyesha kuwa kuuzwa kwa kampuni hiyo serikali haijanufaika kupata kodi na kuhitaji maelezo ya kina ya Msajili wa Hazina, Kamishna wa TRA.
Hisa za Zain zimeuzwa lakini hakuna kodi iliyongia serikalini sasa tunahitaji kupata ufafanuzi wa kina juu ya hali hii kwani ili nchi iweze kujiendesha sio kufanya ujanja; kinachotakiwa Airtel ni kulipa kodi tu, alisema Zitto.
Alisema katika kuhakikisha wanasimamia hilo kamati yake imeazimia siku ya Ijumaa kukutana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Ramadhan Kijah, Kamishna Mkuu wa TRA, Hanry Kitilya, na Msajili Hazina.