Mgombea Ubunge Jimbo la Kigoma Mjini kupitia Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe, amesema chama hicho kitafanya kampeni katika kila kona ya nchi endapo Mahakama Kuu itatoa maamuzi yatakayoruhusu Luhaga Mpina kugombea urais kwa tiketi ya chama hicho
Akizungumza Oktoba 6, 2025 katika mkutano wa kampeni uliofanyika Kata ya Katanga, Jimbo la Kakonko mkoani Kigoma, alipokuwa akimnadi mgombea ubunge wa chama hicho katika jimbo hilo, Olaf Kaboboye, Zitto alisema wapo tayari kuingia barabarani mara tu watakaporuhusiwa na mahakama
“Hata kama itabaki wiki moja ya kampeni, tukiruhusiwa kugombea, tutapiga jaramba kila kona ya nchi hii, tutashinda na kuing’oa CCM madarakani,” alisema Zitto
Aliongeza kuwa endapo chama hicho hakitashinda mahakamani, kitatoa maelekezo kwa wananchi kuhusu namna watakavyopiga kura katika nafasi ya urais
Mnamo Septemba 15, 2025, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Johari Hamza, aliwasilisha pingamizi dhidi ya Mgombea Urais wa ACT Wazalendo, Luhaga Mpina, hatua iliyosababisha Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) kumtoa kwenye kinyang’anyiro cha urais