Zitto ndo Rais wa Ukawa 2015

Zitto ndo Rais wa Ukawa 2015

NAMTUMBA

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2014
Posts
1,939
Reaction score
600
1. Anasifa 100%, ni chaguo la wengi.
Kwasasa katiba ya Chadema inamruhusu kuomba upya uanachama na atapokelewa na akawania kiti cha urais 2015. Hana sababu yakulaumu mtu yoyote ndani ya chama kwa sababu yeye mwenyewe ndo amejifukuza na uongozi wa chama umetekeleza majukumu yake kwa mujibu wa katiba.

2. Asirubuniwe na upepo wa ACT. Zitto asijiongopee kwamba anaweza kufanya makubwa ndani ya ACT kwakuwa siasa za Tanzania bado ni changa sana. Kujiunga ACT kwa sasa kujimaliza kisiasa wakati bado taifa linahitaji mchango wake katika harakati za ukombozi mpya wa Tanzania. Kwa ushauri wa bure ambao nampa huyu mtoto wetu ni kwamba kama anaipenda siasa arudi nyuma, aombe msamaha, pia aombe uanachama upya lakini kama anahisi hawezi kukaa Chadema aombe uanachama ndani ya chama chochote kinaunda umoja wa UKAWA ili ndoto zake zakuwa rais kijana zitimie na naamini anaweza kushinda nafasi hiyo.

3. Zitto lazima akubali kwamba Chadema sio wajinga na hawajamtimua kwa bahati mbaya. Zitto aache utoto. Asijione yeye ni bora kuliko chama, lakini pia Chadema wasijione kwamba wao ni maarufu bila uwepo wa wanasiasa maarufu kama zitto. Ili chama kiwe na nguvu kinahitaji watu wenye mvuto na wanaokubalika katika jamii. Jambo la msingi hapa Chadema na Zitto wakae vikao vya siri kulimaliza swala hili.

4.Mbowe na Dr. Slaa musijifanye Mungu watu. Muwe na tabia ya usikivu hata kama kwa unafiki. Ninyi ni akina nani musiokosea, hamutaki kukosolewa, Munavimba vichwa kwa sifa zakijinga. Tunaamini mchango wenu unahitajika sana lakini hebu mujitazame kwenye hizo nafasi munazozikalia kifalme je hakuna wanachadema wengine wanaweza kuongoza zaidi yenu. Wapo watu wanauwezo mkubwa kuliko ninyi hi yo linapokuja swala la uchaguzi ndani ya chama muwe tayari kukubali chaguo jipya la wananchi. Nawashauri Mbowe na Dr. Slaa mujichunguze kwa hili, taifa linawahitaji sana lakini muwe wasafi kwanza kabla hamujawachafua wengine.

5. Nafasi ya urais ndani ya Ukawa. Chadema muwe tayari kukubali mgombea kutoka chama kingine, musitake advantage ya uingi wenu kujiona ninyi ndo munastahili kupewa kiti cha urais. Kwakuwa tumeamua kuungana kuiondoa ccm basi muungano wetu uwe na tija isiwe danganya toto. Na kama Chadema mutachagua mgombea wenu wa urais sio lazima awe Dr. Slaa, munaweza kuweka mtu mwingine yoyote.
 
Attachments

  • IMG_20150311_131900_1.jpg
    IMG_20150311_131900_1.jpg
    421.4 KB · Views: 405
  • IMG_20150311_131952_1.jpg
    IMG_20150311_131952_1.jpg
    451.3 KB · Views: 356
  • IMG_20150311_132555_1.jpg
    IMG_20150311_132555_1.jpg
    483.3 KB · Views: 333
  • IMG_20150311_132559_1.jpg
    IMG_20150311_132559_1.jpg
    482.8 KB · Views: 344
1. Anasifa 100%, ni chaguo la wengi.
Kwasasa katiba ya Chadema inamruhusu kuomba upya uanachama na atapokelewa na akawania kiti cha urais 2015. Hana sababu yakulaumu mtu yoyote ndani ya chama kwa sababu yeye mwenyewe ndo amejifukuza na uongozi wa chama umetekeleza majukumu yake kwa mujibu wa katiba.

2. Asirubuniwe na upepo wa ACT. Zitto asijiongopee kwamba anaweza kufanya makubwa ndani ya ACT kwakuwa siasa za Tanzania bado ni changa sana. Kujiunga ACT kwa sasa kujimaliza kisiasa wakati bado taifa linahitaji mchango wake katika harakati za ukombozi mpya wa Tanzania. Kwa ushauri wa bure ambao nampa huyu mtoto wetu ni kwamba kama anaipenda siasa arudi nyuma, aombe msamaha, pia aombe uanachama upya lakini kama anahisi hawezi kukaa Chadema aombe uanachama ndani ya chama chochote kinaunda umoja wa UKAWA ili ndoto zake zakuwa rais kijana zitimie na naamini anaweza kushinda nafasi hiyo.

3. Zitto lazima akubali kwamba Chadema sio wajinga na hawajamtimua kwa bahati mbaya. Zitto aache utoto. Asijione yeye ni bora kuliko chama, lakini pia Chadema wasijione kwamba wao ni maarufu bila uwepo wa wanasiasa maarufu kama zitto. Ili chama kiwe na nguvu kinahitaji watu wenye mvuto na wanaokubalika katika jamii. Jambo la msingi hapa Chadema na Zitto wakae vikao vya siri kulimaliza swala hili.

4.Mbowe na Dr. Slaa musijifanye Mungu watu. Muwe na tabia ya usikivu hata kama kwa unafiki. Ninyi ni akina nani musiokosea, hamutaki kukosolewa, Munavimba vichwa kwa sifa zakijinga. Tunaamini mchango wenu unahitajika sana lakini hebu mujitazame kwenye hizo nafasi munazozikalia kifalme je hakuna wanachadema wengine wanaweza kuongoza zaidi yenu. Wapo watu wanauwezo mkubwa kuliko ninyi hi yo linapokuja swala la uchaguzi ndani ya chama muwe tayari kukubali chaguo jipya la wananchi. Nawashauri Mbowe na Dr. Slaa mujichunguze kwa hili, taifa linawahitaji sana lakini muwe wasafi kwanza kabla hamujawachafua wengine.

5. Nafasi ya urais ndani ya Ukawa. Chadema muwe tayari kukubali mgombea kutoka chama kingine, musitake advantage ya uingi wenu kujiona ninyi ndo munastahili kupewa kiti cha urais. Kwakuwa tumeamua kuungana kuiondoa ccm basi muungano wetu uwe na tija isiwe danganya toto. Na kama Chadema mutachagua mgombea wenu wa urais sio lazima awe Dr. Slaa, munaweza kuweka mtu mwingine yoyote.

Ukawa ipi? au kuna ukawa nyingine Zambia? maana nimesikia Raisi wao ni mgonjwa
 
Mnashauri sana hadi kinyaaa

Mnadhani zito ni mtoto asiyejua anachokifanya

By the way katiba ya Tanzania haimruhusu kwa sababu ya Umri
 
Sina uhakika, but wanavyomfanya huyo kijana sivyo;

Ifike mahali tufahamu kuwa siyo kila anayeimba wimbo wetu tupo naye njia moja;
Hata kama alikosea hata hivyo hajamfikia yule mlinzi wa Dr.

Mamndenyi

Kwani atakuwa amefikisha ule umri uliopo kisheria?
 
paleka huko halizako vyama vyote vinavyo unda ukawa vimetangaza wagombea uraisi bado chadema tu ndiko amefukuzwa jeitakuaje
 
Sina uhakika, but wanavyomfanya huyo kijana sivyo;

Ifike mahali tufahamu kuwa siyo kila anayeimba wimbo wetu tupo naye njia moja;
Hata kama alikosea hata hivyo hajamfikia yule mlinzi wa Dr.

Mamndenyi mimi mwenyewe kabla sijafahamu kiuhakika kuhusu huyu bwana nilikua namwonea huruma

Lakini laiti ungejua true colors zake ungeipongeza chadema

Hivi unajua aliunda chama ndani ya chama.

Na ACT ni ya kwake tangu kusajiliwa hadi sasa
 
Uko sahihi kabisa kama hii hapa

IMG-20150225-WA0003.jpg
 
Last edited by a moderator:
Hakuna aliyekamilika,
Kila kitu kinamapungufu yake;
Huoni hata watoto wanamwondoa mzazi ili warithi mali?
Mamndenyi mimi mwenyewe kabla sijafahamu kiuhakika kuhusu huyu bwana nilikua namwonea huruma

Lakini laiti ungejua true colors zake ungeipongeza chadema

Hivi unajua aliunda chama ndani ya chama.

Na ACT ni ya kwake tangu kusajiliwa hadi sasa
 
Mkuu haya mambo ya umri yaliwekwa na wazee ili kutunyima haki zetu. Kama anafaa ni anafaa tu hata akiwa 18yrs poa tu.
NAMTUMBA

Sijasema hafai bali katiba nadhani ndiyo haifai, tupigane tupate katiba ya wananchi na sio katiba ya majoka yenye makengeza
 
Last edited by a moderator:
NAMTUMBA

Sijasema hafai bali katiba nadhani ndiyo haifai, tupigane tupate katiba ya wananchi na sio katiba ya majoka yenye makengeza

Yes, na ndo maana hata maasikofu wanashauri tuikatae ili tupate muda wakutosha wakuandika katiba safiiii.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom