Supreme Leader na image ya ACT akiwa Shinyanga alipandikiza chuki kali kati ya wana kanda ya ziwa na wana kaskazini hususani Arusha na K.njaro.Akahubiri kuwa mikoa ya kanda ya ziwa ina mchango mkubwa kwenye pato la taifa lakini hakuna maendeleo kwa sababu ya mgao hafifu tofauti na Kilimanjaro na Arusha ambao wana maendeleo lakini mchango wao ni mdogo kwenye pato la taifa.Sasa Zito Kabwe awaeleze wananchi Kigoma inachangia
kiasi gani pato la taifa na
akishamaliza atuambie kama
maendeleo ya Kigoma
aliyojitapa nayo ya barabara,
gati lake Tanganyika, umeme,
uwanja wa ndege, daraja la
Malagarasi na miradi mingine
mingi Kikwete aliyowapeleka
Kigoma kwa kuupea kipaumbele
ni halali mpaka kuyatungia
wimbo!
Na kwanini anataja Kilimanjaro
tu.c.c Nguruvi3 Geza Ulole
Mwanasiasa mahiri na mbunge aliyestahili kuitwa mbunge taifa kwa kuwatetea watanzania wote wa mikoa yote,
Kama Shinyanga na Arusha kwenye madini yao, Mwanza na pamba yao, Tabora na Tumbaku yao, Kilimanjaro na kahawa yao na mikoa ya kusini kwa korosho yao.
mikoa yote hiyo alijitahidi kuibana serikali iboreshe maisha ya wananchi kupitia shuguri zao za kila siku za kujipatia riziki na kupelekea kutungwa sheria mpya ya madini leo hii unaulizia alichokifanya?
Kweli nimeamini chuki hupofusha macho.
Wananchi wa kigoma hawahitaji hata kukumbushwa akichokifanya zito kwa mkoa wa kigoma
Kwa mkazi yeyote wa kigoma hata umwamshe usingizini atakwambia mazuri mengi ambayo zito ameufanyia mkoa wa kigoma na kuuletea heshima kubwaKila mwanakigoma leo anajivunia kusema mimi ni mutu wa kigoma popote pale alipo tofauti na ilivyokuwa hapo kabla.
Wakazi wa kigoma mjini chonde chonde msifanye makosa hapo mwezi wa kumi turudishieni jembe letu ZITO ZUBERI KABWE bungeni.
Last edited by a moderator: